Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

20241106_114246.jpg
 
Imetangazwa dakika chache zilizopita na vyombo vya Habari

=====

Rais wa zamani Donald Trump kutoka chama cha Republican, ameshinda Uchaguzi wa Marekani.
View attachment 3144969
Chanzo: Spectator Index

Donald Trump ameoa mara tatu, Ivana na Marla Maples, mke wa kwanza na wa pili mtawalia ambao wote ametalikiana nao. Mke wake wa sasa ni Bi Melania.

Bwana Trump ana watoto watoto watano, watatu wa kiume Donald Trump Jr, Eric, Barron na watoto wawili wa kike Ivanka na Tiffany.

Rais huyo wa Zamani wa Marekani alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita.

Babake Fred alikuwa tajiri aliyemilki majumba na babu zake Trump walikua wahamiaji kutoka Ujerumani.

Mamake Mary alikuwa mzaliwa wa Scotland.
View attachment 3144983
Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York.

Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968.

Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa New York.

Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn.

Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980.

Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump.

Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.
Bora kashinda trump
 
.Wamarekani walionekana kumkubali sana mwanamama Kamala Haris. Ila lilipofika suala la kupiga kura ya urais, wakatafakari mara ya pili. Kuwa Mwanamke aongoze nchi? Inawezekana? Hapo ndipo wakatulia na kupata majibu,wakamtosa wakamchagua kaburu Trump. Watanzania tuwe na la kujifunza hasa linapokuja
suala la kuongoza nchi.
Sema wewe hutamchagua. Mimi nitamchagua Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan. Kwa nini? Kazi alizofanya ni uthibitisho kujadili jinsia ktk uongozi ni primitive nonsense. Muhimu ni merits na Mhe. Samia anazo za juu.🙏🙏🙏
 
.Wamarekani walionekana kumkubali sana mwanamama Kamala Haris. Ila lilipofika suala la kupiga kura ya urais, wakatafakari mara ya pili. Kuwa Mwanamke aongoze nchi? Inawezekana? Hapo ndipo wakatulia na kupata majibu,wakamtosa wakamchagua kaburu Trump. Watanzania tuwe na la kujifunza hasa linapokuja
suala la kuongoza nchi.
Taifa kubwa kama Marekani si rahisi kuongozwa na mwanamama ni nchi zetu hizi tu ndo zinaongozwa na akina mama sababu hazina impact yoyote ulimwenguni.
 
.Wamarekani walionekana kumkubali sana mwanamama Kamala Haris. Ila lilipofika suala la kupiga kura ya urais, wakatafakari mara ya pili. Kuwa Mwanamke aongoze nchi? Inawezekana? Hapo ndipo wakatulia na kupata majibu,wakamtosa wakamchagua kaburu Trump. Watanzania tuwe na la kujifunza hasa linapokuja
suala la kuongoza nchi.
Tunaishukuru sana serikali ya mama kwa kufanikisha hili la nchi kubwa kukataa kuongozwa na mwanamke!
 
Urafiki lazima kuna tabia zinafanan Trump hapendi upumbavu lazima atamwambia mshikaji wake Putin rudisha majimbo ya Ukrein vita inaisha
Yale majimbo kurudi ni ndoto za Alinacha, mkuu. Labda mrudishe gharama zooote ambazo Russia imetumia tangu kuanza kwa SMO, jumlisha vikwazo, jumlisha vilema na vifo, pamoja na hasara za kibiashara na kiuchumi na kashfa mbaya dhidi yake.

Hapo bado sijataja ile Nord Stream II ambayo Marekani aliilipua kisha akamsakazia Putin. Bado hasara za wabia wa Urusi kama bosi wa Chelsea na klabu yake. Mabenki? Makampuni?

Kifupi, kama Google tu imetozwa faini ya dola desilioni 20 (sifuri 33!), unadhani Marekani inaweza kutozwa fidia kiasi gani kwenye hili?
 
Huyo amekurupuka usingizini, arudi kulala.

Trump atamwambia Putin abaki na alichomega, huku kichaa Zele akae kwa kutulia vita isitishwe (Isitishwe kwa maana Putin lazima atakuja kuiendeleza au vizazi vijavyo hadi lengo lao litimie)
 
.Wamarekani walionekana kumkubali sana mwanamama Kamala Haris. Ila lilipofika suala la kupiga kura ya urais, wakatafakari mara ya pili. Kuwa Mwanamke aongoze nchi? Inawezekana? Hapo ndipo wakatulia na kupata majibu,wakamtosa wakamchagua kaburu Trump. Watanzania tuwe na la kujifunza hasa linapokuja
suala la kuongoza nchi.
Tunazingatia
 
Back
Top Bottom