Double standards: TAKUKURU yashindwa kuwachukulia hatua watoa rushwa wa CCM wasema chama ndio kiwachukulie hatua

Double standards: TAKUKURU yashindwa kuwachukulia hatua watoa rushwa wa CCM wasema chama ndio kiwachukulie hatua

Hapa ndipo unaona uteuzi wa hawa wakuu wa hizi idara nyeti unatakiwa ufanyiwe veting ya kutosha na kuangalia weledi.
Huu ndio ujinga mkubwa kuwahi kutokea kufanywa na TAKUKURU
 
Hatari sana, nimeona pia gazeti moja limemchafua sana Tundu Lisu Leo, Nikajiuliza hivi ndo ingekuwa magufuli kaandikwa hivi ingekuwaje.....Ila hivi vyombo vya serikali vijue kabisa kuwa Urais ni kupokezana , Leo huyo mnaempendelea kesho atakuwa mpinzani, na huyu mnarmkandamiza kesho ndo atakuwa rais, Sijui mtaficha wapi sura zenu. Kumbukeni Malawi, Kenya, Zimbabwe, Congo na nchi nyingine nyingi kuwa vyama tawala sasa hivi ndio vyama vya upinzani.
wamuulize Yusuf Manji!
 
Mimi nilijua wanawapeleka mahakamani!!Sikuwahi kujua kuwa TAKUKURU wanakifanyia kazi chama!Yaani watoa rushwa wanashitakiwa kwenye chama?

Ajabu ya mwaka. Kisha boss wa Takukuru anatembea na kombati la jeshi kila siku. Sanasana kwa kushindwa kudhibiti rushwa, analifanya hata jeshi kupata taswira ya kuwa ni watetezi wa wala rushwa.
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
 
Unashangaa ya Tundu Lissu kuitwa mropokaji, gazeti Hilo Hilo Jana liliandika kuwa Maalim Seif Ni shoga,
😀😀😀😀😀😀😀mbavu zangu mimi loooooooh....ni magazeti gani hayo tena
 
Ni kweli waliandika hivyo mkuu@Johnny Sack ? Ni gazeti gani? Tunaomba picha tuweke kumbukumbu, kesho tuwe na ushahidi.
Hili
IMG_20200813_120258.jpg
IMG_20200813_120253.jpg
 
TAKUKURU ni Taasisi inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria na inataratibu zake katika utendaji, hata maamuzi yaliyotelewa dhidi ya watia nia wa CCM yametokana na taratibu za utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.

What?
 
Kwani rushwa si ni kosa lajinai hiyo kamati ya chama ndo inayohusika na makosa ya jinai nchi imeharibika na rushwa za hao watu halafu badala ya kufikishwa mahakamani wanachiwa kamati ya maadili ya chama haya ni maajabu
 
Hivi chukulia mfano ndani kwenu uko wew baba na mama yako halaf wazaz wako wakakosea unategemea utawafokea,, si utafukuzwa
 
Back
Top Bottom