Azim Sokoine
JF-Expert Member
- Aug 20, 2014
- 1,443
- 2,643
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂😂😂😂Hawatashinda, Taifa Stars ndio itashinda. Hivyo vyenda uchi si ajabu vikaenda uchi uwanjani badala ya Samata na Msuva ikawa mapaja na shanga
Hata ikishinda Tanzania sababu haitakuwa hamasa ya wanasiasa.Hii game Ngoja niweke akiba ya maneno kwanza!
Maana unaweza ukaongea sana halafu hao wanasiasa wakaibuka washindi
Naamini stars ilikuwa na uwezo wa kufuzu kwenye hili kundi bila kutegemea matokeo ya mechi za mwisho sema mfumo wa Amunike umetugharimu jamaa ana wachezaji wazuri ila ndio hivyo penye miti wajenzi hawaonekaninimekuelewa mleta mada! ila sidhani kama tutafuzu maana tulishindwa kutumia vizuri ile mechi ya chamanzi complex dhidi ya LESOTHO. Uganda wana clean sheet hawajafungwa goli hata moja kwenye haya mashindano
AMUNIKE sio kocha mzuri naona kama mbabaishaji tu anaweza kukupangia kikosi tusichotegemea hasa kwenye midfield, techical benchi linaongozwa na Ammy ninje tayari lina ukakasi.
ikitokea tumefungwa itakuwa bahati mbaya... maana tulikosea hapo mwanzoni tujipange next game.
kila la heri Taifa Stars nitawashangilia mwanzo mwisho
jinga jinga jingalao sio kila sehem utetee hapa sio ccm!! weka ukada pemben angalia hojaHamasa huletwa na wasanii sio wachezaji kila mtu ana umuhimu wake
Shilole Jana Yupo Mbele ya Media Anauliza AFCON ni Nini? Hadi anawekwa Kwenye Kamati, anaitwa Kwenye Kikao, a nafika Mbele ya Media
Ndo Anauliza Maana ya AFCON [emoji23][emoji23]. Tanzania Tuna Shida Mahali
Sent using Jamii Forums mobile app
Kisa jingine kubwa ni kuiweka hiyo kamati chini mhuni na muuaji bashite ambaye hakubaliki kwa watu waliostarabika hapa dar. Lazima tupige bao tujifunze kutenganisha mpira na siasaKule Ulaya na mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka,inapotokea kunahitajika hamasa kubwa ya kujenga morali kwa wachezaji na mashabiki basi wale wachezaji Nguli wastaafu hutumika sana kuhamasisha morali ya ushindi.
Hii hutumiwa sana na Vilabu vikubwa duniani ama timu za taifa ambapo wakongwe(Legendaries) huwekwa jukwaani sehemu maalum kabisa ikiaminika kuwa wale waliopo uwanjani wakitazama jukwaani na kuwaona wakongwe morali inapanda na hata kwenye kujenga hamasa wachezaji waliocheza kwa mafanikio hutumika sana.
Sasa nakaribu kutazama mbinu inayotumiwa na kamati maalum ya kuhamasisha ushindi wa timu ya Taifa hapo keshokutwa.
Kwenye mkutano wao na waandishi wa
habari,mbali na kuwajumuisha waandishi wa michezo,lakini naona inawatumia zaidi waigizaji maarufu nchini akina Wema,Shilole,Steve Nyerere n.k na kuwaweka kando wanasoka waliocheza kwa mafanikio miaka ya nyuma.
Kwa nini kamati inaacha kuwatumia wanasoka waliowika miaka ya nyuma inakimbilia kuwatumia waigizaji?kwa nini tusiandae vipande vya vidio vya wanasoka waliowika huko nyuma wakiwahamasisha vijana wetu na wanasoka hawa siku ya jumapili wakatengewa eneo maalum pale Jukwaani?
Kwa nini tumewatenga wanasoka walio hai ambao waliipekea Tanzania katika fainali za mataifa huru Afrika mwaka 1980 kama
sehemu ya hamasa kwa wachezaji na Watanzania?
Kwa nini tusiwarekodi na hata kwenda nao kwenye "Press Conference" wachezaji wakongwe waliocheza fainali hizi na wakasema neno la hamasa kwa watanzania na hata tukawaambia watanzania wajae uwanjani waungane na wakongwe pekee waliofuzu fainali hizi kutoka Tanzania na badala yake tunawatumia akina Wema pekee?
Nafahamu akina Wema wanamashabiki nyuma,lakini katika hili la Jumapili hebu tunatumie zaidi wachezaji wetu waliocheza kwa mafanikio wakati wao.
Mbali na akina Tenga waliokuwemo kwenye kikosi cha Stars kilichofuzu fainali hizi pekee,kwa nini pia tusiwatumie wanasoka waliocheza kwa mafanikio kwenye Vilabu na hata kufika ngazi ya juu?
Waliokuwemo kwenye Kikosi cha Simba kilichocheza Fainali za kombe la Shirikilo la Soka Afrika mwaka 1991 na walicheza timu ya taifa wengi wao wapo,kwa nini tusiwatumie hawa kama sehemu ya hamasa?
Walioifikisha Yanga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 bado wapo kwa nini tusiwatumie kama sehemu ya hamasa na badala yake tunawatumia zaidi waigizaji na waimba muziki?
Tunapowatumia waigizaji na waimba Muziki kuhamaisha ushindi wa Stars,tusiwaache wachezaji nguli wa zamani akina Leodigar Tenga,Sunday Manara,Abdalah Kibaden,Juma Pondamali,Adolf Richard,Zamoyoni Mogella,Mohamed Mwameja,Ken Mkapa ,Peter Tino
mfumgaji wa bao la
Star lililoipeleka Tanzania kwenye fainali za
mataifa huru na wengine wengi katika kuhamasisha wachezaji,kuhamasisha mashabiki ili jumapili tupate ushindi.
#nizamuyetu
Kule sio sawa na kwenda kuomba kuraHamasa huletwa na wasanii sio wachezaji kila mtu ana umuhimu wake
Ukiacha makandokando ya kuwatumia akina wema,Amunike amechangia kwa kiwango kikubwa kuinyima nafasi Starsnimekuelewa mleta mada! ila sidhani kama tutafuzu maana tulishindwa kutumia vizuri ile mechi ya chamanzi complex dhidi ya LESOTHO. Uganda wana clean sheet hawajafungwa goli hata moja kwenye haya mashindano
AMUNIKE sio kocha mzuri naona kama mbabaishaji tu anaweza kukupangia kikosi tusichotegemea hasa kwenye midfield, techical benchi linaongozwa na Ammy ninje tayari lina ukakasi.
ikitokea tumefungwa itakuwa bahati mbaya... maana tulikosea hapo mwanzoni tujipange next game.
kila la heri Taifa Stars nitawashangilia mwanzo mwisho
Mwandishi ana wivu tena wivu wa jinsia KE. Mbona wachezaji wazamani wanaonekana wakihamasisha?Tusianze kubaguana kwa matukio.Wanasiasa na wasanii ndo wenye ushawishi mkubwa hapa nchini