DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Hilo ndo tulilotarajia, hao walitakiwa wapewe tender ya kufanya operations kama ilivyo TICTS na siyo kumilikishwa bandari, hilo haliwezekani.
Hamna mtu wa kuwapa Bandari yote. Wanacover sehemu TICTS walipotoka ila wao kwa ufanisi zaidi.
 
Hao waKenya gani wamepinga ebu wataje tuwanange.
Maana kila mtu anawalaumu bila kuwataja.
Wote wanaosema Mkataba umesainiwa ni wakenya. Wote wanaosema DPWorld wamepewa bandari zote ni Wakenya, wanaksema DPWorld wamepewa bandari ya dar yote ni wakenya
 
Kwani maneno Yako ni mkataba 😃😃😃😃 dp world anapewa bandari kuiendesha , unajua Maana ya kuendesha au ujui , km ujui Rudi Shule alafu ukija uje na ugolo wako , kwann tupakue na kupakia kotena laki 7 ni Kwa sababu hatuna vifaa vya kisasa , km tumekopa na kujenga bandari Kwa tr 1.4tunashindwa kununua mitambo ya kisasa tukashusha makasha Kwa Siku Moja Toka Kweny meli , kipi kinashindikana mifumo isisomane wakati tunao wataalam wa tehama nchi nzima , walete ttcl wakae pale km Kuna mfumo hautasomana , huo ni utetezi hewa viongozi mnashindwa kutumbua hao watendaji wabovu , Kwa mkataba wa msingi ndo unaoonyesha mikataba inayokuja itakuwaje , hatutaki badari yetu wapewe hao Kwa mkataba wa hovyo kabisa ,
 
Wenye uwezo ni kina nani

Hao

Ova
Sio rais, bali Nchi tumeamua kutafuta muwekezaji. Sababu wenyewe tumeshindwa endesha bandari hadi Kagame anasema akipewa bandari anaweza lisha africa mashariki na kulipa mishahara
 
Soma hapo kwenye kifungu cha pili uone kama wameandika posa au mkatabaView attachment 2658248
Ooh! Hapo ndo panakuchanganya. Huo ni mkataba wa Ushirikiano. Sio mkataba wa uwekezaji. Hata China tunamkataba nao wa Ushirikiano. Ajabu ni nini hapo? Mumejazwa upepo kumbe? Mbona huu mkataba hujalalamika? Mikataba ya Ushirikiano ipo mingi Tanzania inaingia. Itakua neno bandari ndo limekushitua. Relax

Sasa hapa mbona hukusema wameuza na kukabidhi utamaduni na sanaa yetu kwa wachina? Je, huu makataba una miaka mingapi?

Acha kusikiliza watu wanaokupotosha. Nisikilize mimi
 
Wacha inyeshe uone inapovuja.

Kadiri wanvyozidi kujieleza ndivyo wanazidi kijichanganya.

1. Mkataba umetaja Bandari ya Dar es Salaam wao wanasema siyo yote ni gati namba ngapi hadi ngapi. Mbona mkataba haujaspecify sasa. Tu naaminije unacho ongea tu bila maandishi. Profesa mbona ananiangusha sana na uprofesa wake aise.

2. Mkataba inasema ni Bandari zote za Tanzania Bara maziwa, mito na baharini. Yeye anasema Bandari ya Tanga, Bagamoyo na Mtwara hazipo kwenye makubaliano haya. Tunajuaje kama hazipo wakati mkataba haijaweka exception. Mbona mheshimiwa waziri anafanya haya mambo kama mtoto mdogo namna hii aise.

3. Mkataba mama unasema wazi kabisa hakuna kujitoa kwa namna yeyote ile, hata kama tutaingia vita na Dubai bado mkataba utaendelea kuexist. Waziri anasema tutajitoa. Tutakitoaje kwanini wasikiri tu mapungufu basi yarekebishwe.


Hawa wahuni ni kuendelea kuwakomalia kusema umwachie Mungu ni kuendelea kukubali kuonewa na kuibiwa. Ni either wakubali kubadili vifungu au waachane na huo Mkataba. Tuendelee kushika kamba no way back.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
Narudia tena na nakuomba uache kushupaza shingo kana kwamba unajua kila kitu. Hakuna popote ambapo kuna mkataba wa Bandari ambao umesainiwa au haujasainiwa. Kilichopo ni Mkataba wa Ushirikiano.

Tatizo Nchi hii kila mtu anajifanya anajua Sheria. Hata Maazimio ya bunge mnasema bunge limepitisha mkataba. Shule mlienda kusoma ujinga?
 
Mkuu unajua mnaongelea haya mambo embu muwe basi mnajua hata mnaongelea nini? namna mnavyotetea mnaonekana kabisa hamjui nini mnaelewa mfano wa makosa nayoona wengi mnayafanya ni kuita geti badala ya gati ........... hapo tuu inaonekana kabisa wazungumzaji wengi hawajui bandari hata kidogo hata tofauti ya hayo maneno mawili hawajui ndipo unapata shaka sasa kwenye maelezo yafutayo ya utetezi je kweli tuna haja ya kuamini kuamini sasa haya maelezo.

mimi nimewasaidia tuu wanajamii maana kuna watu wana wahadaa wasio kuwa na ufahamu walau kidogo wa haya mambo so please nenda mjue kwanza GATI NI NINI? NDIO UJUE NA UTETEZI .

NAWASILISHA WAKUU
 
Kwani mnalipwa sh ngap na mimi nijisajili huko??
 
Kuhusu kupakua mako

Kuhusu kupakua makontena 16 kama ndiyo yaliyopo mkuu unategemea mengine yatoke wapi? Labda kama unamaanisha kuna makonte yanabaki kwenye meli bila kushushwa sawa.
 
Karamagi, Kanji bai na Mombasa kwish nehi
 
Unatafuta utukanwe sio
 
Ndo maana nimependekeza Mkataba uwekwe kwa kiswahili ili watu kama wewe wasiendelee kupotoshwa
Hao vichaa wenzako watakuelewa huo mkataba uwe kwa kiswahili.maana hata wao pamoja na ww hamuelewi chochote kwenye mkataba huo ndio maana kwa sababu na ww inakutatiza kuelewa ndio maana umeshauri hivyo na hutaki kuwaelewa wanaokusaidia unataka na ww ujifiche kwenye kundi la wanaojua sheria na kiingereza cha kisheria shauri yako.
 
Hivi Bandari yetu inachangia kiasi gani kwa mwaka? Maana hiyo asilimia 35% hatujui kiasi gani?

Alafu DP World ikiendesha bandari itachangia pesa kiasi gani kwa mwaka? Tupe elimu sasa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…