Dondoo za masomo ya PhD UDSM

Kusoma SUA kunataka moyo sana na navyosikia na UDSM pia
Mimi nina watu wapo hapo, yaani kuna hao madoctor na maprofesor yaani wanatia vichomi watu. Kama huna muda wa kumsimamia mtu si lazima uwe unasimamia wanafunzi, yaan nimekuwa nikiwatia watu moyo ili wamalize maana washaanza na ada wamelipa ila mimi siendi. Na hivi karibu baraza limekaa la senate kusema ukichelewa utalipa ada nzima 4mil badala ya 50000, huoni kama ni ujinga wakati wao wenyewe ndio wanasababisha kwa kweli
 
Ni upuuzi sana yani, apo unakuta mtu Hana scholarship wala funding yoyote anajisomesha mwenyewe halafu unamletea mambo kama haya
 
elimu ambayo itabaki ngumu ni degree ya kwanza tu huo ndio ukweli lakini degree ya pili kama supervisor yupo kawaida anazingatia muda utamaliza kwa wakati wale waliosoma ulaya wanajua ukishomba kusoma degree ya pili mwanafunzi lazima uwe na ratiba ya kuonyesha utapeleka lini research title, chapter one ni lini chapter two ni lini chapter three ni lini na hapo supervisor ukiikosea anakurekebisha tena anasema fanya hivi na hivi umalize hapa sasa paskistani tatizo linaanza kwenye title tu ndio shida inaanzia hapo vyuo vingi havina ratiba ya kumubana supervisor akamiilishe kazi kwa wakati walishakuwa miungu watu wakisingizia wana kazi nyingi
 
u love to stress yourself.

PhD ya nini sasa mkuu?

Au unataka excuse ya kutokuwa na hela?

Kwamba uwaambie watu bado unasoma ndio maana hauna hela?
 
Jaribu Open university
Aliye kuambia Open University ni rahisi ni nani? Kwenye list ya SUA
Nimeona watu wameanza 2021 hadi 2024 amegraduate hiyo mbona ni mapema
miaka 3 mbona ni mapema kabisa kwa Master of Science.

Pale Open University kugraduate Master of Science ukiwahi sana ni miaka 4 na kuendelea
na wengi huwa wanaachia njiani sio mchezo. Na mbaya zaidi Supervisors huonani nao mara kwa mara
ni kuwasiliana kwa email mara nyingi hata akikucheleweshea miezi 3 utamuona wapi?

Angalau labda wale wa MA, Business ndio ndio kidogo wanawahi wengine miaka 2, 3
na kuendelea.

PhD nayo wengi ni miaka 6 kwenda mbele ndio wana graduate

Kwenye uhakika ni bora vyuo vya nje angalau utachukua nusu ya miaka utakayo
soma hapa.
 
Bora kusoma nje kwa kweli
 
Hapa utajitahidi lakini unaangushwa na supervisor
 
Ni miaka 12 Toka nimemalia B.A hapo UDSM na sijawahi kuendelea Tena na mambo ya shule, jina UDSM sitaki hata kulisikia achilia mbali tu kusoma hapo.
Wana mambo ya kijinga sana, kuna rafiki yangu alisomaga SUA alikutana na Lecturer mmoja anamwambia sijawahi kuwa na darasa lililojaa hv, inamaana anafurahi watu wakirudi nyumbani pumbafu zake
 
SUA ni hatari Masters tu hutagraduate on time hata kama uko hard working utacheleweshwa mno, kupangiwa presentation tu ni kazi hadi wajiskie
Kusoma SUA kunahitaji vijana ila sisi tulio wazee na tulio makazini alafu tumejipata kiuchumi hatujisumbui huku.

Najiendea zangu Mkwawa au Tumaini au kile cha mwanaza cha kikatolic au kile cha Kiislamu cha Morogoro au vile vya Mbeya. Napata cheti changu cha masters tena nikiwa na ufaulu wa hali ya juu.

First degree ndio unatakiwa usome kwa shida. Huku kwingine hutakiwi kiwa na stress.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kumbe na kwenyewe mziki ule ule mungu atusaidie sisi watu wa lower middle class tunaotegemea elimu kubwa itutoe kimaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…