Don K. “Mayaula Mayoni”, kiongozi wa Genge la wahalifu wa Pembejeo na bei ya korosho mikoa ya Kusini

Don K. “Mayaula Mayoni”, kiongozi wa Genge la wahalifu wa Pembejeo na bei ya korosho mikoa ya Kusini

Tryagain

Member
Joined
Nov 23, 2021
Posts
73
Reaction score
458
Serikali ifike mahali iondoe mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye korosho. Genge la walanguzi wa Don K. Mayaula Mayoni.

Mayaula Mayoni Don K ni mwenyeji wa mikoa inayolima Korosho, alipaswa kuwa sauti yetu sisi wakulima wa korosho. Ambao hatuhitaji korosho nyingi ila tunahitaji soko bora la Korosho, tunajua lipo ila kwa kuwa si mwenzetu umetumia korosho kama sehemu ya maslahi yake binafsi.

Mwalimu Mayaula Mayoni Don K uzalishaji wa Korosho umepungua, Anguko hili limetokana tamaa zako kwa sisi ndugu zako wakulima wa korosho kuuziwa pembejeo feki.

Don K upatikanaji hafifu wa Pembejeo uliosababishwa na genge lako kwa makusudi ulitulazimu kununua Pembejeo kwa gharama kubwa kutoka kwa watu ambaye mmoja kati yao alitajwa kwenye mkutano wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM kuwa kwenye Pembejeo hizi kuna mkono wako.

Changamoto ya kuuziwa Pembejeo Feki imesababisha kudorora kwa uzalishaji katika zao hili tegemezi kwa wakazi wa Kusini. Hivi Mayaula Mayoni huoni aibu kwenye hili sisi shangazi zako na Baba na Mama zako kununua pembejeo feki.?

Wakulima wengi wameitupia lawama Serikali ambayo kimsingi ndiyo yenye dhamana ya kubeba mzigo wa lawama na kuwajibika kwa kusababisha uzalishaji wa korosho kushuka na bei kuporomoka katika msimu wa mwaka huu.

Wengi wana maswali juu ya vyombo vya dola vilikuwa wapi wakati sisi tunauziwa Pembejeo feki…? Mkono wako ni mrefu unalotaka lifanyike linafanyika Don K iwe Lindi, Mtwara hata Ruvuma kufika hadi Mafia.

Ukweli ni kwamba changamoto ya uhaba na kucheleweshwa pembejeo na bei ya pembejeo ni mchezo uliochezwa kati ya vyama vya ushirika na wafanyabiashara washirika wa Mayaula Mayoni Don K sisi wakulima wa Mtwara tulimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ndiyo sababu kubwa ila wapo wengi. Mhalifu huyu mshirika wa Don K alisababisha wakulima kununua pembejeo feki kwa gharama kubwa pasipo kujali kuwa anasababisha hasara kwa wakulima na Serikali.

Licha ya Serikali yenyewe kupitia wizara ya kilimo iliahidi kutoa pembejeo bure! Ahadi hii ya serikali kugawa bure pembejeo iligubikwa na ukiritimba kutoka kwa wauzaji wa pembejeo hasa Salfa ambao walificha pembejeo hizi na kupelekea uhaba na kufanya mahitaji kutotoshelezeka.

Jambo hili lilipelekea kuwe na uhaba mkubwa wa pembejeo na mahitaji kuwa makubwa Hivyo kusababisha pembejeo chache iliyokuwepo kuuzwa kwa bei kubwa kutokana na mahitaji kuwa makubwa hali iliyopelekea Wananchi kununua Pembejeo feki kutoka kwa Don K.

Pamoja na suala la Pembejeo Kuna suala la kupanga bei jambo hili nalo ni usiri mkubwa na mienendo ya ulaji na makubaliano ya gizani kati ya vyama vya ushirika na wanunuzi kuna kampuni ambayo ni washirika wa Don K kutoka Vietnam inayoitwa Sibatanza hii kampuni imeshiriki kwa namna moja au nyingine kutengeneza mianya ya ulaji kutoka kwa vyama vya ushirika na kuwanyonya wakulima wa korosho.

Licha ya Serikali kuweka bei Elekezi, Genge la Don K akishirikiana na wenye hila na kupanga mikakati na vyama vya ushirika na wanunuzi kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kuenda sambamba na bei elekezi kutoka serikalini.

Don K Mayaula Mayoni wewe ni mnyongaji wetu namba moja na wala si sauti yetu wakulima wa Korosho Mtwara tunamuomba Mhe. Rais kuingilia kati usambazwaji wa Pembejeo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 kuepuka haya mambo kujirudia.

Genge la Don K Mayaula Mayoni lina nguvu huko mikoa ya Kusini haligusiki linatishia ustawi wa zao la Korosho, Wabunge wote ni Genge la Don K ndiyo maana hutasikia popote pale kelele hizi za Pembejeo na Uhuni wa upangaji bei kupitia stakabadhi ghalani.
 
Ila Mayaula Mayoni si ni jina la aliyekuwa Mwanamuziki wa Congo?, bila shaka huyo "muhalifu" ana jina lake halali.

Ila poleni kwa mitihani, ndio nchi za Kiafrica hizo...huko kwa Wenzetu wapo makini sana na Kilimo ngumu kukuta hujuma za kiholela.
 
Majuzi niliona wakulima wa alizeti wakilia kilio cha samaki baada ya mbegu za ruzuku walizopewa na serikali kuwa ni feki....mkulima mmoja alikuja na sampuli ya hizo mbegu walizopewa na kumuonyesha mkuu wa Mkoa, naamini hadi kesho hiyo msambazaji wa mbegu yupo zake anadunda mtaani na Mama kaenda kutafuta pesa za kumlipa ili mwakani asambaze mbegu zingine feki!
 
Kweli Don K Mayaula anatisha sana nadhani mama anayo yote ni suala la muda tu
 
Asee mayaula mayoni ana nyimbo kali Sana hasa kwa SS wahenga

Vp DIBLO DIBALA naye
Unamuelezeaje


Nipo zangu hapa RUANGWA nataka kulichukua Jimbo hili
 
Back
Top Bottom