Does Africa have its own (unique) definition of democracy?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Does Africa have its own (unique) definition of democracy?

Je, Afrika ina tafsiri yake binafsi (ya kipekee) ya neno demokrasia?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, nimepokea ujumbe huu kutokwa kwa mtoto wa ndugu yangu analiyezaliwa na kuishi huko huko Ulaya (Uholanzi) na hajawaji kukanyaga huku Tanzania (Africa). Huyu dogo ana miaka 15, kama angekuwa huku Tanzania let's say labda angekuwa form II?

Just imagine wewe ndio Infantry Soldier, ungewezaje kumjibu huyu mtoto wa ndugu yako?

PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Ninaweza kusema NDIO na HAPANA kwa wakati mmoja. Wazungu wasilazimishe utaratibu wa siasa zao ndio iwe desturi yetu.

Afrika tuna siasa zete zinazofanana na sisi, maisha pamoja na mazingira yetu.

Democracy ya mzungu ndio inaua wanawake na watoto huko Iraq, Afghanistan, Libya na Syria.
 
Tafsiri ya Demokrasia ni MOJA TU mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote.

Tofauti na hapo, ni kitu kingine kabisa.
Mkuu, kwa hiyo una maanisha "Africa doesn't has its own (unique) definition of democracy" but follows the generally-accepted one? Au sio?
 
Mkuu, kwa hiyo una maanisha "Africa doesn't has its own (unique) definition of democracy" but follows the generally-accepted one? Au sio?
Ndio, kwa maana ya kwamba, uwepo wa Demokrasia barani Afrika unatokana ama utatokana na hiyo tafsiri MOJA TU iliyopo mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote ambayo kwa hiyo ama kwayo tunaweza kuihakikisha kuwa ipo.

Kuhusu uwepo wa hiyo Demokrasia barani Afrika ni jambo jingine ama mjadala mwingine.
 
Du
Tafsiri ya Demokrasia ni MOJA TU mahali kokote kule ama popote pale na wakati wote.

Tofauti na hapo, ni kitu kingine kabisa.
Dunia ya sasa imeisha- prove wrong dhana hiyo mkuu. Hivyo unavyo itasfiri wewe, yule au mimi si lazima iwe sawa. Kwani tafsili Ile haikuwa ' law' bali ilikuwa 'principal' tu.
 
Hatuwezi kuwa definition yetu ya democracy kwa kuwa hili neno lenyewe tumeletewa na hao wazungu wakaleta na definition yao

Kwa kifupi wametupangia maisha kutoka wakati walipo Anza kututawala

Wakati huo ndio walivyo haribu kabisa mfumo wote wa kuendesha maisha kwa hapa Africa toka kwenye politics mpaka education system na aspects zingine zote za maisha yetu
 
Du

Dunia ya sasa imeisha- prove wrong dhana hiyo mkuu. Hivyo unavyo itasfiri wewe, yule au mimi si lazima iwe sawa. Kwani tafsili Ile haikuwa ' law' bali ilikuwa 'principal' tu.
Huo utofauti wa kuitafsiri Demokrasia ni makosa yanayofanywa na watu kwa kujua ama kwa kutokujua.

Si sahihi kabisa kwa kitu chenye tafsiri MOJA inayoeleweka kutafsiriwa tofauti na tafsiri yake inayopaswa kuwa.

Iweje utengeneze kitu kingine tofauti na ukipe tafsiri ya 'Demokrasia'? Kwanini usikipe kitu hicho tafsiri ya kuendana na jinsi kitu hicho kilivyo?
 
Suala linalohitaji mjadala mpana unalijibu kiurahisi rahisi na unahitimisha unachokijua ndiyo jibu.
 
Suala linalohitaji mjadala mpana unalijibu kiurahisi rahisi na unahitimisha unachokijua ndiyo jibu.
Hebu nawe ndugu lijibu suala hilo 'kiugumu ugumu' kupitia huo "mjadala mpana" kisha hitimisha kile unachokijua.

Asante.
 
Hebu nawe ndugu lijibu suala hilo 'kiugumu ugumu' kupitia huo "mjadala mpana" kisha hitimisha kile unachokijua.

Asante.
Siwezi kufanya hivyo maana najua ninachochangia.

Nitakachoweza ni kutoa maoni tu. Sio kuhitimisha mjadala.

Hakuna mjadala kwenye uzi...naona wachangiaji wakibishana tu.
 
Ninaona umeamua kuandika kitabu kizima. hakika wewe ni noma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…