Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?

Kuyaongea hayo naona tofauti na kumsifia Baba yako kwa sababu kakununulia Viatu vya shule.
Ni miradi mingine ameikuta.

Ifike mahala watanzania tudemand outstanding decisions, na wala sio kuwamoved na propaganda za viongozi.

Tungekuwa watu wakufuatilia vitu, na sio wakuwa moved na incidences tutafika mbali.
Sasa hivi media inatumika vizuri kuendelea kumanipulate mawazo ya watanzania.
 
TRA,TAKUKURU na wizara ya fedha chini ya Dk. Mpango ndio wameifikisha hii nchi(ICU) hapa ilipo katika awamu hii ya tano.
Wamekuwa waongo,wala rushwa na wanafiki huku wakimdanganya mh.JPM kwa mambo ya uzushi kuanzia makinikia hadi CELTEL.
 


Unajua kukosoa na kucheka ni kitu rahisi kuliko vyote Duniani, kila mtu analia na kulalamika halafu mtu akichukuwa hatua mnakuja na misemo sijui tulikwambia, ona sasa umefika wapi, kujifanya unajua, sijui kiko wapi, yote haya ni ya nini? Huu usenge hauwezi kututoa hapa, kama mtu akijaribu hata kama akishindwa anapaswa kuungwa mkono ndivyo watu na jamii zinavyoendelea!
 
Pascal Mayalla Hiyo ni taarifa kutokana na uzalishaji wa Bulyahulu au ni taarifa ya migodi yote ikiwa ni pamoja na Buzwagi na North Mara?

Ulinganifu wa mapato ya mwaka uliopita (2016) na mwaka wa 2017 hauna maana kwa vile mwaka uliotangulia migodi yote ilikuwa inazalisha kwa ful capacity! Gharama za uzalishaji za mwaka uliofuata (2017) zinapaswa kuwa chini kwa vile hapakuwa na gharama za uzalishaji kwa kiwango kikubwa katika migodi ya Buzwagi na Bulyahulu kwa vile wafanyakazi wengi walikuwa wameachishwa kazi!

Juu ya yote hayo, tusisahau kwamba ni Barrick Coperate ndio walikuwa wanafanya mazungumzo na serikali ya Tanzania na sio Acacia (ingawa siwezi kutofautisha sana hawa watu wawili) ikiwa na maana kwamba makubaliano hayo hayakuihusu Acacia (kumbukeni kujiuzulu au kustaafishwa kwa Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Acacia kutokana na kauli zao wakati mjadala ulipokuwa ukiendelea Dar es Salaam kati ya Barrick na serikali)

Jambo la msingi ambalo labda tunapaswa kuwauliza wawakilishi wetu katika majadiliano yale ni juu ya muda uliokubaliwa (time frame) katika kutekeleza yaliyoafikiwa! Suala la ama Acacia wana uwezo au la, si la kutusumbulia akili sana!

Wakishindwa ama kwa kupata hasara au kwa makusudi, tutanadi mali zao kwa muwekezaji atakayekuwa na nia njema ya kufanya biashara ya uchimbaji na sisi!
Tafakari!
 
Uko sawa, Ila pia inategemea na feed grade, /recovery/tonnage, kama feed grade ni nzuri, unaweza operate kwa hata dollar 500 kwa wakia moja.
 
Kukosoa ni jambo rahisi kweli, na kucheka ni jambo rahisi zaidi.

Utendaji on the other hand ni mgumu sana pale unapokuwa tied to many(indepted to many).
Na utendaji huwa mgumu zaidi pale mtendaji anapoweka mbele popularity dhidi ya shabaha alizoziweka.
Na sasa hivi ni kama hakuna shabaha ila kuna maamuzi ya kuridhisha watu kwa muda huu.

Utendaji makini hauhitaji media power au propaganda ili kudhihirisha kazi inafanyika.
Sasa sisi tumefanya vice versa
 
Pascal Mayalla Safi sana hapa umeongea bila kumung'unya umetoa makavu live ukiendelea hivi ntakukubali 95%

SIZONJE akipitia hii lazma atakunja uso [emoji37] [emoji31] [emoji37] [emoji37]
Umeongea kikubwa sio ile kupindapinda
 
Pascal Mayalla Ati Shemeji wasema kishika Uchumba, kipi?Mbona Mwali aliolewa bila hata kutolewa posa halafu unatafuta kishika Uchumba shauri yako.

Mlidhani alichoongea Lissu uongo eh, sababu watanzania hatupendi ukweli,sasa Lissu alisema miaka 20 iliyokwisha Mwali/binti yetu kaolewa bila hata ya POSA tukamtukana tukamuweka kizuizini,juzi kasema jamani ili tumpate binti yetu na wajukuu zetu basi twende namna hii mkamlaza Nairobi.

Haya tusubiri kishika uchumba wakati Mwali keshachukuliwa bila hata ya 'POSA'
 
Kweli rafiki! Tunapojenga nyumba mmoja, ni afadhali tugombee fito kuliko kuficha fito!
 


Unasahau kama Magufuli ni Raisi wa nchi hivyo kila anachokifanya ani lazima kitapata media coverage, hilo halikwepeki, sasa nashindwa kuelewa unaposema hiyo ulioiita ,,hauhitaji media power "unamaanisha nini?
 
Si mlijifanya mnaakili kuliko mtaalam LISSU
 
Kwani alichaguliwa ili ajaribu? ni hatari sana kufanya majaribio ukiwa ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…