Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Siyo kazi rahisi,miji inaweza kukua lakin lazima iwe na Business Potentials. Nimewahi kuishi Dodoma,hauna mazao makubwa ya kilimo kama ilivyo Mbeya,haina Bandari,haina Ziwa. Ni land locked area.
Mfano mmoja ni Abuja na Lagos. Pamoja na Serikali kuhamia Abuja,bado Lagos iko juu mara 18 ya Abuja kwa kila kitu. Sema miji mikubwa mipya huwa imepangwa ikapangika,inavutia. Kwa hiyo Dodoma haitaweza kirahisi kuipita hata Mwanza,sisemi Dar es Salaam Nairobi au Mombasa! Siyo jambo rahisi,ingawa unaweza kupangika kisasa lakini hadhi ya kuizidi N'bi,M'mbasa au Dar bado kidogo. Kwa sababu unapotoa masterplan hizo za kisasa kwa Dodoma,tambua basi hata Dar wanatoa mpya,Mtwara,Mbeya,Mombasa,Kampala,Kisumu,Arusha,Nakuru,Morogoro nk.