Dotto Bulendu: Soka limekabidhiwa wanasiasa na wasanii ndio tutarajie ushindi dhidi ya Uganda? Wanasoka wetu wastaafu hawapo? Hawathaminiwi?

Dotto Bulendu: Soka limekabidhiwa wanasiasa na wasanii ndio tutarajie ushindi dhidi ya Uganda? Wanasoka wetu wastaafu hawapo? Hawathaminiwi?

Yes Siasa imeiingia kwenye mpira ila ki ukwel kabisa Tenga, Mahadhi, Mohemed Husein, Lunyamala wanaweza kwel kuhamashisha watu wakajaa uwanjan kwa hulka zetu sie tulivyo?
 
Kule Ulaya na mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka,inapotokea kunahitajika hamasa kubwa ya kujenga morali kwa wachezaji na mashabiki basi wale wachezaji Nguli wastaafu hutumika sana kuhamasisha morali ya ushindi.

Hii hutumiwa sana na Vilabu vikubwa duniani ama timu za taifa ambapo wakongwe(Legendaries) huwekwa jukwaani sehemu maalum kabisa ikiaminika kuwa wale waliopo uwanjani wakitazama jukwaani na kuwaona wakongwe morali inapanda na hata kwenye kujenga hamasa wachezaji waliocheza kwa mafanikio hutumika sana.

Sasa nakaribu kutazama mbinu inayotumiwa na kamati maalum ya kuhamasisha ushindi wa timu ya Taifa hapo keshokutwa.

Kwenye mkutano wao na waandishi wa
habari,mbali na kuwajumuisha waandishi wa michezo,lakini naona inawatumia zaidi waigizaji maarufu nchini akina Wema,Shilole,Steve Nyerere n.k na kuwaweka kando wanasoka waliocheza kwa mafanikio miaka ya nyuma.

Kwa nini kamati inaacha kuwatumia wanasoka waliowika miaka ya nyuma inakimbilia kuwatumia waigizaji?kwa nini tusiandae vipande vya vidio vya wanasoka waliowika huko nyuma wakiwahamasisha vijana wetu na wanasoka hawa siku ya jumapili wakatengewa eneo maalum pale Jukwaani?

Kwa nini tumewatenga wanasoka walio hai ambao waliipekea Tanzania katika fainali za mataifa huru Afrika mwaka 1980 kama
sehemu ya hamasa kwa wachezaji na Watanzania?

Kwa nini tusiwarekodi na hata kwenda nao kwenye "Press Conference" wachezaji wakongwe waliocheza fainali hizi na wakasema neno la hamasa kwa watanzania na hata tukawaambia watanzania wajae uwanjani waungane na wakongwe pekee waliofuzu fainali hizi kutoka Tanzania na badala yake tunawatumia akina Wema pekee?

Nafahamu akina Wema wanamashabiki nyuma,lakini katika hili la Jumapili hebu tunatumie zaidi wachezaji wetu waliocheza kwa mafanikio wakati wao.

Mbali na akina Tenga waliokuwemo kwenye kikosi cha Stars kilichofuzu fainali hizi pekee,kwa nini pia tusiwatumie wanasoka waliocheza kwa mafanikio kwenye Vilabu na hata kufika ngazi ya juu?

Waliokuwemo kwenye Kikosi cha Simba kilichocheza Fainali za kombe la Shirikilo la Soka Afrika mwaka 1991 na walicheza timu ya taifa wengi wao wapo,kwa nini tusiwatumie hawa kama sehemu ya hamasa?

Walioifikisha Yanga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 bado wapo kwa nini tusiwatumie kama sehemu ya hamasa na badala yake tunawatumia zaidi waigizaji na waimba muziki?

Tunapowatumia waigizaji na waimba Muziki kuhamaisha ushindi wa Stars,tusiwaache wachezaji nguli wa zamani akina Leodigar Tenga,Sunday Manara,Abdalah Kibaden,Juma Pondamali,Adolf Richard,Zamoyoni Mogella,Mohamed Mwameja,Ken Mkapa ,Peter Tino
mfumgaji wa bao la
Star lililoipeleka Tanzania kwenye fainali za
mataifa huru na wengine wengi katika kuhamasisha wachezaji,kuhamasisha mashabiki ili jumapili tupate ushindi.
#nizamuyetu
Mkuu Bulendu sijui kwanini hadi sasa bado upo hapo star tv maana kwa uweledi ulio nao naona kama unachelewa huko

In God we trust
 
Dotto Bulendu, Utaitwa mchochezi na usiye mzalendo kwa nchi yako.
Afadhali aseme ukweli kuliko kuendelea kuwa kondoo wakati tunaumia kwa maamuzi ya watu wachache

