Uingereza waziri wa mambo ya ndani na usalama wa taifa ni muhindi
Uingereza hawapeani vyeo ili kupata unafuu wa maisha.
Waingereza Wanapeana uongozi ili kuwapa Waingereza unafuu wa maisha.
Huku ni Wajanja Wanapeana nafasi za uongozi ili mambo yao binafsi yaende vizuri.
Wanajipenyeza kila mahali Kwa namna yoyote na Sasa wanatutengenezea mpaka Sheria.
Sheria nyingi ni za kumkandamiza mnyonge.
Hivi NHC inafaida Gani Kwa Mtanzania mnyonge anayepangisha nyumba Kwa bei mbaya wakati Kuna Wageni wanajinafasi kwenye shirika la Nyumba la Taifa ? matokeo yake watanzania Kwa watanzania tunanyonyana Kwa watu kama yule aliyejenga nyumba mia Tano ili awapangishie Wanyonge. ILALA ndilo Jiji lakini halina stand kubwa ya mabasi,Ina masoko yanayoingiza mabilion ya pesa lakini hayana hata Miundo mbinu ya kisiasa zaidi ya kujengwa na magunia mpaka yanawaka moto.
Hawa hawapo Kwa ajili ya Vijana wa kitanzania waliojazana mitaani wakiwa hawana ajira halafu tunawapa ajira magobachori Toka nje ya nchi Tena bila kufanya uchaguzi badala ya uchafuzi.
Ili hata Mchina agombee basi ni lazima pawe na Demokrasia iliyopevuka sana na uongozi na cheo kiwe ni dhamana na pawe na katiba inayoweka miiko ya uongozi.
Pawe na Uraia Pacha mana tunawabagua watanzania wenzetu wanaoishi Nje wakati tunawakumbatia Wageni ambao Wana kwao na wakienda kwao wanapokekewa na ndio wanaotoa taarifa za kiuchunguzi Kwa nchi yetu na kuhujumu uchumi wetu.
Siku hizi Kuna mpaka Mchele na asali Toka India .Yani Kweli tunaona ni sawa na hatuhujumiwi na Hawa mawakala waliojazana kwenye mifumo na wenye kutumia fedha kuwa karibu na watawala na mihimili iliyopo !!!!!!!