LGE2024 Dodoma: RC Senyamule apiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa

LGE2024 Dodoma: RC Senyamule apiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepiga kura katika kituo cha shule ya msingi Dodoma Mlimani iliyopo Mtaa wa Salmini kata ya Tambukareli.
IMG_1021.jpeg

Baada ya kupiga kura amezungumza na Waandishi wa habari ambapo amewahimiza wakazi wa Dodoma kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ambae pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Dkt. Frederick Sagamiko amekuwa wa kwanza kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Dodoma Mlimani kilichopo mtaa wa Salmini kata ya Tambukareli.

Dkt. Sagamiko, amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura kutimiza haki yao ya Kikatiba.

Aidha, Wananchi wa mtaa wa Relini kata ya Kizota Dodoma wamepiga kura na kuwaasa wananchi wengine kujitokeza kupiga kura ili kuweza kupata Viongozi bora.

Wakizungumza na Dodoma FM/TV wameeleza kuwa wametimiza haki yao kikatiba na watasubiri mpaka watahakikisha wanapata matokeo.
 
Back
Top Bottom