Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Wakandarasi wa ndani ya nchi wana ubabaishaji mwingi Sana, they're not serious.
Sababu HAWANA PESA km Wakandarasi wa NJE Wakandarasi wa Ndani wanategemea wapewe Pesa NDIO wafanye kazi km Pesa hakuna Kazi inadoda Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
 
Nasikia karibuni tunaanza export mitumba ya nguo na viatu kutoka Tanzania kwenda sehemu zote za dunia...😃😃
Tuna export vitu vingi tuu ila ni vichache na vyenye thamanindogo sana kulinganisha na tunavyo import.

Tuanze kwanza na substitutes ya vitu tunavyoweza Kuzalisha ,inakuaje Tina import maziwa na Mafuta ya kula?
 
Kama unaruhusu wachina waje kuwa machinga kariakoo

Kama umeruhusu wachina wajenge jengo la maduka Ubungo badala ya kiwanda unategemea maajabu yapi?
Wewe ulitakaje? Ulitaka Nini kiruhusiwe na Nini kisiruhusiwe? Kwani wabongo hawapo China?
 
Sababu HAWANA PESA km Wakandarasi wa NJE Wakandarasi wa Ndani wanategemea wapewe Pesa NDIO wafanye kazi km Pesa hakuna Kazi inadoda Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
Kama Wana pesa mbona miradi Yao imesimama? Kwa nini hawajengi Ili Waendelee kudai si Wana pesa? Labda pesa ya kuhonga.

Mnaotetea huu ujinga nadhani mtakuwa ni punguani mahala
 
Kila siku tunalia kuhusu kuadikika Kwa Dola licha ya juhudi za kukuza Uchumi lakini hakuna ambae anajadili jambo Hilo Kwa kuangalia sababu za msingi.

Mojawapo ya vitu vinavyosababisha kuadikika Kwa Dola Nchini no hizo hapa 👇

1. Kuwapa kazi za Ujenzi wakandarasi wa kigeni badala ya wazawa Kwa visingizio vya hawana uwezo na uzoefu(wageni hulipwa Kwa Dola)

2. Kuagiza bidhaa nyingi ambazo tunaweza Kuzalisha wenyewe ndani ya mwaka eg maziwa,ngano,Mafuta ya kula,sabuni,vyakula vya mifugo,mbegu nk

3. Kukwamisha uwekezaji kutoka Nje kutokana na mitizamo ya siasa za ujamaa(kusema Nchi imeuzwa Kwa Waarabu,kuwa na sera ambazo hazitabiriki,Urasimu wa Kiserikali na Rushwa) eg miradi ya Lindi LNG na Liganga imekwama kutokana na siasa uchwara.

---
WAGENI WAVUNA FEDHA ZA MIRADI KULIKO WAZAWA

SERIKALI imesema asilimia kubwa ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inawanufaisha wageni kutoka nje ya nchi kuliko wazawa.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema bungeni Dodoma kuwa sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni uwezo mdogo wa makandarasi wa ndani wa kifedha, mitambo na wataalamu hivyo inakuwa vigumu kwao kushindana kwenye zabuni za kazi na makandarasi kutoka nje hasa kampuni za Kichina.

Bashungwa amesema hayo akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni Dodoma jana. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Usajili wa Makandarasi, kati ya miradi 36,839, wazawa walitekeleza miradi 35,351 sawa na asilimia 95.9 ya miradi hiyo.

Hata hivyo, Bashungwa amesema miradi iliyotekelezwa na wazawa ni midogomidogo yenye thamani ya Sh trilioni 23.749, sawa na asilimia 38.5 ya thamani ya miradi yote iliyosajiliwa na kutekelezwa katika kipindi hicho ambayo ni Sh trilioni 61.638.

“Hivyo, makandarasi wa nje ambao ni takribani asilimia 4.1 walitekeleza miradi michache yenye thamani kubwa (asilimia 61.5 ya thamani ya miradi yote),” amesema Bashungwa.

Kwa mujibu wake, kuna kampuni 14,800 za ndani za makandarasi, za ushauri wa wahandisi ni 252 na kampuni za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ni 461.

Chanzo: Habari Leo

My Take
Naunga mkono wazo la Bashungwa kuanza kuwaamini Wakandarasi Wazawa.Sheria hii isiishie Wizara ya Ujenzi pekee Bali Taasisi zote.Tanzania sio Mali ya Wachina pekee.

