Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Kutoka katika Ukumbi wa JKCC uliopo jijini Dodoma, mawakili wa Tanzania Bara wamekusanyika kwa ajili ya zoezi muhimu la kupiga kura kuchagua Rais, Makamu wa Rais, na viongozi wengine wa Chama cha Mawakili Tanzania bara(Tanganyika Law Society - TLS). Matokeo ya uchaguzi huu yanatarajiwa kutolewa leo mchana.
Hata hivyo, hali ya sintofahamu imeibuka miongoni mwa wapiga kura kutokana na mfumo wa "Mjue Wakili" almaarufu kama E-Wakili kushindwa kufanya kazi. Hali hii imeleta wasiwasi kuhusu uwepo wa mamluki, mawakili wasio huisha (renew) leseni hasa mawakili wa serikali, ambao inaaminika wameletwa na baadhi ya wagombea ili kuhujumu wapinzani wao.
Ikumbukwe kuwa ni mawakili wa kujitegemea walio huisha lesini zao za uwakili pekee ndiyo wenye haki na ruhusa ya kupiga kura katika uchaguzi wa TLS, hivyo kutopatikana kwa mtandao wa E-Wakili kunaleta changamoto kubwa ya kuthibitisha uhalali wa wapiga kura.
Kwa taarifa zaidi nitawafahamisha wakuu.
PIA FATILIA: LIVE: Uchaguzi Wa Rais TLS: Nani Kuibuka Kidedea Urais TLS