Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
▶️DONDOO ZA JIKONI:-
1🧂Ukiandaa nyama kwa viungo kama tangawizi, thomu na masala ongeza mafuta kidogo na mtindi vijiko viwili utafurahi.
2🧂Ukikosa vanilla unaweza saga ganda la limao bichi linaleta harufu nzuri kwenye keki na chapati za maji.
3🧂Ukipika mboga ya karanga tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga.
4🧂Ukiunguza wali penyeza mapande makubwa ya pilipili hoho inatoa kbs harufu ya kuungua.
5🧂Ukiona mafuta yamezidi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa silesi kupitisha kwa juu itanyonya mafuta.
6🧂Ukitaka maharage yawe na rojo zuri pale unapoyachemsha weka na mafuta ya kupikia kidogo yawive pamoja.
7🧂Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu chemshia pamoja na mchaichai inakuwa nzuri sana.
8🧂Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe laini ichovye kwenye maji baridi na uipashe bila mafuta itakuwa kama ndio umeipika muda huo.
9🧂Ukipika matembele jaribu kuweka tangawizi na pilipili manga utajionea maajabu.
10🧂Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung'ang'ania kwenye chuma unapowakaanga tengeneza rojo ya ngano wachovye pia huwa ni watamu sana.
11🧂Ukitaka utumbo iwive haraka weka limao bila ya chumvi kwa yale maji ya kwanza.
12🧂Chumvi ikizidi kwenye mchuzi menya kiazi mbatata weka ganda lake acha uchemke chumvi itapungua sana.
13🧂Maharage ukitaka yawive upesi weka kijiko kimoja cha baking powder.
14🧂Mchuzi ukitaka uwe na rojo zito na huna nyanya za kutosha koroga kijiko kimoja cha unga wa ngano weka na acha uchemke.
15🧂Muhogo ukiwa chelema weka kijiko kimoja cha baking powder.
16🧂Nyama ikiwa ngumu au ukitaka ilainike vizuri kwangulia papai bichi.
17🧂Karoti zikisinyaa kwa kukaa muda mrefu ziweke kwenye maji baridi kwa nusu saa zitakuwa kama zimetoka shamba.
18🧂Kama unatumia jiko la gas kupikia basi tumia maji baridi kupikia wali utaona mambo.
19🧂Ukiunguza wali kwa mara nyingine kata kitunguu maji nusu kiweke katikati harufu ya kuungua hutoweka.