Wanamuziki wetu wengi wana Talanta, lakini wanakosa kitu muhimu sana kinaitwa strategies.. Kwasasa industry nzima imekariri kuwa ukitaka kiki basi uwadiss WCB.. Ni kweli utaongelewa ila ni poor strategy
First time nimesikia huu wimbo nilisikia huo mstari na nikajua tu nini kinatafutwa na nikasikitishwa sana na darasa..
Nitoe mfano; hakuna shabiki ambaye anashabikia msanii mmoja pekee.. Kwa mfano mimi shabiki mkubwa wa muziki wa WCB lakini pia ni shabiki wa Darasa toka enzi zile..
Sasa; muziki ni hisia na huwezi kupenda mziki wa mtu ambaye roho yako haina amani naye! Sasa inapotokea msanii akafanya upuuzi wa kuanzisha chokochoko na msanii mwingine unayemshabikia lazima hisia zako kama mshabiki zitachagua side.. Ndio kusema kwa mfano kwa ishu hii shabiki The Bold lazima ushabiki wake kwa darasa utapungua na kubakia kuwa shabiki wa WCB! Sasa darasa ajiulize anapoteza mashabiki wangapi kwa mtindo huu..
Nitoe mfano mwingine; juzi kati fiesta ilivyokuja Moro nikapata 'shavu' fulani hivi katika maandalizi yake and kwa wiki nzima ile nikajikuta nasikiliza sana clouds fm tofauti na kawaida yangu.. Nakumbuka kuna siku Darasa alikuwa anahojiwa na Diva, akaulizwa unazungumziaje mziki wa singeli na man fongo? Akajibu simjui man fongo... Diva na mbwembwe zake zile akahamaki "ooooohh my gooorsh kwahiyo hujawahi kusikia Hainaga ushemeji?? Unasikikizaga nini sasa kwenye redio??" Akajibu sisikilizi mziki wowote zaidi ya mziki wangu..!!!!
Doooohh nikasema ndugu yetu sifa zishamzidi, nayeye anajiona 'tembo' sasa..
Ila nikapotezea mpaka sasa ndio nakumbuka yale majibu yake yanareflect vipi personality yake ya sasa..
Ninachojaribu kusema ni nini??
Kuna kitabu mashuhuri sana cha Jemedari wa kivita Bwana Sun Tzu (ART OF WAR) na kuna kanuni moja anazungumzia kuwa "dont fight unnecessary wars".. Vita yoyote ina gharama! Kwahiyo kabla ujaanzisha/ujaingia kwenye vita yoyote kwanza fanya tathimini faida na hasara ya vita hiyo.. Je gharama utakayoitumia kupigana vita hiyo inaendana na manufaa utakayoyapata???
Sasa wabongofleva wao wanajua kuanzisha vita tu bila kutathimini gharama za vita hizo na faida gani watapata! Wao wamekariri tu "nitapata kiki"
Hiki ndicho kimemgharimu Dimpoz.. Alianzisha vita bila kufanya tathimini,
Yeye alipagawishwa tu "nitapata kiki" bila kujua gharama ya vita anayoianzisha..
Hakujua mashabiki wake wengi ndio hao hao mashabiki wa WCB na ulipofika muda wa kuchagua kuwekeza hisia zao za muziki kati ya dimpoz na WCB asilimia kubwa wakachagua kuwekeza hisia WCB.!!
Hapa ndipo ninaposema wasanii wetu wengi wana talanta lakini hawana Strategies.. Hata wakiweka strategies wanaweka poor strategies.. Ndio maana sijawahi kujutia kuwaunga mkono WCB, wana mikakati mwanana, muziki mwanana, washauri vichwa na hata wakiamua kuanzisha vita, wanaanzisha vita ambayo wana uhakika hawawezi kushindwa..
The Bold.