Donald Trump plans to shut dozens of US embassies – including 8 in Africa

Donald Trump plans to shut dozens of US embassies – including 8 in Africa

Ni kweli mkuu lakini ni ujinga wa mwafrika tu. Sasa hivi watu wa Trump wameingia mpaka vyuoni kunyang'anya wanafunzi viza hasa wale walioshiriki kupinga yanayoendelea Gaza. Yaani ile nchi tuliyokuwa tunaambiwa ni mfano wa demokrasia sasa inageuka kwa kasi sana. Nimesema ni ujinga wetu kwani tungungana wote leo na kuwaambia wafunge balozi zao zote Afrika basi angeomba poo.
Watu wasome alama za nyakati, Africa hawawezi kuungana sababu muungano unataka long run plans ambayo hatuna. Africa tumeamua ile inayoitwa tupo tupo tu ilimradi
 
Nimeamini mzee anajiandaa na vita na iran
Ndio Mana anaharikisha vita vya ukraine viishe upesi
Mi nahisi China ndio maana anataka kujiondoa Ukraine, ili kujipanga zaidi. Ni kama walivyoondoka Afghanstan kwa haraka kama wamefukuzwa , kube walijua kuna vita ya Ukraine na Russia, walihisi ingesambaa zaidi lakini mpaka sasa bado iko pale plae.
 
Serikali ya Tanzania nayo iige kupunguza matumizi ya safari za Dodoma- Dar es Salaam, gari za kifahari za serikali, manunuzi ya fenicha kutoka nje ya nchi, tiketi za first class na business class kwa vigogo wa serikali zifutwe,,malipo ya nyumba ya maji, umeme, simu za mkononi za maofisa wa serikali zifutwe, safari za kwenda kushuhudia bajeti zao kusomwa bungeni zifutwe n.k n.k
haya yakitokea bongo basi ujue kenge siku hiyo atajua kucheza disco! au nguruwe kuruka angani!
 
Ni kweli mkuu lakini ni ujinga wa mwafrika tu. Sasa hivi watu wa Trump wameingia mpaka vyuoni kunyang'anya wanafunzi viza hasa wale walioshiriki kupinga yanayoendelea Gaza. Yaani ile nchi tuliyokuwa tunaambiwa ni mfano wa demokrasia sasa inageuka kwa kasi sana. Nimesema ni ujinga wetu kwani tungungana wote leo na kuwaambia wafunge balozi zao zote Afrika basi angeomba poo.
ncha ya mkuki haipigwi ngumi! hivi venezuela mkate mmoja kununua ni big deal!toilet paper hakuna dukani! dawa ya mswaki kwa folleni ingawa kuna wese la nguvu. nakupa wiki mbili tuu utaona pale bukina faso bei ya kisamvu itapanda,mihogo na matoke kitafunio cha anasa! watu kula misumali ya bati(dagaa) siku za sherehe ya harusi! usipige ngumi ncha ya mkuki!
 
Trump alichowafanyia wamarekani kawarudisha kwenye ujima na mwakani chama chake kitapoteza wabunge na wawakilishi wengi
dua la mbuzi halimpati chui! wewe badala ya kumtukana IRAN kujifanya mbabe unakalia mambo ya marekani.kumbuka ukiwa kipenzi cha israel na mungu anakubariki 70x70
 
dua la mbuzi halimpati chui! wewe badala ya kumtukana IRAN kujifanya mbabe unakalia mambo ya marekani.kumbuka ukiwa kipenzi cha israel na mungu anakubariki 70x70
Vilaza tayari mmeshaiingilia mada....
 
20 Aprili 2025
Bujumbura, Burundi

Uholanzi inafunga ubalozi wake mjini Bujumbura: uamuzi wenye athari kubwa kwa ushirikiano wa nchi mbili​



Serikali ya Uholanzi imetangaza kufungwa kwa mawasilisho yake kadhaa ya kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa na utawala mkuu umejikita, kama sehemu ya upangaji upya wa kimkakati wa mtandao wake wa kidiplomasia. Uamuzi huu unakuja wakati Uholanzi imekuwa mshirika mkuu wa maendeleo nchini Burundi.

Katika barua kwa Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Mambo ya Nje Caspar Veldkamp alisema:

“Ninakusudia kufunga balozi tano na balozi mbili za jumla: Bujumbura (Burundi), Havana (Cuba), Juba (Sudan Kusini), Tripoli (Libya), Yangon (Myanmar), ubalozi mdogo wa Antwerp na ubalozi mdogo wa Rio de Janeiro.
Hatua hii ni sehemu ya sera ya kupunguza bajeti inayolenga kuokoa euro milioni 25. Serikali ya Uholanzi, ikiungwa mkono na vyama kama vile PVV, VVD, NSC na BBB, inatafuta kupunguza matumizi ya umma, ikiwa ni pamoja na kupunguza 22% ya bajeti katika wizara kadhaa.

Mshirika mkuu wa maendeleo wa Burundi

Kufungwa kwa ubalozi huo mjini Bujumbura kunaweza kuwa na athari kubwa katika ushirikiano wa pande mbili. Uholanzi imekuwa mojawapo ya wafadhili wakubwa wa Burundi, ikiwa na wastani wa dola milioni 33.9 za misaada ya kila mwaka mwaka 2022, kulingana na data ya Benki ya Dunia.

Kati ya 2023 na 2027, Uholanzi ilikuwa imetenga Euro milioni 160 kusaidia sekta mbalimbali nchini Burundi, ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula, afya ya uzazi, haki za binadamu na ajira kwa vijana.


Ahadi ya Uholanzi imesababisha miradi kadhaa madhubuti:

Ruzuku ya dola milioni 7.8 kwa afya ya uzazi, inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanawake.

Ufadhili wa euro milioni 10 kwa Mfuko wa Pamoja wa Mbolea na Marekebisho, kusaidia kilimo cha Burundi.

Mchango wa euro milioni moja kwa Sensa ya Jumla ya Kilimo na Mifugo, kwa ushirikiano na UNFPA na FAO.

Kuelekea ufafanuzi upya wa ushirikiano

Licha ya kufungwa kwa ubalozi huo, Uholanzi ilionyesha nia yake ya kudumisha dhamira yake kwa maendeleo ya Burundi. Waziri Veldkamp alionyesha kuwa uwakilishi unaweza kufunguliwa katika maeneo mengine kulingana na maendeleo ya kijiografia, haswa katika Mashariki ya Kati.

Mamlaka ya Burundi na washirika wa ndani wanatumai kuwa upangaji upya huu hautahatarisha miradi inayoendelea na kwamba ushirikiano unaweza kuendelea kwa njia zingine.
 
Back
Top Bottom