Dokezo Jipya: Baada ya Bunge kuvunjwa kuna mafuriko ya wana CHADEMA wanahamia NCCR Mageuzi

Chadema kimepoteza sifa zote za kuwa chama pinzani.

Chadema kumpindua Slaa na kumweka Lowassa #haikubaliki


Chadema kuwapokea mafisadi(mamluki) wa sisiem #haikubaliki

Mwenyekiti wa chadema mlafi wa madaraka,ni miaka 20 sasa #ni aibu

Ushauri
Mbowe ungepumzika sasa,ubaki kuwa mshauri wa chama.

Chama ili kiwe kisafi hakiwezi kupokea wachafu kutoka chama A kuleta chama B,tena wakapewa first priority ya kugombea(si sawa),kama wanaipenda chadema na wako teyari kuitumikia,wapeni miaka mitano ya uangalizi bila kugombea nyadhifa zozote uone kama wana uvumilivu ama wamekuja kimaslai.
 
Pia ninachojua mimi Mafuriko ya wabunge tutakayoyaona ni ya kutoka CCM kwenda vyama vingine ...... na hasa wanapojua hawana nafasi katika Chama ..... kuna mtu anahang anaitwa Membe watch out hana sifa zote za Lowasa...Lipumba ..... Mrema .....bomu la kutegeshwa .....dhidi ya upinzani ......wanamuona kama mkolofi fulani hivi ndani ya CCM lakini kwa nini kipindi hiki cha uchaguzi ndio afukuzwe ....kumbuka huyu ni usalama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watafuata mpunga, hii nchi bwana
 
Mbona watu wengi tu wenye akili na msimamo bado wanaikubali na kuiunga mkono Chadema
 
CDM hifi ng'oo mnajisumbua subiri uone mambo yatakavyokuwa mwaka huu mwishoni.
 
Ongezea na Tundu Lissu kuwapokea mabwana wake wa ACCASIA uwanja wa KIA na kukaa nao hotel kujadili namna ya kuishitaki Serikali #haikubaliki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahame tu
Chadema itaendelea kuwepo
Kila mmoja aombe corona isimmalize
mbatia aombe sana
 
Ndio siasa,kuhama Ni kawaida,hata Trump alikuwa Democrat akahamia Republican,,sioni tatizo,cdm haiwezi kukosa wagombea
 
Alisikika mlevi mmoja akipayuka kwa sauti ya juu akiwa ndotoni!!
 
Hata kama watasepa wote,CHADEMA isije thubutu fanya usajili kama wa 2015.Ule ndo umeharibu CHADEMA.Watumie wanachama waliopo CHADEMA sasa.Bora jimbo likose mgombea kuliko kuweka oil chafu toka CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…