Doto Biteko, ishi na watu wa Pwani kwa akili; siyo mara zote wanapenda mtu aliyepo serious

Doto Biteko, ishi na watu wa Pwani kwa akili; siyo mara zote wanapenda mtu aliyepo serious

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kuna njia nyingi za kummaliza mwanasiasa kisiasa; moja ya njia hizi ni kuteua na kutumbua bila kutoa kupewa sababu ya kuteuliwa na bila sababu ya kutumbuliwa.

Kanda ya Ziwa ni eneo moja wapo ambalo kwa bahati mbaya halina wanasiasa wenye nguvu katika bunge la sasa. Mhe. Magufuli alihakikisha anapambana na brains zote akaacha chache ambazo moja wapo ni Dotto na wapili ni Bashungwa.

Wakati CCM ikiwa haina watu kwenye ukanda huu ,tayari upinzani una watu wengi wenye nguvu kisiasa na ambao wakiunganisha nguvu upo uwezekano mkubwa kanda hii ikiwa chini ya upinzani

Kwa kulitambua ilo watu wa pwani wanacheza karata zakuwaonyesha watu wa kanda ya ziwa kwamba bado wanakumbukwa. Endapo Dotto na Bashungwa watajisahau wakadharau au kuonyesha kuonyesha wanaweza kuliko watoto wa Mtama, Bumbuli, Msoga, Kizimkazi na Kisarawe upo uwezekano baada ya kutumika kwenye uchaguzi 2025 wakaachwa kupisha harakati za 2030

Natambua Biteko amewekwa kwenye mtego wa kikatiba kama Mrema, natambua Mrema alifurahia uwaziri mkuu mdogo bila kujua wanashughulika naye kisiasa.

Mdogo wangu Dotto usishtuke na usiuzunike moyoni mwako piga kazi kwa kumtegemea Mungu. Ila napenda kukuhasa kwamba" Tundu Lissu amesema umeshiriki kuiba madini na kuweka ndugu zako kwenye madini huko kanda ya ziwa, natumai Tundu Lissu ajaropoka ameongea akiwa na facts na may be anajua mengi kuhusu uhusiano wa wizara ya madini na utajiri wako.

Anza kuona hizi kama alert mbaya kwako, anza kujiuliza kwanini hizi taarifa zianze sasa? Then rekebisha kama unaamini kwa namna moja au nyingine kuna sehemu siasa inaanza kukufanya uwe fisadi au kuna watu wanakutumia kufanya ufisadi basi wakwepe.

Umekuwa mbunge bila fedha, kwanini uamini kwamba ili uishi lazima ukwapue fedha za wanyonge? Achana na fikra za Ali Bongo, bora ukose uwaziri mkuu kwa umaskini kuliko uwaziri mkuu wakunyaswa na watu wa pwani.

Nikutakae tafakari njema
 
Hilo la kuwanufaisha watu wenye asili ya Rwanda kwenye madini, halina ubishi. Na Bila shaka huu uteuzi mpya hatakuwa umeufurahia maana unamwondoa sehemu ambayo amejenga mizizi mirefu ya kujinufaisha. Akina Evaree watakuwa wamehuzunika sana.
 
Mnajifanya mnamjua kuliko aliyemuona akamteua? Mlikua wapi msimwambie hayo yote alipokua waziri wa kawaida muwachage tabia za kinafiki watanzania.
 
Back
Top Bottom