Doreen Mrema afunguka mazito!

Doreen Mrema afunguka mazito!

Kwamba bibie alikufa akaoza kwa Mh. Ila wanawake hapana aisee 😂😂
Hapana huyu Alijiegesha akijua huyu Baba atakufa Mapema. Bora tu angejiita Nesi na si Mke. Mgonjwa wa Sukari, Dialysis, kutembea na kushika Vitu taabu. Kulikuwa na Ndoa gani hapo.? Gold Digger 🙄🙄
 
Ndo haya mnayokutana nayo.hivi unadhani ndugu zake watakubali kirahisi tu.ukae na ndugu yao chini ya mwaka uje kurithi Mali alizotafutq zaidi ya miaka 50+?
Sidhani kama anastahili mgao mkubwa ni ile tu kuappreciate kumlea ndugu yenu kipindi cha ugonjwa hata kama ni kwa muda mfupi.
Ana stahili kupata kidogo...ndio mtu ambaye mzee alimchagua awe karibu yake kipindi cha uzee wake why leo mumuache hana kitu kabisa? Not fair
 
Sidhani kama anastahili mgao mkubwa ni ile tu kuappreciate kumlea ndugu yenu kipindi cha ugonjwa hata kama ni kwa muda mfupi.
Ana stahili kupata kidogo...ndio mtu ambaye mzee alimchagua awe karibu yake kipindi cha uzee wake why leo mumuache hana kitu kabisa? Not fair
Na wewe utakubali upewe kidogo wakati unasema ni mume wako wa NDOA?yaani happy wakikubali tu wampe kidogo wameshaajiingiza kwenye mtego.huyo mama hatokubali.MALI IBILISI
 
Na wewe utakubali upewe kidogo wakati unasema ni mume wako wa NDOA?yaani happy wakikubali tu wampe kidogo wameshaajiingiza kwenye mtego.huyo mama hatokubali.MALI IBILISI
Mimi nakubali chochote. Gari wasingemnyang'anya..ni kitu kidogo sana
 
Hapana huyu Alijiegesha akijua huyu Baba atakufa Mapema. Bora tu angejiita Nesi na si Mke. Mgonjwa wa Sukari, Dialysis, kutembea na kushika Vitu taabu. Kulikuwa na Ndoa gani hapo.? Gold Digger 🙄🙄
Alijiweka kimkakati sana na kuna hatari akakosa vyote sababu ya pupa.
 
Siku chache baada ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Augustine lyatonga Mrema mke wake aliyefunga naye ndoa siku za karibuni amefunguka mbele ya wanahabari mambo mbalimbali ilkiwa pamoja na anayodai ni usia alioachiwa na marehemu mume wake pamoja na matumaini yake baada ya kifo cha mumewe.Ikumbukwe kwamba baada ya kifo cha mumewe maoni mengi yametolewa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu maisha yake baada ya kifo cha mumewe hasa ukizingatia kwamba ndoa Yao haikufanikiwa kudumu kwa muda mrefu (kutokana na kifo cha mumewe) ukizingatia swala la kurithi Mali.Wapo wanaodai hastahili kupata mgao kwa kua kwa muda waliofanikiwa kuishi pamoja si rahisi kwamba walichuma Mali pamoja kumstahilisha urithi,wapo wanaosema hawakufanikiwapata mtoto pamoja hivyo kumpunguzia vigezo vya urithi.Wapo wanaodai alijiegesha kiujanja ujanja ili apate Mali japo mwanamama huyu alishawahi kusikika akisema anamiradi yake(ya Maua ) maeneo ya Moshi hivyo kilichompeleka kwa mzee Ni upendo na si Mali .Ikumbukwe kwamba siku za karibuni imejitokeza minong'ono na hata kufikia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba huko ndani Hali si shwari.Ati wasema magari yanatolewa Hadi baadhi ya vifaa 🙊Amesema pamoja na changamoto alizopitia na anazopitia anaimani mtetezi wake yu hai na ama hakika mungu yu hai atampigania.
Nukuu
👇
"yapo yanayosemwa kwa kuyashuhudia kwa macho, ninaamini baba hajafunga macho, kama alivyoniahidi, kuwa hata akifa hatafumba macho, na ninaamini katika maneno yake."

"Sitakuwa na hofu wala sitakuwa na huzuni kwani naamini nimeachwa katika mikono salama. Bado nitaendelea kuishi kwa unyenyekevu, kama niliyekuwa mke wa Mrema, nitaendelea kuwaheshimu na kuwapenda wale ambao niliachwa kwao kama mke wa ndugu yao," amesema

"Nitaendelea kuwa mnyenyekevu kwa Serikali ya Tanzania na Watanzania wote na wote waliokuwa na mapenzi mema na familia ya Mrema" ameeleza

Amesema yapo mengi yanayozungumzwa kuhusu hatma yake akibainisha kuwa yapo baadhi yana ukweli na mengine ni upotoshaji.

"Yapo mengi yanayozungumzwa kwenye vyombo vya habari juu ya hatma ya maisha ya Doreen, yapo ambayo ni ya kweli na hayahitaji uchunguzi wa kiintelijensia na kimaabara."

"Lakini yapo ya upotoshaji kwa sababu ya dhamira mbalimbali nisisitize tu kwa kuwa changamoto zozote zilizotokea na zinazotokea naendelea kuzihifadhi lakini ninaamini mtetezi wangu yu hai” amesema na kusisitiza

“Niendelee kuwahakikishia Watanzania nitamuenzi mume wangu mpenzi na kuishi vile alivyoniasa na kunihusia, muondoe shaka juu yangu ila tumaini langu na imani yangu ni kwa Mungu aliye hai atampigania.
Nafikiri Dada huyu anapitia wakati mgumu kwa namna moja au nyingine anastahili kufarijiwa na watu wa karibu na watu wa unasihi pia wakimtembekea ni vizuri .Anaweza akawa anawaza kweli Hilo la Mali kwamba je nitapata Mali Kama mke halali au la.Je aachane na yote akaolewe na nanaumw mwingine(ukizingatia bado kijana)
Lakini Pia wajuvi wa mambo ukizingatia wapo wadau wa Sheria humu vp baada ya kufunga
ndoa Alikuwa mke halali wa ndoa Ila ukizingatia muda mfupi alioishi na mume wake stahiki zake Kama mke zinakuwa katika utaratibu upi Kama elimu kwa walio wengi kwani tumeshuhudia matatizo makubwa anapoondoka mtu na ukute ameacha mali . Just elimu kwa uma
Apewe UTEUZI
 
Hapa kwa kweli kuna shida bi dada sio mvumilivu kabisa ivi kirahisi tu wachaga wakupe urithi kwa miezi hiyo uliyokaa ndoani na anao wanae wakubwa tuu sidhani
 
Ndugu watafute vyao. Mke Halali atafute mwanasheria akapate haki yake mahakamani.
 
Yaani kule kwetu ukipeleka demu unaulizwa ametokea wapi ukisema arusha au moshi lazima upelekwe kwa sheh ukafanyiwe dua maana wanaona umeanza kuchanganyikiwa yaani hao waoane wenyewe kwa wenyewe tu wanapenda hela wako tayari hata kukutoa uhai.
 
Back
Top Bottom