Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Kila siku tunalia kuhusu kuadikika Kwa Dola licha ya juhudi za kukuza Uchumi lakini hakuna ambae anajadili jambo Hilo Kwa kuangalia sababu za msingi.

Mojawapo ya vitu vinavyosababisha kuadikika Kwa Dola Nchini no hizo hapa 👇

1. Kuwapa kazi za Ujenzi wakandarasi wa kigeni badala ya wazawa Kwa visingizio vya hawana uwezo na uzoefu(wageni hulipwa Kwa Dola)

2. Kuagiza bidhaa nyingi ambazo tunaweza Kuzalisha wenyewe ndani ya mwaka eg maziwa,ngano,Mafuta ya kula, sabuni, vyakula vya mifugo, mbegu nk

3. Kukwamisha uwekezaji kutoka Nje kutokana na mitizamo ya siasa za ujamaa(kusema Nchi imeuzwa Kwa Waarabu,kuwa na sera ambazo hazitabiriki,Urasimu wa Kiserikali na Rushwa) eg miradi ya Lindi LNG na Liganga imekwama kutokana na siasa uchwara.

---
WAGENI WAVUNA FEDHA ZA MIRADI KULIKO WAZAWA

SERIKALI imesema asilimia kubwa ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inawanufaisha wageni kutoka nje ya nchi kuliko wazawa.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema bungeni Dodoma kuwa sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni uwezo mdogo wa makandarasi wa ndani wa kifedha, mitambo na wataalamu hivyo inakuwa vigumu kwao kushindana kwenye zabuni za kazi na makandarasi kutoka nje hasa kampuni za Kichina.

Bashungwa amesema hayo akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni Dodoma jana. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Usajili wa Makandarasi, kati ya miradi 36,839, wazawa walitekeleza miradi 35,351 sawa na asilimia 95.9 ya miradi hiyo.

Hata hivyo, Bashungwa amesema miradi iliyotekelezwa na wazawa ni midogomidogo yenye thamani ya Sh trilioni 23.749, sawa na asilimia 38.5 ya thamani ya miradi yote iliyosajiliwa na kutekelezwa katika kipindi hicho ambayo ni Sh trilioni 61.638.

“Hivyo, makandarasi wa nje ambao ni takribani asilimia 4.1 walitekeleza miradi michache yenye thamani kubwa (asilimia 61.5 ya thamani ya miradi yote),” amesema Bashungwa.

Kwa mujibu wake, kuna kampuni 14,800 za ndani za makandarasi, za ushauri wa wahandisi ni 252 na kampuni za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ni 461.

Chanzo: Habari Leo

My Take
Naunga mkono wazo la Bashungwa kuanza kuwaamini Wakandarasi Wazawa.Sheria hii isiishie Wizara ya Ujenzi pekee Bali Taasisi zote.Tanzania sio Mali ya Wachina pekee.

Safi sana,utekelezwaji umeanza.

View: https://twitter.com/mamayukokazini/status/1809105269336473793?t=V-Zo2_7Ye2EB2ZQVpd19PA&s=19
 
Sababu kubwa ni kwamba there's 'No Balance of Trade.'
Bidhaa nyingi sana kama siyo bidhaa karibia zote tunaagiza kutoka nje ya nchi hii, wakati huo huo sisi hatuna bidhaa yoyote ile ya maana ambayo tunauza nje ya nchi hii.
Elewa mada yangu, balance of trade utaipata Kwa kuagiza bidhaa amabzo uanaeza uzalishaji mwenyewe? Hujaona orodha ya bidhaa nilizotaja hapo Juu?

Tanzania Hatuwezi uzalishaji Mafuta ya kula au maziwa fresh?
 
Apa kwenye bidhaa naona tz bidhaa zipo za kutosha lakini ni bei ghali mno,mfano tunduma nilikuta sukari ya zambia kwa mlaji wa mwisho gharama ni ndogo ukifananisha na tunazo zalisha ndani!.
Sababu kubwa ni kwamba there's 'No Balance of Trade.'
Bidhaa nyingi sana kama siyo bidhaa karibia zote tunaagiza kutoka nje ya nchi hii, wakati huo huo sisi hatuna bidhaa yoyote ile ya maana ambayo tunauza nje ya nchi hii.
 
Njia 8 amejenga Mchina? Kwanza hamuwalipi mnawakopa unadhani watakua vipi? Zipo kampuni kibao za ndani Zenye uwezo ila hazipewi kazi.
kama ulikua hujui nikwambie tu kuwa hao wakandarasi wa bongo ni tia maji sana, wengi wao ni wezi na hawako punctual kwenye kazi zao, uvivu [kazi ya mwezi itakamilika ndani ya mwaka kwa visingizio vingi sana] - talking from experience.
 
kama ulikua hujui nikwambie tu kuwa hao wakandarasi wa bongo ni tia maji sana, wengi wao ni wezi na hawako punctual kwenye kazi zao, uvivu [kazi ya mwezi itakamilika ndani ya mwaka kwa visingizio vingi sana] - talking from experience.
Wakandarasi wa ndani ya nchi wana ubabaishaji mwingi Sana, they're not serious.
 
Back
Top Bottom