Ni uzuzu na kutojitambua kwa wasanii wa Tanzania hasa wakati huu ambapo social network ndio njia kuu ya mawasiliano, uwepo wa mitandao kama instagram, youtube, jf, fb na mingine inaweza kumsogeza msanii mbele na akauza kazi yake ya sanaa. Msanii kama Ruby anakipaji, watu wanajua na wanafurahia kipaji chake sidhani kama yuko makini angeshindwa kuuza bidhaa yake ya mziki kwa kutumia majukwaa yote niliotaja hapo.
Mfano, msanii akiamua kutengeneza album na akauza kwa sh.2000 tu, na akaamua kuwa ni project yake ya hata miezi 6 tu, na akaweka target ya kuwafikia watu laki moja(2000*100,000=200,000,000) atatengeneza 200M, hela ambayo hawezi pata kwa hiyo miezi 6, na hapo ni ameweza kuwafikia watu lakimoja tu.