Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hilo Hummer aseme kanunua used..2010 GM walibaki na Hummer 2200 na zote zilishaisha...lakini kwani Hummer Big deal? mbona yamezagaa jamani na used Hummers Na used Hummers Prices ranger zake ni $28000-$61 000 while brand new toka kiwandani ambayo hayapo tena sa ivi price range zake ni $129,399.00 for the open-top; the wagon $140,796.00, H1 Alpha was priced at $150,975.00...in that range so huyu aiswafanywe watoto wadogo
MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh Dotnata amefanya kufuru baada ya kutoa burungutu kununuamkoko wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka.
Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua mchuma huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani.
Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa, alisema Dotnata.Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima.
Leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, alimaliza Dotnata
Hivi kukodisha "Hummer" kwa masaa 24 ni TZS ngapi?
Nataka kutoka na nyumba ndogo wikiendi kwenda Loliondo kupata "kikombe"[/QUOTE]
Dada katangaza biashara, mteja huyu kapatikana
Hapa kuna la kujifunza. Sina tatizo na mtu kuwa na gari, gari ni muhimu sana kiasi kwamba hata kama huna nyumba unaweza ukanunua kwanza gari na nyumba (kulingana na mazingira unayoishi) ikafuata baadae. Ila nina tatizo na gari ya gharama (or any other "toys") kubwa kiasi hicho. Gari kama hiyo inamfaidisha mtu mmoja tu, wakati kwa pesa hiyo hiyo unaweza ukajenga shule ambayo itafanya watu wapate maarifa/elimu, waalimu wapate ajira, na mwekezaji apate faida. Gari kama Hummer haileti pesa, bali inakula pesa ktk mafuta na vipuri. May be I don't know how it feels like to be a star....
Mh! jamani msimshambulie sana ndiyo ubongo ulipofikia kutuletea habari kama hiii. Unakuta familia za watu wanakufa njaa wewe unafanya ubishoo ili watu wakujue. Ila kwa mdada sidhani kama ana ubavu huo na kama anao na amenunua mashauzi hayo. Glory be to God. Mungu amuondelee uvivu wa kufikiri maana Hammer is nothing compared to the life we have.
P
wabongo kweli maskini ..mtu kanunua hummer anakuwa celebrit lol!
Kwahiyo akinunua Hummer! Ndio Tunafanyaje?
Angenunua Escalede au Cadillac ingekuwa vipi? Nadhani ingekwa zaidi ya matangazo na habari wasanii wa kibongo wanapenda sifa za KIJINGA vitu vidogo tu Matangazo kila mtu ajue Gari kama hiyo sasa hivi Saudia ni Taxi
msanii matawi ya juu katika tasnia ya filamu bongo, husna mohamed posh dotnata amefanya kufuru baada ya kutoa burungutu kununuamkoko wa kifahari aina ya hummer, amani jipya limeinyaka.
Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika bandari ya dar es salaam, dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo milioni 270 kununua mchuma huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko detroit, nchini marekani.
kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa, alisema dotnata.
![]()
akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima.
leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, alimaliza dotnata
![]()