Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?

Jambo ambalo sijawahi kulielewa maisha yangu yote kuhusu jamii yetu ni hili, ni kwa nini huwa mnafurahia sisi kushindwa? I mean, ukiangalia jamii yetu ni kama watu wamekaa wanasubiri ushindwe wakucheke na kukukebehi, kwangu mimi sisi Watanzania ni watu childish sana, so immature, maisha hayako hivyo, watu wengi waliofanikiwa Duniani ni kwa kujaribu, kuchukuwa risks ndiyo unaweza kwenda mbele!

Bill Gates aliacha Chuo Harvard na kuanzisha Microsoft kama Wazungu wangekuwa childish na immature kama sisi kukaa kusubiri ushindwe ili wakucheke asingepata support, lkn wazazi wake na nchi nzima iko nyuma yake na kama microsoft ingeshindwa angerudi Chuoni na hakuna ambaye angemcheka au kumkebehi!

Sasa Raisi Magufuli amejaribu kama ameshindwa hatupaswi kumcheka wala kumkebehi bali tunapaswa kujipanga na kuanza upya, bila kubadilisha hii tabia hakuna tutakapoenda, kwa kifupi mnawarithisha hata Watoto wenu negativity na watashindwa pia maishani na ku-compete na Dunia kwani mnawajaza woga na misemo ya ******* kama sijui tulikwambia acheni huo ujinga vinginevyo tutaendelea kubakia masikini maisha yote na kuitwa ,,shithole" !
Unachosema ni sahihi, but not applicable in the political example you provided.

Kwenye politics ukiwa rais, unafanya maamuzi kwa niaba ya wananchi wote.

Hiyo unasema “kujaribu jaribu” kwenye nafasi ya urais unatakiwa ujipange.
 
Mkuu shida in ccm ndo imeleta umimi,yaani jambo likiwa zuri nila ccm yaani ccm wanabeba credit badala ya credit kupewa watanzania,likiwa baya ndo tunatwishwa mzigo watu wote, kwa mfano hili la acicia watu walijifanya wao ndo wazalendo na wafia nchi hii,MTU yeyote aliyekuwa ama mawazo tofauti au njia toufati na yao ya kulisolve alionekana ni adui na msaliti,Mfano Lissu anaitwa kibaraka cha wanzungu kwa kosa gani? Mimi na elimu Yangu ndogo niliona na kusikia Lissu akitutahadhalisha some possible outcomes juu ya hatua tulizochukua na tunazotaka kuendelea kuchukua dhidi ya Acacia, but nyie wasomi mnaelewa sana hakujari na mkambatiza majina,sas

Mbona kama Mh alisuggest njia sahihi ya kupitia na mh Nape akakazia kwa kusema kuliko na makelele mengi usipuuzi tu maana unaweza ukaokota hata Moja lenye maana but we didn't care


Ulitaka Raisi wa nchi achukuwe kila aina ya ushauri ktk kwa kila mtu? Tume alizounda zilijumuisha watu wasiokuwa na Chama na Wataalaamu wa Sayansi, Uchumi na Sheria Maprofesa ktk UDSM, na hatua alizochukuwa zimetokana na ushauri waliompa, sasa ulitakaje tena? Na hata Bunge na kamati za Bunge pia zilichangia na Spika wa Bunge alifikisha ripoti Ikulu, sasa ulitakaje tena? Ulitaka asikilize ushauri wa nani mwingine?
 
Ok kijana unaonekana unajua kudadavua mambo ila unasumbuliwa na ukurupukaji ambao unatilia shaka elimu yako uliyokariri.
Serikali haijawahi kujadiliana wala kukubaliana kulipana na kampuni ya Acacia Bali ilijadiliana na kampuni ya Barrick kuhusu hayo. Unapotuletea financial report ya Acacia unatuchanganya na upupu wako. Na kama umefuatilia financial report ya Barrick wakakwambia subiri hadi Feb,14 kwa nn husisubiri ??? Kila mmoja wetu hapa anasubiria kwa hamu na ukisha ji commit kulipa hauna maana kuwa ni wakati huohuo on the spot. Njoo na taarifa ulizonazo za uhakika siyo kutuchosha na report za acaccia ambao tuliwakana kwa kutosajiliwa nchini. Next time husituletee threads za kukurupuka Fanya kazi ununue Noah yako nyambafu wewe
Siyo nia yangu kuiponda ACACIA au kuitetea Serikali lakini moja ya makampuni ya kitapeli Duniani ni pamoja na Barrick na hiyo kampuni tanzu yake ACACIA. Tangu Barrick waanze kazi zao za uzalishaji Tanzania mwaka 2002 kwa madai yao hawajawahi kupata faida jambo ambalo si kweli. Katika andiko lako umesema wakia moja ya dhahabu inauzwa dola 779, hakuna kitu kama hicho Paskali na kwa hesabu za kimetalajia kama bei ya dhahabu inashuka chini ya dola 900 kwa wakia moja basi kampuni inaweza ama kusimamisha uzalishaji au kuangalia namna bora ya kuongeza kipato. Kwa taarifa yako bei ya dhahabu kwa wakia moja muda huu ninavyoandika ni dola za kimarekani 1333 japo inaweza kubadilika badilika muda wowote lakini siyo variation kubwa kiasi hicho na si kweli kwamba kwa sasa dhahabu inauzwa dola 779 kwa wakia moja
Majibu yenu yana mashiko.
Angalau yanaonesha mantiki fulani kuliko maoni ya wachangiaji wengi wameegemea ktk hisia na siasa.
 
