KERO Dodoma: Wakazi wa mtaa wa Mapinduzi, Makulu Oysterbay hatuna maji takriban miezi miwili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari JamiiForums, mimi ni mkazi wa Dodoma, Makulu Oysterbay mtaa unaitwa Mapinduzi. Ni miezi miwili sasa maji hajawahi kutoka hata tone maji na hamna taarifa yoyote wala tahadhari na ni hali ambayo imekuwa inatokea mara kwa mara bila maelezo yoyote.

Tumeshafika kwenye ofisi za wahusika na kulalamika lakini hamna kilichobadilika mpaka hivi sasa.

Tunaomba JamiiForums mtusaidie kuchapisha taarifa wakazi wa Mapinduzi tunaomba mamlaka nyingine kuingilia na kuiwajibisha DUWASA kwa uzembe huu hasa hasa ofisi za Waziri wa Maji.

Mwisho naambatanisha nyaraka zote ambazo suala hili limekuwa likifuatiliwa tokea mara ya mwisho maji kutoka ambapo ilikua kati ya september 8-10 hivi

 

Attachments

Watani zangu wagogo kuhusu maji ongeeni vizuri na wahaya mtekenyo kidogo tu maji bwilili kama umeng'oa Koki waaaaaaawhhh😹😹
 
 
Mji wa Dodoma unakuwa kwa haraka sana,mamlaka zisipofanya jitihada za makusudi hali itakuwa mbaya sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…