In God we trust
 
Akili zetu ni za kuiba vitu kama kura etc basi, maendeleo ni shida kwa akili zetu. Umeona wapi kitu aina hiyo? wanasiasa kwenye soka? badala ya kuwa na ubunifu wanatumia kejeli kwa UGANDA, acha tuone
Karia kaliharibu soka letu na kapoteza upenzi wa watanzania walio wengi

In God we trust
 
Nilipoona wenyekiti wa hiyo kamati nikaona isiwe shida... Yani tuna tatizo kubwa kama taifa!
Hata ivyo kila la kheri stars, TFF inapoongozwa na makada tusahau kabisa mpira wetu kusonga mbele
Watashangilia wao hilo lipo wazi kabisa

In God we trust
 
Watu wasiokuwa na maadili katika jamii ndio wanakadhiwa jukumu la kuhamasisha. Wafoji vyeti, wa picha za ngono, waongo, wala rambi rambi ndio wanapewa uhamasishaji. Watu wenye akili wameshawadharau pamoja na mbwe mbwe zao zote!
Ni jambo la aibu sana

In God we trust
 
M
Hii game Ngoja niweke akiba ya maneno kwanza!
Maana unaweza ukaongea sana halafu hao wanasiasa wakaibuka ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mimi ninchokiona katika maono yangu ile game tunafungwa mapeeeeema wagannda watatulaza na viatu..................................Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Daudi Albert Bashite yeye anamjua Amber Rutty tu na ndiye kamtumia kuhamasisha ushindi wa Taifa Stars. Kwa kweli mimi nitashabikia The Cranes kwa sababu Bashite kashainajisi Stars na hao akina Amber Rutty.
 
Yes Siasa imeiingia kwenye mpira ila ki ukwel kabisa Tenga, Mahadhi, Mohemed Husein, Lunyamala wanaweza kwel kuhamashisha watu wakajaa uwanjan kwa hulka zetu sie tulivyo?
Sasa Wewe unamlinganisha le mutuz na Tenga kweli?!!

Yaani katika soka umsimamishe Steve Nyerere na Leodgar Tenga halafu watu wamsikilize huyo Melenge wa mama Wema.........acha maskhala mkuu Bonny!
 
Dotto kuna mambo mengine wakati mwingine yanatia kinyaa hata kuyasikia,hawa waingizaji wanaojiachia na mapicha ya utupu ndiyo wanapewa kipaumbele cha kuhamasisha watanzania kuelekea mechi yetu na Uganda?,kweli?.

Jana huyo Shisha sijui shishi ilibidi nicheke mwenyewe yaani ni kama kumchukua mtu ukamfunika usoni na kumpeleka mahali ukamwachia asijue yuko wapi,ndo nilikioni jana mtu hajui hata alichoitiwa,anaishia kuuliza ni nini tena?,wenzake wanamwambia AFCON oooooo,yes ni afcon kweli.

Kweli yajayo yafurahisha,#Tukutane Taifa Jumapili
 
Sasa Wewe unamlinganisha le mutuz na Tenga kweli?!!

Yaani katika soka umsimamishe Steve Nyerere na Leodgar Tenga halafu watu wamsikilize huyo Melenge wa mama Wema.........acha maskhala mkuu Bonny!
Hujanielewa Mkuu sjawalinganisha kutokana na thaman au mchango wao ila nmelinganisha kutoana na umaarufu wao leo hii rud mtaan kwako sema nan anamfahamu Steve Nyerere na nan anamfahamu Tenga utaona tofauti yake.
Point yangu ni kwamba asilimia kubwa ya watanzania kwa sasa hvi tutafata atakachosema Steve nyerere zaid kuliko atakachosema Tenga.
 
Hamasa huletwa na wasanii sio wachezaji kila mtu ana umuhimu wake
Dotto kaweka facts za kinacho fanyikaga Ulaya kwa kutumia wachezaji wastaafu na walio fanya vizuri, sasa na wewe weka mifano ya hao wana muziki sehemu zingine za dunia.
 
Hii game Ngoja niweke akiba ya maneno kwanza!
Maana unaweza ukaongea sana halafu hao wanasiasa wakaibuka washindi
Hata kama wakiibuka washindi lakini itakuwa SIYO kwa sababu ya hawa wababaishaji waliojiweka viti vya mbele. Soka la Tanzania litaendelea kuwa chini mpaka siku tutakapokubali kushangilia ushindi wa kubahatisha hapa na pale. Hata saa mbovu inasema kweli wakati mwingine ati... lakini siyo kama ni nzima.
 
Back
Top Bottom