Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Msanii wa Singeli Dogo Paten amesema kuzuiwa kuingia Nchini China kulisababishwa na changamoto mbili ikiwemo kutokuwa na kadi ya benki ambayo angeitumia akiwa Nchini humo pamoja na kutokuelewana kwa lugha kati yake na Afisa wa Uhamiaji wa China aliyekuwa akimhoji katika Uwanja wa Ndege wa Guangzhou.
Akizungumza katika mahojiano na AyoTV, Dogo Paten amesema maandalizi ya Tamasha walilokuwa wamealikwa kufanya yalikuwa yamekamilika, huku malipo yao yakishatolewa na tiketi za tukio hilo zikiwa tayari zimeuzwa.
Hata hivyo, changamoto hiyo ya uhamiaji ilipelekea ashindwe kuingia Nchini humo ambapo amesema visa yake ilifungiwa kwa muda na anatarajia kuweza kurejea tena Nchini China baada ya kipindi cha miezi mitatu kukamilika.
Dogo Paten amesema suala hilo halikutokana na kosa la jinai au matatizo ya usalama, bali lilihusishwa zaidi na taratibu za uhamiaji na uwezo wa kuthibitisha namna angejiendesha kifedha akiwa Nchini China.