Donald Trump ashangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai

Kwa sisi tuliosomea Cuba tunafahamu vizuri kwamba lile lilikuwa dongo kwa wale viongozi wengine waliotumia muda uliobaki kuongea vifaransa vyao, mpaka alipowastopisha kwa kisingizio cha muda mchache wa maongezi uliobaki.

Unawambiaje watu eti umebaki na muda mchache wa maongezi, na wakati umewaalika kwako wewe mwenyewe!

Trump huwa hapendi kusikia lugha nyingine kinyume na English, ndio maana kipindi kile cha operation ya kwanza ya wahamiaji haramu nchini kwake aliwahi kusema kuwa lugha ya Marekani ni English tu na sio Hispanish wala lugha nyingine yoyote. Lengo likiwa mtu yeyote anaeongea Hispanish aonekane ni mhamiaji haramu kutokea Mexico, Venezuela na nchi nyingine za Amerika ya Kusini.

Alisema hivyo huku akifahamu fika kuwa Marekani kuna wamarekani wenye asili ya Mexico, haswa katika majimbo yaliopo mpakani na Mexico wanaongea ki hispanish kama lugha yao mama.

Ukiangalia raisi wa Liberia aliongea English ya kawaida sana, ila kwa vile alikuwa na lake jambo kwa waongea French, basi akaamua kutumia English cha raisi wa Liberia kama kichaka cha kutaka na wengine wakajifunze English, ili wakiwa wanaenda White House waende wakaongea English wasifiwe kama mwenzao.

Angalia Ilipofika tu zamu ya waongea kifaransa. Trump hakutaka kutumia muda kuwasikiliza au kuvaa lile dude masikioni.. alichofanya aliomba tu majina yao na nchi wanazotoka, na kuwaambia nashukuru kwa kuja kwenu.

Jamaa hakupenda kuendelea kusikiliza french akaomba mkutano uishe haraka haraka kwa lengo la kukwepa kusikiliza kifaransa muda mrefu 🤣🤣🤣🤣
Hata mimi kuna lugha sizipendi, mfano kichina
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameshangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai:

"Asante, na Kiingereza kizuri namna hii, kizuri sana. Ulijifunzia wapi kuzungumza kwa uzuri namna hii, wapi? Ulisoma wapi? Liberia?," alihoji.

Trump amewakaribisha viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa ajili ya majadiliano na chakula cha mchana Ikulu ya White House Jumatano hii, ambapo mazungumzo hayo yanalenga fursa za kibiashara.

Wamarekani ni wapumbavu sana.
 
Ina maana hajui kua Liberia ilikua Koloni la Marekani? hajui kama watu wa Liberia wanazungumza Kiingereza cha kimarekani? kumuuliza amesomea wapi ni ujinga pia
Liberia haikutawaliwa na marekani haijawahi tawala nchi yoyote ila liberia ni nchi iliyoundwa na wamarekani weusi walio kuwa utumwani america na kuamua kurudi nyumbani africa
 
Ni kweli, kuna lugha ambazo zikiongelewa hata dakika 5 kwenye masikio yako unahisi kichwa kinakuuma kuzisikia 🤣🤣
kipindi niko chuo nilikaa hostel na mshkaji mmoja wa manyara, ebanaeee yule jamaaa ni mtu poa sana mstaarabu.

ikifika usiku nimelala yeye midahiyo yeye anaongea na dem wake wa kijijini kwao kimanyara, aloo iyo lugha ikiongewa huwezi kupata usingizi kama umemeza dawa za kuzuia usingizi na jamaa anaongea masaa2+

ilibidi nimwambie jamaa, mimi sina shida ya kisikia anachoongeaga na dem wake daily. ila kama dem wake anajua kiswahili au lugha nyingine yoyote ambayo haizuii usinginzi bas watumie lugha hiyo tofauti na wanavyofanya.

