Dola hutumia nadharia njama kututoa tusijadili mambo ya maana badala yake tujadili uzushi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Nadharia Njama (Consipirancy Theory) ni hali ya kuamini kwamba kuna taasisi au watu fulani wanahusika kufanya jambo fulani la siri kwa faida yao. Lakini pia inawezekana ikawa ni hoja fikirishi ya kutungwa dhidi ya kitu fulani lakini hoja yenyewe isiwe ya kweli.

Siku moja miaka ya themanini (1987) kulitokea habari kwamba kwenye eneo fulani kule Buguruni kuna mtu kageuka nyoka. Zama zile kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii wala teknolojia ya kusafirisha habari kama ilivyo hivi sasa, lakini habari hiyo ilisambaa kwenye mji wa Dar es salaam kwa kasi ya ajabu sana. Ghafla mji mzima ukashikwa na taharuki na kukawa na heka heka kubwa sana ya watu kuelekea Kituo cha Polisi Buguruni kwenda kumuona huyo mtu aliyegeuka kuwa nyoka.

Habari hii haikuwa mwisho wa habari kama hizo kutokea katika taifa letu. Na aghalabu habari zenyewe huja wakati kama Taifa huwa tunakuwa kwenye hali fulani inayohitaji mjadala wa Kitaifa. Kwa waliosoma kwenye shule za umma za Dar es salaam miaka ya sabini na themanini, watakumbuka vurumai za wanafunzi kutimua mbio kisa wameambiwa kuna Mumiani au majini yanakuja kwenye shule yao. Kuna wakati shule hadi zililazimika kufungwa kwa kuwa waalimu hawakuwa na amani kwenda shule kufundisha na wazazi nao ,walikuwa na hofu ya watoto wao kunyonywa damu ama na Majini au Mumiani.

Lakini hebu tujiulize, hivi ile habari ya "Rama mla watu" iliishaje? Ilikuwaje Taifa zima likasombwa kwenda Samunge kwa Babu? Nani anajiuliza dalali alikubalije kuziuza nyumba za Lugumi kwa kuambiwa tu kuwa "mia tisa itapendeza zaidi" na Dokta Shika?

Au hizi habari huwa zinazushwa ili kutupumbaza tusijali na kujadili mambo ya msingi kwa Taifa letu??
 
Kuna habari za kisiasa, kiuchumi, kijamii, utamaduni, mila na desturi ambazo zipo kila siku na huwezi kuziepuka. Ni jukumu la mtu kuchagua kipi afuatilie na kipi aache.
Afterall, kwenye haya maisha,; mambo tusiyoyajua ni mengi kuliko tunayoyajua
 
Tusiyoyajua huwa tunajua kwamba hatuyajui kwa kuletewa ujuzi wake. Ila kuzusha jambo ili watu wahamaki, hicho ni kitu kingine!!
 
Nadharia Njama (Consipirancy Theory) ni hali ya kuamini kwamba kuna taasisi au watu fulani wanahusika kufanya jambo fulani la siri kwa faida yao. Lakini pia inawezekana ikawa ni hoja fikirishi ya kutungwa dhidi ya kitu fulani lakini hoja yenyewe isiwe ya kweli.

Siku moja miaka ya themanini (1987) kulitokea habari kwamba kwenye eneo fulani kule Buguruni kuna mtu kageuka nyoka. Zama zile kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii wala teknolojia ya kusafirisha habari kama ilivyo hivi sasa, lakini habari hiyo ilisambaa kwenye mji wa Dar es salaam kwa kasi ya ajabu sana. Ghafla mji mzima ukashikwa na taharuki na kukawa na heka heka kubwa sana ya watu kuelekea Kituo cha Polisi Buguruni kwenda kumuona huyo mtu aliyegeuka kuwa nyoka.

Habari hii haikuwa mwisho wa habari kama hizo kutokea katika taifa letu. Na aghalabu habari zenyewe huja wakati kama Taifa huwa tunakuwa kwenye hali fulani inayohitaji mjadala wa Kitaifa. Kwa waliosoma kwenye shule za umma za Dar es salaam miaka ya sabini na themanini, watakumbuka vurumai za wanafunzi kutimua mbio kisa wameambiwa kuna Mumiani au majini yanakuja kwenye shule yao. Kuna wakati shule hadi zililazimika kufungwa kwa kuwa waalimu hawakuwa na amani kwenda shule kufundisha na wazazi nao ,walikuwa na hofu ya watoto wao kunyonywa damu ama na Majini au Mumiani.

Lakini hebu tujiulize, hivi ile habari ya "Rama mla watu" iliishaje? Ilikuwaje Taifa zima likasombwa kwenda Samunge kwa Babu? Nani anajiuliza dalali alikubalije kuziuza nyumba za Lugumi kwa kuambiwa tu kuwa "mia tisa itapendeza zaidi" na Dokta Shika?

