BuDDaH MBiSHi
JF-Expert Member
- Jan 14, 2021
- 468
- 495
Nje ya mada.... Hivi zile stori za kwamba umeme utapungua bei baada ya bwawa kuanza kazi zilikua za vijiwe vya kahawa tu eee?....Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesema kuwa mashine moja iliyokuwa imewashwa kwenye bwawa la Mwl Nyerere imezimwa baada ya maji kujaa sana kwenye bwawa kinyume na matarajio ya awali kwamba bwawa hilo litatumia miaka 2 kujaa lakini sasa limetumia mwezi mmoja tu kujaa na sasa maji yanalazimika kupunguzwa.
Hapo mwanzo Chadema walitoa tahadhari kwamba bwawa halitajaa kutokana na miti millioni 3 kukatwa na Magufuli hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira na ukame nchini.