Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?


Maana yako ni kuwa, atiwe moyo (encouraged) ili aendelee "kupuyanga" kuufanya "ujinga" kwa sababu ya "mihemuko " yake tu, au siyo?

Mimi sipo tayari kwa hilo. Bali namtia moyo kujihakikishia kupata elimu zaidi juu ya namna bora yenye akili kushughulikia ishu ngumu na nyeti kama hiyo!!
 
hili halijanishangaza kabisa..
labda wanajipanga waje wamchukue mwali jumla jumla😀
 
Nakubaliana na wewe kwenye kujenga mustakabali mmoja wa kitaifa,kila upande ujishushe,wawe kitu kimoja washauriane,hapo tutafika. Nionavyo mimi haya mambo ya kutunishiana misuli bila kukaa na kutafuta mustakabali wa pamoja hayana tija kwa kila upande kwa Taifa hili. Nadhan tunakosa baraka za Mungu kwa mtengano wetu usio wa lazima.
 
Tunapigwa sana ni wimbo mpya wenye chorus ya zamani.Najiuliza tuna miaka miwili sasa tangu tuanze kuimba hii nyimbo je hatua zilizochukuliwa zina tija kiasi gani?
 
Paskal mtani wako wa Chato alizuia wasitafsiri ile Lugha ya malikia ili wengi wasijue yule prof anaongea nini.Changa la macho .hapo ndipo mtamkumbuka Sir Lissu na kungundua mzalendo wa kwel ni yupi
 
Kwa hiyo Kwa taarifa hii ya Pasco ndio unaamini hatutalipwa?
Kweli naamini maneno ya Trump
mkuu,mimi naamini tutalipwa siku moja,nauliza tu,hivi kwa uwezo wako wa kujua mambo nyeti kuna kipengele cha kuwapo kwa riba katika hayo malipo incase wakiwa wanachelewa kulipa??maana wao mikopo yao mingi kama si yote wanaweka riba sisi tulikumbuka kuweka kipengele cha riba?hebu nusanusa mkuu ulete mrejesho
 
....The late Nyerere alishauri yasichimbwe mpaka pale tutakapokuwa na capacity ya kutosha but tukamuona lofa...
 
Nakumbuka wakati nipo mwanza siku moja kabla ya kamati kumkabidhi Pogba taarifa ya kupika kuna gari lililotoka ofisi ya RC lilikuwa likitangaza na kuhimiza wananchi waende kwenye mabaa kuangalia tukio hilo ( ikumbukwe kuna marufuku ya kwenda bar ndani ya saa za kazi lakini siku hiyo ruksa hata kupiga lager)!. Tatizo la Magu anapenda kiki (ujiko) hata kwa jambo la kipuuzi! mpaka leo hakuna hata sumni nyekundu tuliyoipata baada ya kupoteza muda
 
Pasco subiri Musiba akusome kisha akufungulie kesi ndani ya nchi na kimataifa... kumbuka kesi ya Takwimu haijampata mtu.. Zitto anaogopwa sababu tetezi zake hufichua zaidi badala ya kumnyamazisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…