Katibu Mkuu NLD na aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka 2025, Doyo Hassan Doyo, akizungumza kwenye mahojiano na Wasafi Media leo Julai 2, 2026
"Ni kweli siasa ya nchi hii inahitaji fedha. Ukizungumzia mikutano ya hadhara, mkutano mmoja mdogo ambao unaweza ukauandaa sehemu ya wilaya tu, zaidi ya milioni moja mdogo kabisa. Acha hii ya mikoani ambayo ina majukwaa makubwa, ina mamiziki, milioni tatu, nne ndio unaweza ukafanya mkutano.
Sasa kwa chama ambacho hakina ruzuku, huwezi ukakiona. Na ninyi mnasikia kuna vyama vina wafadhili mpaka wa kigeni. Kwa hiyo wao wana hizo njia za kufanya mipango mpaka wanapata fedha nyingi nje kwa ajili ya masuala kama hayo ya mikutano na kujitokeza mara kwa mara kwao sio tatizo kwa sababu shughuli zile zinahitaji fedha nyingi sana.
Kwa hiyo chama chetu baada ya usajili hakijawahi kupata uwakilishi lwa wabunge. Lakini madiwani kiliwahi kupata, mfano mkoa wa Kagera tulipata madiwani watatu, Masasi tulipata diwani mmoja ambaye ndio alizaliwa mheshimiwa mwenyekiti wetu wa kwanza ndugu Makaidi. Kwa hiyo kinapata nafasi kutokana na udogo wake, yaani kila mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake. Kwa hiyo tumeshiriki matukio ya kisiasa na tumefanikiwa."