Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

kama ulikua hujui nikwambie tu kuwa hao wakandarasi wa bongo ni tia maji sana, wengi wao ni wezi na hawako punctual kwenye kazi zao, uvivu [kazi ya mwezi itakamilika ndani ya mwaka kwa visingizio vingi sana] - talking from experience.
Shida vikazi vya miamia ndo mnawapa wazawa kazi za mabilion mnawapa wachina unawaza nini wewe mwaga pesa.
 
Sababu kubwa ni kwamba there's 'No Balance of Trade.'
Bidhaa nyingi sana kama siyo bidhaa karibia zote tunaagiza kutoka nje ya nchi hii, wakati huo huo sisi hatuna bidhaa yoyote ile ya maana ambayo tunauza nje ya nchi hii.
Kuna ma IT wengi Tanzania ambao wanaweza kutengeneza software na kuuza duniani kote ila shida ni upokeaji wa fedha.
Tanzania ni jehanamu, unanunua software kwa paypal ila huwezi kupokea pesa kutoka paypal😁😁😁😁. Ukiangalia viongozi wanakula rushwa, wanafanya ufisadi wa kila namna ila wanaogopa paypal.
 
Shida vikazi vya miamia ndo mnawapa wazawa kazi za mabilion mnawapa wachina unawaza nini wewe mwaga pesa.
Makandarasi wa kibongo hawana exposure, dili nyingi wanapewa na mzee kaishia darasa la saba unategemea nini apo au na ilo pia hujui?
 
Yaani thread zingine na justification ni vitu viwili tofauti daaah. Kiswahili hiki, kina maneno mengi sana.
Mfabo mtoa thread unayesema dollar zimeadimika, wewe dollar unatumia za kazi gani? Ukinijibu hili nitakujibu pia.
 
Muongo
 
Tuhamie BRICS
 
Sababu namba 2 Ndiyo ya msingi kunasababisha tusiwe wabunifu
 
Kuna kitu kinafichwa ....
Ni kwamba mradi wa ujenzi wa bwawa kufua umeme la Julius Nyerere zilikopwa hela kutoka nje kwa mfumo wa kibiashara ..
Yaani kulipa inakuwa na riba kubwa sana na kwa muda mfupi ..
Serikali inabidi kulipa deni hilo kwa haraka na ni kwa dollar..

Pia kuna miradi mikubwa sana inaendelea inayohitaji dollar nyingi sana kulipa nje ya nchi ..hasa ya ujenzi iliyoanzishwa miaka michache nyuma
 
Haya ndio madudu ya serikali ya CCM.
Kama nakosea niambie wapi
 
Kwani kukopa ni nini? Unakopa harafu unampa Mchina hapo unaingiliwa mara 2
 
Sawa kwa vile unashinda Jamii forum kusoma umbeya, ukitoka unaingia whatsApp kuangalia status, ukitoka hapo unaingia Youtube kuangalia video za Mwakatobe, ukitoka hapo unaingia tiktok na unamalizia facebook huwezi kuelewa ndiyo maana umeishia na jibu moja tu la muongo.
Mitandaoni kuna pesa nyingi sana shida mfumo wa upokeaji wa fedha. Kwa akili yako huwezi kuelewa kwasababu wewe ni msoma umbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…