Pre GE2025 Dotto Biteko: Watanzania tufanye kazi, siasa haitaleta mkate mezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yeye mwenyewe mgawanyaji. Ukishakuwa ccm lazima uwe na tabia hizo. Uwachukie wanaopinga hoja na misimamo yako na usipeleke maendeleo kwao. Si kugawanya huko? Na mbona yeye anafanya siasa huko anafaidika nn mpaka yeye asiache Ili wengine wafanye na kwa nn hataki watu wafanye siasa. Awaambie watu wafanye siasa na za kistàraabu na kazi siyo kuwaambia watu wasifanye siasa wafanye kazi. Mm sijamuelewa.
 
Dotto, amesoma ualimu WA cheti, akaripoti kazini na kurudi chuo kujiendekeza kielimu kwa dip, cert tena, Bach na masters na akawa afisa elimu taalumu WA wilaya ya nyang'hwale huko geita.
Aliingia kwenye siasa akianza na za cwt na baadae CCM akachaguliwa kuwa mwenyekiti WA wazazi mkoa

Dotto amefundisha wakati WA BTP aka field pekee.

Dotto ni mpwa WA Kabuzi, aliyewahi kuwa mbunge WA busanda.

Bila connection hupati cheo bongo .
 
Huyu jamaa namuheshimu sana kwa maana hiyo sita-comment nilichotaka ni-comment
 
Wanasiasa wa Tanzania wengi ni wajinga sana.

Mtu mwanasiasa anakwambiaje tuachane na siasa?

Yeye akiachana na siasa hata hicho cheo chake atakuwa nacho?
 
Bila siasa yeye angekuwa hapo alipo? Hopeless kabisa!
 
Kama siasa haileti mkate kwanini wamekuwa ving'ang'anizi wa madaraka?
 
Hayo alistahili kumwambia Samia, na taasisi zake zinazoteka na kuua watu.

Tangu lini wauaji wakawa na umoja na wanaouawa?

Tukitaka wananchi wawe na upendo na umoja miongoni mwao, CCM ni lazima iache siasa za kishetani za kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kuwateka, kuwatesa na kuwaua wananchi wanaomkosoa Rais na Serikali yake.

Kwa sasa CCM na Serikali ndiye shetani mbaya kuliko wote kwa umoja wetu.
 
Kwahiyo yeye anatangaza lini kuacha siasa? Au anatuzuga tu.
CCM imejaa watu matapeli na waliojaa hadaa.

Hivi Biteko bila siasa, ana nini cha pekee?

Hivi Samia bila siasa, ana nini cha maana?

Imefika mahali sasa wananchi wanatakiwa kuwazomea palepale hawa wanasiasa matapeli, wanapotoa hizo kauli zao za kipuuzi.
 
Anashau kwamba siasa hiyohiyo Inaweza kuchangia ugumu wa kuupata huo mkate!!
 
Kuwa CCM ni janga kubwa sana.. Yani yeye ni mwanasiasaa yuko jukwaani anahubiri siasa halafu anawakataza wengine kufanya siasa
Nafikiri alimanisha kwamba wengine tufanye kazi zingine . Sio wote tukimbilie siasa
 
Amesomea ualimu chuo cha ualimu Kigurunyembe, Diploma.

Akaenda chuo cha SAUT MWANZA, UALIMU DEGREE.

Hiyo PhD ya Udom!

Andiko lake alichoaandika sijui,aliandika nani sijui!

Hila upstairs ni low thinker!
tanzania bwana vilaza ndio wana madaraka.
namba 1 kilaza
waziri mkuu kilaza
naibu waziri kilaza
duuh vilaza wako mstari wa mbele. wananzengo mtafika kweli????
 
Anataka tufanyd kazi kwa bidii ili mapato yawe makubwa waongezewe posho nakulipa na kuzifuja nyingine kwa kuzuia Maandamano ya CDM.
 
Nchi hii hapana aisee, kwaiyo siasa ni kwao kujifurahisha au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…