Dogodogo alivomuharibia baba mkubwa dakika za mwisho

Dogodogo alivomuharibia baba mkubwa dakika za mwisho

Z kali

Member
Joined
May 25, 2022
Posts
86
Reaction score
159
Nawasalimu nyote,

Ni baba angu mkubwa kabisa, ni mstaafu mpya kutoka serikalini ana mwaka ivi na miezi kadhaa uraiani.
Akiwa kazini alioa na kupata watoto wanne, mambo yalikuwa POA tu amani na furaha, watoto wamekuwa na washaolewa/kuoa

Mwaka Jana mzee akamaliza mda wa utumishi wake na kusitaafu kwa amani kabisa. Sasa mwaka huu mwazoni, nazan January mzee akataka kuongeza mke wa pili, na ikawa ivo, akajipatia dogodogo Kama yule wa mzee (hayati) Mrema, M/Mungu amlaze pema, ili amliwaze na kumrudisha utotoni Kama sio ujanani.

Siku zikapita mitala ikaendelea kama ilivoamrishwa. Aisee! mwez huu mwanzoni mzee alipata maradhi, kwenda hospital hana damu, kaongezewa chupa 4 na maji ya kutosha, hali mbaya, hamna nafuu, wakichek vipimo ugonjwa hauonekani, labda kalogwa, Mara itakuwa katupiwa jini, Mara ivi Mara vile.

Kwa bahati mwanae kaja majuzi Kati, yy anaishi mkoa mwingne, akashauri mzee acheki HIV/AIDS, na ikawa ivo na kwa bahati mbaya mzee kakutwa na maambukizi ya HIV.

Wakaitwa wake zake wote wawili nao ikabidi kupimwa HIV/AIDS na kwa bahati mbaya tena mke mdogo (dogodogo) anakutwa na maambukizi na bahati nzuri kwa mke mkubwa Yuko salama.

Sasa baada ya purukushani za hapa na pale, ikaonekana bi mdogo ndo kampa mzee ngoma, baada ya kubanwa bi mdogo akakiri ni kweli Yuko na maambukizi MIAKA MITANO Sasa na anatumia dozi, mzee aligoma kuamini first time aisee, ilikuwa noma Sana ila now kakubali matokeo na ameanza kutumia dozi rasmi.

Mzee alisitaafu vizuri kabisa ila mtaa hauna hurama, Ugonjwa upo wakuu, tuchukue tahadhari.

Assalam alaekum

Tujiandae na maswali 100 ya SENSA kesho
 
Sio mbaya mzee akizingatia maelekezo ya dawa na chakula bado ana miaka 15 ya kuishi kibishi... Angekua kijana ni zaidi ya miaka 30 anaishi na virusi
 
Mafao imemletea Mzee HIV bila shaka bila mafao Mzee angebakia njia kuu
 
A
Kama angekuwa anatumia dawa kwa usahihi asingeweza kumuambukiza huyo mzee.Huyo demu alikuwa hatumii dawa kwa usahihi au mzee alikuwa anazama kwenye tope
Acha hizo iman au theori zako ndugu...
 
Kama waliishi pamoja, huyo dog doho alijificha ticha vipi na loop lake la dawa?
 
Mzee alioa bila kucheki afya huyo bila shaka itakuwa alikuwa mwalimu.
 
Basi mzee baba karuhusu goli dakika ya tisini na mkeka umechanika.
 
Huyu mzee atakufa kwa stress.

Kwanza ndo ataona upande wa pili wa mke mkubwa... Demon side of his first wife.


Huyo mke mkubwa atatumia silaha ya ukimya mpaka huyo mzee awe na adabu
 
Screenshot_20220720-130912_Quora.jpg
pole kwa mzee...
 
Back
Top Bottom