Don Williams V/S Kenny Rogers

kwang wote ni wazuri inaniwia vigumu sana kumchagua mmoja ila nikisikiliza nyimbo zao wote wawili nafarijika sanaa especially senorita ya don na luccile ya kenny rogers
 
yaah kuna show moja niliitazama youtube alitoa kisa cha huo wimbo kuwa umebeba uhalisia kutoka kwenye maisha yake. Ametokea familia ya maisha duni ila alipambana na akaweza kuinyanyua kwa kipaji chake.
Kweli
 
 
Jamani jamani mm hawa wote kwangu nawapa 50/50 yaan nawakubali balaa nikisikiliza nyimbo zao huwa sometime nahisi machozi yananitoka
 
Umeshawahi kujaribu kuimba? Barry White na Leonard Cohen (RIP) walikuwa wakiunguruma tu na siyo kuimba na bado wamependwa sana duniani. Yaani akina Dada walikuwa wakisikia sauti ni lowolowo 🙂
Usikate tamaa, jaribu shule za waimbaji. Anzia hata kanisani.

Kwa kweli wote wakali
Na wote wana sauti ya ajabu
Ila hii something Inside So Strong aliimba jamaa mmoja mweusi anaitwa Labi Siffre ni masterpiece kwa kweli
Kuna watu wana vipaji
Sijui kwanini sikuwa mwimbaji hahaha
 
Hahaaha too old for that now
Ingawa hata kina Rolling stones waliungana tena wakiwa wazee lakini walikubalika na wakajaza watu kibao
Ngoja nijaribu kuimba za watu kama alivyokuwa Demis Roussos
 
Naomba nianze kwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa mkuu dawa yenu, pia shukrani za dhati kwa rafiki yangu wa karibu sana ambaye ni kama ndugu kwa kunifahamisha huu mjadala kwani sikuwa hewani kwa muda flani pili wachangiaji wote wa mada hii husika kwani nimefarijika kuona muziki wa country bado kuna watu wana uelewa vzr kabisa. Nami narudi kwenye upigaji wa kura na moja kwa moja kura yangu inamuangukia don Williams lakini hii ni kwa sababu ya kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa nyimbo zaidi ya 10 zenye mvuto uleule sawa na wimbo wa kwanza kuanzia kwenye mashairi na mpangirio wa ala za muziki ndani yake, lakini pia nisimuache mbali mzee wangu wa kazi Kenny R kwani nae hakuwa nyuma kwenye kutoa vitu vikali vyenye stori za maisha kali na mpangilio wa ala za muziki kali sana, mbali na hayo yote kura yangu imemuangukia Mzee don(rip) na heshima zangu zote nazielekeza kwao wote manguri wa muziki nina mengi sana ya kuongea lakini ningeomba baada ya muda kadhaa mkuu dawa yenu utupe idadi ya kura zilizopigwa( i salute all country music lovers)
 
Wimbo wa Lucille-Kenny Rogers...Naukubali mno.
 
Nimepokea hiyo shukrani kwa mikono miwili mkuu, naona wengi mpo upande wa Don, kiuhalisia kashinda na bahati nzuri watu wamekuwa wakitoa na sababu pia za kumpitisha....
 
Kamwe huwezi kumlinganisha the humble giant of country music na Kenny Rodgers. Don ni hatari aisee.

Kenny rodgers ni nyimbo tatu tuu ndio maarufu The Gambler, coward of the county, lucine and island in the stream fet dolly parton

Consigliere
Achaa kudanganya were
She believe me
Loving arms
 
Nimepokea hiyo shukrani kwa mikono miwili mkuu, naona wengi mpo upande wa Don, kiuhalisia kashinda na bahati nzuri watu wamekuwa wakitoa na sababu pia za kumpitisha....
Pamoja sana mkuu wacha tuendelee kuufurahia huu muziki mtam wa country
 
Nadhani sio lazima wakati wote tuwe na mshindi mmoja,leo naomba niseme kwenye country kuna washindi wawili nimeshindwa kuchagua asee.

So true hata mimi nimekwama hapa

Don Williams-I believe in you,Listen to the radio,your my best friend,Some broken hearts never mend,senorita....and the list goes on

Kenny Rogers-The Coward of the County,Day time Friends,Gambler,Lucile and the list goes on
 
Sijawasikiliza sana wanawake ila mpaka sasa ninayemkubali ni Dolly Patron hasa kupitia ngoma yake ya many colours

I will always love you .Dolly Patron ni habari nyingine kwa kina Mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…