Doing Business in Mozambique


Asante. Naangalia uwezekano wa kufanya biashara huko. Nikiwa tayari nitakutafuta kukuuliza maswali mengine.
 
je unapovuka mpaka kutoka tz kwenda mozambique na mizigo mpakani hawasumbui? Ni vibali gani vinahitajika ili mizigo ipite?

mkuu kuna malori ya kusafirisha mizigo mpaka mozambique, kama ungependa kujua nakushauri unde kariakoo kama cjckosea mtaa wa swahili kuna gest unaitwa vunjo jaribu ulizia utapata details zote
 
mkuu washawasha, umepotea sana

hao jamaa vyakula vyao vyenye asili ya ki portugese wanapenda sana kutumia vitunguu saumu, unaweza kujua kama vinaweza kuwa ni potential au soko linaweza kupatikana?
Nipo Kiongozi wetu,ni kweli kabisa huku bila kitunguu swaumu mchuzi haujapikika wala samaki/kuku hajakaangika,ila makaburu wa RSA kwa hapa Maputo wanaingiza sana vitunguu na wenyeji na wao wanalima pia,kitunguu kimoja kinachambuliwa au kinauzwa kizima kwa 5 au 10mt. Na exchange rate US$ 1 =27mt. Hiyo ni bei ya kitunguu jijini Maputo.
 
Aisee kumbe pesa ya Mozambique inathamani kuliko ya tanzania by Far.
Dola 1 ni sawa na Metical 26.8 Source ( XE: (USD/MZN) US Dollar to Mozambican Metical Rate )
wakati Dola 1 ni Sawa na Tsh 1,600.
inamaana Nikiweza kuexport products from Tz to Moza lazima faida iwe kubwa sana.
Naomba kujua Vitu vipi havina import Duty in Mozambique,TRA yao wakoje siyo wasumbufu?
 

duh , hii pesa yao meticash inanguvu sana

inaelekea agro products nyingi wanapata kutoka kwa makaburu RSA, sijui ni agro prducts gani zinaweza kuwa na potential market, hebu jaribu kucheki vitu kama choroko na rossela plants,
 
ok..... nafanya process za loan 10 millioni niko MTWARA, wacha nikafungue biashara huko MOZAMBIQUE..... Tena naenda mwezi wa 12 kufanya survey!!! duuu, JF ni zaidi ya maujanja!!! nina B.A. ACCOUNTING AND FINANCE, mmenipa maujanja mengine jamaaaaaaniiiiiiiii......khaaaaaaa
 

Hawana usumbufu wowote furushi kubwa la nguo ukilipia sana mt 3000 ambayo sawa nda dollar mia!
 
Mkuu je biashara kama ya sembe italipa huko? au nafaka nyingine kama mchele

Huku biashara zote zinalipa sema siwezi kukuakikishia zaid coz me nauza nguo ila kunajamaa alinitonya kuwa mafuta ya kupaka yanalipa sana unatoa tz me mwenyewe mwezi wa kwanza nataka kujaribu!
 
very useful topic, kuna mtu mwingine alishaongelea hii issue ya msumbiji, nami naona dalili ya kunusa huko,je issue ya construction industry vipi huko especially kwa contracts za umeme?
 
Mkuu je biashara kama ya sembe italipa huko? au nafaka nyingine kama mchele

biashara ya sembe inalipa sana mkuu kwa mozambique, ndo naifanya mie huku sema uwe na capital ya kutosha kununua mahind utafaid kuliko kusubir ya kuletewa. Kwa mfano mie niKo Pemba kipindi cha mavuno naenda vijiji vya ndan sana na kupata mahind kwa Bei ya Mt 1.5 mpaka 3. Na kuuza n mt 18 kwa kilo Hapa n wakat wa mavuno Ila kipindi cha napanda mpaka 25. Pia umeme uko bei chee kinoma. Tatizo linakuja kwenye upande wa packing magunia mpaka nipande dar. Karibu usiwe na was
 
Mkuu je biashara kama ya sembe italipa huko? au nafaka nyingine kama mchele
kama unaweza fanikisha kuvusha mchele wa tz utaula kwa jumla hapa Pemba nnauza Mt 55 kwa kilo inshort
Sijafika sehem nyingine Ila kwa Hapa Pemba chakula ni tab sana hata maharage n yaa tab, nyama ya ng'ombe tunapanga Folen na buchan
Mzungu anajifungia saa sita zaid ya hapo kesho
 
very useful topic, kuna mtu mwingine alishaongelea hii issue ya msumbiji, nami naona dalili ya kunusa huko,je issue ya construction industry vipi huko especially kwa contracts za umeme?

kaka nadhan italipa kwa sabab hata mafund mara zote ninao watumia kunifanyia wiring ni wa kitan tu wamekariri ukileta kitu kipya wanashindwa Ila construction inalipa kuna mbunge wa kama ckosei n mtwara alikuwa nayo Huku na contracts alikuwa nazo za kufa mtu, watu wa Huku wanataman sana kuwa na vitu vizur Ila mafund wa Huku kwa sio competent pia gharama zao ziko juu sana. Njoo usurvey kwenye hiyo industry yako Ila by 100% utakimbia pesa.
 
Mkuu tuseme mzigo wa mchele kama kilo 10000 mtu anaweza kuchukua muda gani kuuza?
 
Mkuu tuseme mzigo wa mchele kama kilo 10000 mtu anaweza kuchukua muda gani kuuza?

inategemeana mie ninachofanya kwa sabab na deal na unga pia huwa nawasambazia Wenye maduka baada ya kama wiki au na zaid naenda chukua pesa yangu na kuna kipindi kama mwez wa kwanza mpaka wa pili huwa naja kununua tayar watu washaninunua. Ila naangalia kwenda
Nampula pia kwa sabab kule population ni kubwa sana tofautt na hapa. Tatizo kuvusha toka tanzania unakuwa ni soo hawaruhusu nafaka yoyote kuvuka zaidi ya Masasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…