Mnashindwa kujua kwamba kujitunza kwa wanawake ili wabaki na hizo bikira zao kutamaanisha na wanaume nao itabidi wajitunze, kwa sababu wanawake wote wakisema wajitunze hadi ndoa basi wanaume watakosa wanawake wa kufanya nao kabla ya ndoa sasa ninyi kujitunza hamtaki, mkiambiwa subirini hadi ndoa mnajifanya eti hamtaki kuuziwa mbuzi kwenye gunia halafu leo hii mnataka bikira sasa hizo bikira zitoke wapi mbona ni kama ninyi wenyewe tu hamjui au hamko tayari kufuata hicho mnachokiadvocate
Wanaweza kujifunza kutokuwa playboys (kutochezea wanawake), ili utakapofika wakati wao wa kuoa wasianze kutukana wanawake, kwamba hawajitunzi na hawajiheshimu na siyo wife material
Aiseee mimi natamani sana muanze huo msimamo tena ikiwezekana mfanye na conference kabisa kama ile ya beijing iliyohusu feminism halafu mwisho wa siku mbivu na mbichi zitajulikana, fanyeni yote mnayoyajua ila kitu kimoja ambacho nawahakikishia ni kwamba wanawake kamwe hawatakaa warudi kuwa kama bibi zetu lije jua ije mvua mpaka siku wanaume mtakapokuwa tayari kubadilika, vinginevyo endeleeni kufarijiana na kuwatukana wanawake hadi mwisho wa dahari mkidhani eti mnawakomoa na kwamba ndio watabadilika ilihali alama za nyakati zinaonesha wazi ni wapi tunapoelekea