Dondoo na uchambuzi kuelekea mechi ya Watani wa Jadi

Dondoo na uchambuzi kuelekea mechi ya Watani wa Jadi

endesha

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2015
Posts
1,297
Reaction score
1,877
Siku zinazidi kuchanja mbuga kuelekea pambano la kukata na shoka Kama sio Mundu Kati ya Watani wa Jadi Katika uwanja wa Benjamini Mkapa.Mchezo huo utachezwa majira ya saa 11:00 Jioni

Kuelekea Mchezo huo ,Japo kivyovyote Kama tunavyojua Derby siku zote hua haingalii saaana performance ya Timu Katika wakati husika hasa Kama nyingine inachechemea.Lakini watu wengi hasa wanaojua mpira wa miguu wanaipa nafasi kubwa Simba kuibuka na ushindi mnono Katika pambano Hilo.

Nami naungana nao na Natabiri Mechi hii kuisha kwa Simba SC kuichakaza Yanga bila Huruma goli 3-1.Nitaendelea kuleta Dondoo,Uchambuzi makini na taarifa mbalimbali Mimi Kama mchambuzi mahiri kabisa hapa Jamiiforums kuelekea pambano hilo.

Karibu nawe mwanamichezo mwenzangu kwa utabiri, pamoja na uchambuzi kwa wenye uwezo wa uchambuzi Kama mimi.

UCHAMBUZI
Kuelekea Mechi hii,Kama nilivyosema Awali.Simba wanaenda kwenye mchezo huu wakiwa na Ari na Jeuri kubwa ya kujiamini.Naamini hata Mashabiki watakaofika uwanjani siku ya Jumamosi wengi mno watakua Ni wa Simba kutokana na sababu mbili hapo juu.

Simba hii inaweza kuwaathiri Kama wataingia kwa kujiamini saaana na kuwadharau wapinzani wao ambao kwa vyovyote wataingia wakitaka kutopoteza Mechi hiyo.Hii Ni kwa sababu kuu mbili.Sababu kubwa Ni ili kuwafuta machozi Mashabiki wao ambao kwa namna moja ama nyingine wameshakata tamaa ya ubingwa .Pili Ni kwa sababu ya aina ya mchezo(Watani wa Jadi).Kwa Hiyo Simba sababu ya kushinda Ni juu yao ,hasa ukizingatia ya kwamba Wana kikosi Bora chenye Ari na uwezo kuliko Cha Yanga .Ila wakiingia na mentality ya kwamba Yanga Ni dhaifu ,usije kushangaa Yanga ikatoka na sare Katika game Hiyo ama hata ushindi pia.

Ushindi kwa Simba uko juu yao,washindwe Wenyewe tu

YANGA
Yanga Ni timu nzuri pia,si timu ya kuibeza na kuishusha hadhi hata kidogo.Naamini Pa1 na kwamba walianza msimu vizuri .Isingekua Pressure ya viongozi na Mashabiki wao hakika Yanga wangeendelea na spirit Ya kupambana Sasa Hivi kwenye msimamo wa Ligi na mbio za ubingwa tungekua tunaongea mengine.

Ila kuelekea Mechi hii,Yanga wataingia Kama Wanyonge(Underdog).Hii inaweza kuwafanya waiheshimu Simba na Kama Simba wataidharau Kama nilivyotanabaisha juu Basi wanaweza kuondoka na chochote Katika game hii.

Sehemu kubwa iliyowaangusha Yanga msimu huu Ni sehemu ya ushambuliaji.Na ukiangalia Safu ya ushambuliaji ya Yanga Ni tofauti mno na ya Simba.Na hii inadhihirishwa na magoli yaliyofungwa mpaka Sasa na timu zote mbili.

Yote kwa yote Yanga waingie kwenye Mechi hii kuiheshimu Simba ambayo Kama wataingia kwa kuzingatia niliyotahadharisha awali,Basi Yanga anaweza kupoteza Mechi hii kwa tofauti kubwa kidogo ya magoli.Kuiheshimu Simba kutawafanya nao kujipanga na Pengine kuendana na makali yao.

Kesho nitakuja na kikosi kinachotegemewa kuanza Jumamosi Pamoja na Udhaifu ,uimara ,mfumo kwa Timu zote mbili.Soka Ni burudani na hakika Jumamosi tunategemea kuangalia Mechi yenye ushindani kwa Timu zote mbili.Ahsante

Da Gladiator ,financial services,Shadeeya ,Van De Beek
 
DERBY YA KARIAKOO SIKU ZOTE HAIELEWEKI NA FORM YA TIMU KWENYE LIGI ISIKUPE KIBURI KUWA MTASHINDA NYIE MIKIA... YANGA HUBADILIKA SANA KWENYE DERBY
Endelea kujipa moyo,ila ukweli Simba wanakila sababu ya kuifunga Yanga na Yanga wanakila sababu ya kufungwa na Simba kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja.
 
DERBY YA KARIAKOO SIKU ZOTE HAIELEWEKI NA FORM YA TIMU KWENYE LIGI ISIKUPE KIBURI KUWA MTASHINDA NYIE MIKIA... YANGA HUBADILIKA SANA KWENYE DERBY
Yaani Sarpong,Nchimbi na Fiston wabadilike kisa derby walikuwa wapi kubadilika siku zote hizo wakati timu lenu linapoteza points kizembe na kupoteza matumaini ya ubingwa Vpl
 
Kuna watu wanasema "..derby huwa haiathiriwi na performance ya timu husika..." Watu kama hao technically wanakua wamekiri kuwa timu lao ni bovu na mpinzani ni bora kuliko wao ila wanategemea maajabu hayo ya derby.
 
Back
Top Bottom