Kuna lugha zinakera hatari.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameshangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai:

"Asante, na Kiingereza kizuri namna hii, kizuri sana. Ulijifunzia wapi kuzungumza kwa uzuri namna hii, wapi? Ulisoma wapi? Liberia?," alihoji.

Trump amewakaribisha viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa ajili ya majadiliano na chakula cha mchana Ikulu ya White House Jumatano hii, ambapo mazungumzo hayo yanalenga fursa za kibiashara.

Wakati mwingine Trump ukurupuka sana, ni bingwa wa kutisha tisha mataifa ambayo ni weak au ambao ni washindani wa kiuchumi na kijeshi wa USA.

We fikiria hana habari kwamba Taifa LA Liberia lilianzishwa na watumwa walizaliwa na kuishi w Merikana kabla hawajarudi Africa magharibi miaka ya zamani ndio maana walirithi kingereza kilicho kuwa kinazungumzwa na babu na babu zao, kwani hilo Trump halijui??
 
Huyo ndiye Trump,umpende au umchukie poa tu.The old-babu knows how the game is supposed to be played!
 
🫸🫷
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameshangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai:

"Asante, na Kiingereza kizuri namna hii, kizuri sana. Ulijifunzia wapi kuzungumza kwa uzuri namna hii, wapi? Ulisoma wapi? Liberia?," alihoji.

Trump amewakaribisha viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa ajili ya majadiliano na chakula cha mchana Ikulu ya White House Jumatano hii, ambapo mazungumzo hayo yanalenga fursa za kibiashara.

Kunatofauti ya kiingereza na kigugumiziii..😁😅😊☺️

Umesoma wap ?! Trump kashangaa Sana angekua mwingine hapoo the the the..

Yaan wa Liberia na marekani ni BROTHER & SISTERS maana kwenye BACK TO AFRICA MOVEMENT Kuna more blacks walirudi na kukaa Liberia ndio maana hata wazungu na black Americans wengi unawapata LIBERIA mfano Charles Taylor mbabe wa vita alikua ni shombe la black American na mzungu.

Kwaio hata lugha lazima ipande sio Mimi mmakonde au msukuma KINGEREZA ni Lugha yangu ya Tatu unakuta pronunciation mbovu na hata KINGEREZA haki nyookii vyema na kukandamiza maneno.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameshangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai:

"Asante, na Kiingereza kizuri namna hii, kizuri sana. Ulijifunzia wapi kuzungumza kwa uzuri namna hii, wapi? Ulisoma wapi? Liberia?," alihoji.

Trump amewakaribisha viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa ajili ya majadiliano na chakula cha mchana Ikulu ya White House Jumatano hii, ambapo mazungumzo hayo yanalenga fursa za kibiashara.

Huyu na Magu wanaendana sana mambo yao.
 
Protocol ni vyema kweli kumwambia Raisi mwingine mbele ya vyombo vya habari kuwa ulisoma wapi?
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameshangazwa na Kiingereza kizuri cha Rais wa Liberia Joseph Boakai:

"Asante, na Kiingereza kizuri namna hii, kizuri sana. Ulijifunzia wapi kuzungumza kwa uzuri namna hii, wapi? Ulisoma wapi? Liberia?," alihoji.

Trump amewakaribisha viongozi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa ajili ya majadiliano na chakula cha mchana Ikulu ya White House Jumatano hii, ambapo mazungumzo hayo yanalenga fursa za kibiashara.

Lini mama atasi?fiwa
 
Ni kawaida kwa mwanasiasa kudidtract attention ili uweze kuwin maongezi. Hiyo ni technicalities tu za uongeaji.
 
Ukiwa unajua kiingereza watakusifia sana,ukiwa unajua kutengeza nuke,kuboresha uchumi wako,kiasi cha fuel kuuzwa bei ndogo kuliko maji kama IRAN,ukianza kuzitumia rasilimali zako effectively 100% unazimiliki kama Afghanistan,unakua ADUI.................kusifiana ujinga tu
Acha ugaidi
 
Back
Top Bottom