Black market ina dola...zinauzwa around 2,800. Nani yuko nyuma yake? Kuuza dola kwa black marekt ni uhujumu uchumi.

nachoweza kuona na kujiridhisha ni kuwa ukiona moshi unafuka, jua kuna moto. Hii si dalili njema hata kidogo. Kuna sehemu mambo yanafeli kwa kasi
 
Siwanajenga kwa pesa walizo kuja nazo(Doral) natunanunua kwa Tzshilings

Hivi akuna watz waliowekeza nchi za njwe?.
Kama unaruhusu wachina waje kuwa machinga kariakoo

Kama umeruhusu wachina wajenge jengo la maduka Ubungo badala ya kiwanda unategemea maajabu yapi?
 
Unafikiri utapataje dollar kama hauuzi bidhaa zako nje? Utakuwa na dollar za kutosha kwenye Forex reserve ya taifa mkiexport

Ni kweli tourism, madini na crop export vinatuingizia pesa za kigeni yaani dollar. Ila ukweli ni kwamba kuna low seasonal inflows kutoka kwenye hizo sekta 3 mwisho wa siku tunakuwa na uhaba wa dollar.

Kwa kifupi tunapata dollar kidogo sana kupitia utalii, madini na export crops na huku tuna uhitaji mkubwa wa dollar ili kuimport bidhaa nje, kinachotokea ni uhaba wa dollar.

Ni aibu sana tumepungukiwa dollar mpaka juzi kati IMF wametupa msaada wa US$150 million uende hazina kwa sababu ya dollar shortage.

MY TAKE:
Naona Tanzania tumekuwa na kasi ya kukopa sana. Hizi billions of money tunazokopa kwa nini usimshauri bimkubwa kiasi fulani kiingizwe kwenye manufacturing?

Tuwekeze kwenye Import Substitution Industrialization (ISI). Tuanze kutengeneza wenyewe baadhi ya bidhaa muhimu ambazo tunaona zinatumalizia dollar kwa kuagiza kutoka nje.

Na ninaamini kwenye hizo bidhaa tutakazozalisha licha ya kupunguza importation tutapata na za kuexport nje na tutaingiza dollar.

Tupunguze importation ya baadhi ya bidhaa muhimu tuwe tunatengeneza hapahapa Tanzania. Bila hivyo hili tatizo litaendelea miaka na miaka.

Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
Stow,

Wa nje wanatumia pesa zao kwa maana ipi? Pesa za mradi au pesa za matumizi yao binafsi?
 
Kama Wana pesa mbona miradi Yao imesimama? Kwa nini hawajengi Ili Waendelee kudai si Wana pesa? Labda pesa ya kuhonga.

Mnaotetea huu ujinga nadhani mtakuwa ni punguani mahala

Tumetengeneza mifumo migumu kwa wakandarasi wa ndani ili waonekane hawawezi na hawana hela. Bond zinataka hela nyingi.
Lakini sio kwamba kazi hawawezi. Siku hizi hata kazi ndogo tu wanafanya makampuni ya nje. Unajiuliza kwanini? Jibu liko wazi...hawana hela za kugawa kama wachina.
 
Mentality za kikoloni.
 
Mentality za kikoloni.

Na wanufaika wengine wa haya matatizo ni waheshimiwa, ambao wanawapambania sana wachina waendelee kutawala kazi za ukandarasi.
Ukienda kwenye bomba la mafuta, wachina wanapeana kazi hata kwa kampuni zisizo na uwezo za kichina, ambazo zinauza kazi kwa wazawa.
Unashangaa kwanini sisi kwenye tender za umma tunaweka kipaumbele kwao kwa sababu za uongo. Hii corruption level tuliyofikia ni msala. Tunajibomoa wenyewe tukifikiri tunajenga
 
Sababu HAWANA PESA km Wakandarasi wa NJE Wakandarasi wa Ndani wanategemea wapewe Pesa NDIO wafanye kazi km Pesa hakuna Kazi inadoda Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
Kama wanapesa mbona mkapa stadium wamekwama wanasubiri notice walipwe kwa awamu?.
 
Stow,

Wa nje wanatumia pesa zao kwa maana ipi? Pesa za mradi au pesa za matumizi yao binafsi?
Nitatoa mfano:

Kuna Mkandarasi X wa Mradi wa Umeme au Maji I think mojawapo kati hizo Ila nahisi ni Mradi wa Maji Mkoa fulani, Mkandarasi X ni Mkandarasi mzawa, alipewa tenda kwenye HUO Mradi Ila mradi Pesa ilichelewa kwa HIO ukakwama alichofanya alichukua Pesa yake akaongezea kwenye Mradi ili mradi uishe usisimame na NDIO wanavyofanya ni Pesa za Kampuni SIO Pesa za mtu binafsi, sasa SIO Wakandarasi wote wanaoweza kufanya HIVYO wengi wakikosa Pesa Mradi unafeli

Nahisi hapo nitakua nimeeleweka
 
Back
Top Bottom