Au hizi habari huwa zinazushwa ili kutupumbaza tusijali na kujadili mambo ya msingi kwa Taifa letu??
Umewaza kwa kina sana mkuu hadi kuleta mjadala kama huu, hongera sana.

Binafsi nimekuwa nikijiuliza swali hili ingawa sikuwahi kuzingatia zaidi au ku-share kwa watu Ila fikra zangu mara kadhaa zimekuwa zikidhani hivi ingali sina uhakika zaidi wa kile niwazacho kama ndivyo kilivyo katika uhalisia au ni fikra kama fikra tu.

Tusubiri mawazo ya wengine
 
Nakubaliana nawe mleta mada, habari bandia, na tungo zisizo na uhalisia , dhana na ngano zipo nyingi sana, na zipo kwa malengo maalum.
Uko sahihi.
Japo uamuzi ni wa mtu binafsi kusikiliza na kuzingatia au kusikia na kupotezea.

Watu wengi tunaamini kwamba sisi ni binadamu, tumeumbwa na tunaishi katika sayari inayoitwa dunia.
Tuna uhakika gani kama sio nadharia?

Ikiwa hatufikiri kwa kina hatuwezi kuelewa. Tatizo sio waleta hizo tungo,. Tatizo ni kwa wanaoamini hizo tungo kama walivyoaminishwa kuwa JPM alikuwa dhalimu na dikteta...
 
Tumeshajulikana wabongo tu watu wa namna gani. Issue sensitive inaweza potea chap kwa kupenyeza taarifa ya kizushi au kimbeya. Watu wapo kitengo cha fitna cha kuhakikisha upumbavu unatamba na kuuziba werevu usisikike
 
Sio bongo tu, hata ulaya wanafanya.
Sema technique zao ni za viwango vya juu kiasi kwamba si rahisi kung'amua kama ni uzushi tu!
Mfn issue ya magonjwa ya mlipuko, ugaidi nk, vinaweza kutumika kuzima jambo fulani au kutekeleza kusudi fulani
 
Hakuna kazi iliyo rahisi kama kulitawala fuvu la Mtanzania. wewe lijaze Simba Yanga halafu anzisha kauzushi kadogo mengine liachie fuvu hilo litajaza lenyewe.

Wewe njoo kwenye vijiwe vya kahawa vya huku Tandika usikie yanayojadiliwa mambo ya kipuuzi na propaganda za CUF.

Nyerere aliua elimu na sasa matokeo tunayaona mitaani.
 
Lakini hebu tujiulize, hivi ile habari ya "Rama mla watu" iliishaje? Ilikuwaje Taifa zima likasombwa kwenda Samunge kwa Babu? Nani anajiuliza dalali alikubalije kuziuza nyumba za Lugumi kwa kuambiwa tu kuwa "mia tisa itapendeza zaidi" na Dokta Shika?
Hivi sasa kuna threads zinatrend sana ...kula tunda kimashara nk ukijiuliza zinalenga nini hupati majibu

Hivi sasa kuna threads zinatrend sana ...kula tunda kimashara nk ukijiuliza zinalenga nini hupati majubu
Kwa kweli tuna mambo mengi yanayopewa kipaumbele kwenye jamii yetu hadi unashangaa yanatoka wapi. Maana kwa Babu ilisemwa hadi itajengwa barabara ya lami ili watu wafike kule kirahisi.
 
Kuna wkt waliwahi kuvumisha kuwa huko TEMEKE kuna WAGONI wamenasiana eti kwa sbb mmoja wao ALIZINDIKWA!

Kisha ikaja Habari ya Kutoingia maeneo ya Mjini km Kkoo kwa alievaa Kandambili "Malapa", Habari ilienea na kuenea!

Kadhalika kuna Sheikh Mmoja huko nyuma aliidraft vzr sana Habari ya POPOBAWA na Movie ikatrend haswa huku wanaomjua wakisema yule Bw. TIS

Binafsi nazikumbuka zile story za Makontena ya Mapanga na Visu alokamata MAHITA akidai vimeingizwa na CAF

Nyuma tu hapo mambo ya Koneksheni yalipoanza... uvumi ulikuja kuwa kuna watu wameona CONNECTION ya Mama Mchungaji. Nchi nzina ikaanza kuhaha...

Ila Heshima kwake alieitengeneza Movie ya BABU WA LORIONDO, Movie Ile watu wametajirika, watu wamepoteza wapendwa wao, tulivo wanafiki tupo kimya kanakwamba Babu wa Loriondo hayupo au hana Kikombe!
 
Back
Top Bottom