Serikali ya awamu ya tano ya Hayati Magufuli twajua iliasisi miradi mingi ktk maeneo mbalimbali ya nchi,mfano bwawa la mwal. Nyerere,reli ya mwendo Kasi (SGR) ,barabara za njia nane,ringroads na miradi mingine mingi.
Miradi hii kiukweli ilileta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya miji na vijiji,na kuleta mvuto wa miji maeneo ambayo miradi hiyo ilipita.
Baada ya kifo Cha Hayati Magufuli, aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kuna mijadara mingi mitaani kuhusu kuendelezwa kwa hii miradi,katika pitapita nikakutana na hili la kusitishwa kwa ujenzi wa ringroad ya kati ya jiji la Dodoma ambayo ilipotia maeneo ya mtaa wa Nkuhungu
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma amesitisha ujenzi wa ringroad hiyo na kuwaruhusu wananchi waendelee na shughuli zao za ujenzi kama kawaida, hii ni baadhi ya miradi ambayo iliasisiwa kipindi Cha Hayati Magufuli enzi za uhai wake ktk kulifanya jiji la Dodoma kuwa na muonekano mzuri na uliopangika vizuri.
Kwasasa mitaani watu wanajasili je hii miradi iliyoasisiwa na Hayati Magufuli itakamiika kweli!? au ndo hivyo tena itabaki hadithi ilisiyokuwa na mwisho!
Japo kuna siku nilimsikia Waziri Mkuu aliwatoa wasiwasi watanzania kwa kusema , watu waondoe mashaka miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Serikali ya tano yote itakamilishwa kwa muda uleule uliokuwa umekadiliwa awali enzi za uhai wa Hayati Magufuli.
Je, ilikuwa ni kuwatuliza watu pressure za mashaka au ! Kama hii miradi midogo imeanza kusitishwa mdogomdogo je hii mingine ya mabilioni ya pesa itakuwaje? Anyway ngoja tuone mambo yatakuwaje, ila wananchi tukeyatunza maneno ya Waziri Mkuu kwenye kumbukumbu zetu, alitutia moyo na kutuondoa mashaka kwamba miradi yote iliyoasisiwa na Serikali ya awamu ya tano itakamilika.
Waziri Mkuu tunakumbuka maneno yako,ipo siku tutataka utupe maelezo ,ilikuwaje?