..@Pascal Mayalla,

..Prof.Kabudi aliwahi kusema kuwa kuna mambo mazuri yametokea na wananchi tutatangaziwa karibuni.

..Je unafikiri habari nzuri anazozungumzia Prof.Kabudi zitakuwa zinahusu nini kama siyo kulipwa?
 
Pascal Mayalla
Wewe Pasco Umendika Mambo mazito na inatakiwa watu wenye akili timamu wadadavue.. Sasa kuna jambo najiuliza.. Kwa nini wewe hukamatwi na kuitwa Mchochezi?? Maana unathubutu kuhoji logical issues ila uko mtaani unafurahia uhuru wako...

Kuna jambo lingine linaloonesha jisi tulivyo na viongozi vichwa cucu pale iliposemekana AIRTELO ni ya sirikali asilimia 100.. baada ya kikosi kutumwa tunashangaa anakuja na slang ya asilimia 40 na akataka masungumuso... na kutoa comments za kisomi chake amekutaa na mambo ya aibu na aliyehusika wako naye.. sasa napata shida na sikumbuki kama Pasco umeshaongelea hili maana linanikereketa sana..

Niko Katembe huku Karagwe tunavuna mahagwe..
 
[HASHTAG]#Mayala[/HASHTAG] kuna unachotafuta kumbe, ngoja tusubiri, unatoaje hitimisho kuwa hatujalipwa dola 300
 
Kwani serikali ikilipwa ina haja kuja kuutangazia ulimwengu kua tumelipwa,je kama serikali imelipwa ikaamua kukaa kimya?
Acha tubaki na makinikia yetu,sijawahi sikia dhahabu imeoza hata siku moja
Serikali hii ya awamu ya tano haina uwezo huo Wa kukaa kimya
 
Pasco acha unazi,lete ushahidi kuonesha kuwa hatujalipwa,kuegemea kwenye taarifa zako si jibu sahihi.Kampuni inaweza kuwa haina uwezo wa kulipa deni la kodi lakini ikakopa benki kulipia kodi
 
Nilisha pata elimu kutoka kwa Zitto na nikamuelewa,japo wengi walimuona kama snitch ila lake ndio limebeba ukweli wote
 
Hii siyo hoja ya JF. Inaelekea wewe umetokea kwa Mfuga Mbwa. JF siyo pahala pako!

Hahaha nafuga kwelikweli, pole ndugu najua haupend ila wote tulimsikia, mi nikajua tutalipwa kesho yake.

Kwanza hata wakilipa au wasilipe mimi kodi yangu ntakatwa deile, mshahara wangu utaendelea kukatwa. i dont give a damn, to hell with it. Mtajijua wenyewe mimi napambana mwenyewe huyo jamaa atakaa hapo naye ataachia tu, watakuja wengine and so forth,

Baaada ya povu lote hili naomba nikutakie usiku mwema kesho nina majukumu yatakayo fanya nikatwe kodi yangu ili upatiwe huduma za kijamii za kimagumashi
 
Pascal Mayalla Katika hii ishu ya kishika uchumba, hivi mwali ndio sisi Tanzania? mume ndiyo ACACIA? na baba mkwe ndio Barrick? inaonekana hiki kishika uchumba kinalipwa na mchumba kwa kutumia fedha ya urithi ya mwali.

Yaani mwali anamhonga mchumba wake ili awasilishe kishika uchumba. baadaye mwali atamhonga mchumba mahari, ili aje atoe mbele ya kadamnasi. lakini zote hizo ni mali za urithi za mwali. wizi mtupu. udanganyifu mtupu. tatizo siyo la huyo mchumba. tatizo liko kwa mwali na familia yake.
 
Rais hapaswi kulaumiwa kwenye hili na anahitaji kutiwa moyo na watanzania wote bila kuingiza itakadi za vyama. Kwa hakika amepambana lakini kuna sehemu tunakwama, hasa kwenye utaalamu wa mambo haya ya madini na mikataba mibovu ambayo inasimamiwa kimataifa na ilishaingiwa huko nyuma.

Naamini Kinu cha uchenjuaji makinikia kitakua suluhisho la huu wizi wa mchana, rais aendelee kubana hayo mkontena haiwekani muuza korosho ajiendeshe kwa kuuza maganda ya korosho badala ya korosho yenyewe. Tumeibiwa sana.

Lissu aliposema tatizo liko kwenye mikataba kwanini yeye alionyesha kwamba Lissu ni msaliti? wakati Lissu alipokuwa anapigania mambo ya madini yeye alikuwa kimya analinda cheo chake. Saa hii Lissu yuko hosptali kwa kuonekana msaliti, kisha nyie wapambe ndio mnaamka kusema mikataba ndio tatizo? Sawa tuseme kweli mikataba ilishaingiwa huko nyuma, mbona hakuipeleka bungeni kujadiliwa ili kionekane kipi kipo humo ndani? Kwanini bado imebaki kuwa siri kama ilivyokuwa hapa kabla yake?
 
Back
Top Bottom