Ukitumia gold mining data, za Acacia na duniani kwa ujumla, utapata conclusion kwamba, sio tu Acacia bali hata hao Barrick Gold Mine hawana uwezo wa kulipa zile pesa... I repeat, HAWANA UBAVU. Data zetu zipo so irrelevant!
Look, according to
USA Gold, total gold produced duniani in 2016 ni tani 3100.
Tani 3100 ni sawa na 3,100,000 kg
Kwa mujibu wa mtandao wa
GoldPrice, bei ya dhahabu at 14:15 EAT ilikuwa 1,333.01 per ounce. Anyway, sijui pametokea nini manake pamekuwa na sharp decline in price from around US$ 1342 to 1,333.01 lakini wametoa
best price as $1356 per ounce (for gold bar).
1 oz ni takribani 28.5 grams.
3,100,000 kg = 3,100,000,000 grams = 109 M ounce (maximum)
Thamani yake ni 109,000,000 x $1356 = $ 148 Billion (maximum)
Hii maana yake ni kwamba, dhahabu iliyozalishwa duniani kote mwaka 2016 ina thamani ya takribani $150 Billion wakati pesa tunayodai sisi ni $190 Billion!
Yaani, Acacia/Barrick kulipa ile pesa ina maana waachiwe dhahabu YOOOOOOTE duniani kwa mwaka mzima. Aidha, wazalishe dhahabu hiyo at ZERO cost ndipo wanaweza kulipa deni (assuming uzalishaji na bei vinabaki constant)!!!
Look again, hoja ni kwamba ni tunaabiwa kupita kiasi.
Ina maana na Australia wanaibiwa kupita kiasi?
Mwaka 2016 Australia walizalisha 270 tani za dhahabu! Remember, Australia ni among top gold producers duniani!!!!
Tani 270 = 270,000 kg = 270,000,000 grams = 9.5M ounce (Maximum)
Thamani yake kama ingeuzwa leo, ingekuwa 9,500,000 x $1356 = $13 Billion (maximum).
Hii maana yake ni kwamba, endapo Australia wataamua kuwalipia deni Acacia, basi watalazimika kutumia dhahabu yao yooooooooote kwa takribani miaka 15 (190 billion/13 Billion) ndipo wanaweza kumaliza deni lote la Acacia na hapo tuki-assume, Australia wanazalisha dhahabu hiyo at ZERO cost na kila mwaka wanazalisha tani 270.
Kwahiyo kwa data zisizo-make sense kama hizo TUSAHAU eti kwamba Acacia au hata Barrick watakuja kulipa hata 25% ya kile wanachodaiwa! Na hili nilisema tangu awali.
Na ukweli ni kwamba, sioni uwezekano wa kulipa hata 10% ya kile wanachodaiwa!
BONUS: According to
Bloomberg, New York Stock Exchange walifunga soko tarehe 12.01.2018 wakati Barrick Gold wakiwa kwenye position ifuatayo:
Unaona hapo chini, Market Cap ni 17.64 Billion. Na tunaposema Barrick ina maana na hesabu za Acacia zipo ndani yake bila kusahau hesabu za kampuni zao zingine zote.
So, with Market Cap ya 17.64, ina maana endapo shareholders WOOOOOOOTE wa Barrick Gold wangeamua kutoa shares zao zoooooooooote free of charge kwa Barrick kisha Barrick wakauza shares zooooooote na kuamua kutumia mapato ya uuzaji wa hizo share, bado wangeweza kulipa ONLY $17.64 Billion wakati tunawadai $190 Billion na huku pia tunaiacha Barrick Gold mikono mitupu!!!
Hii maana yake ni kwamba, deni husika HALILIPIKI kwa sababu takwimu zilizotolewa ni za UONGO... simple and clear!!