DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Vipi kuhusu Zenji? Kuleni nchi waarabu, zama zenu hizi. Tumeshaanza kuona joto ya jiwe mitaani. Mandinga tunayaona na kanzu zenu.
Alipokuwepo TICTS mbona hamjasema vipi Zanzibar mbona TICTS haipo?

Leo anakuja DPW baada ya TICTS kuondoka ndipo umekumbuka Zanzibar? Au unaota? Ushalishwa matango pori huko nawe unajifanya kuujua Mkataba. Akili yako imejaa ubaguzi
 
Kuna kitu hujaelewa bado. Makubaliano ya mashirikiano hayana muda

Pili Hakuna mkataba wa Bandari haddi sasa.

Tatu DPW anapewa sehemu ya bandari ya Dar aiendeshe.

Nne, hapewi kitu kingine nje ya sehemu ya bandari ya Dar.

Sema wewe umesoma upotoshaji na ndio umeshikia bango kama watu wengine. Ila taratibu tutaelewana
Screenshot_2023-06-17-23-39-33-78_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
 
Haya mambo ya Kisheria ni magumu sana. Hayasomwi kama Novel. Hapo juu wamekuambia ni Makubaliano ya Nchi na Nchi katika kuwekeza kwenye Bandari na usafirishaji Baharini. Nioneshe kitu Contract. Au agreement ndo umeita Contract? Sikilizeni wanasheria wetu wanachosema. Mtapotoshwa sana na Wakenya.
Screenshot_20230618-000531.png
 
Kwa upande wangu Dp world hana baya na niwaombe viongozi wasonge mbele kwani wananchi wengi wamejazwa ujinga na wapigaji wanaonufaika pale bandarini.
 
Nimekulia makuzi na madhira na maudhi ya muwekezaji hewa anaitwa Anger trust lmtd asie na ofisi wala anuani. Siwezi kuwa sehemu ya kuunga mkono wawekezaji kutoka bala asia daima dumu.
Mkuu:
Ni kweli unacho ki-elezea. Miaka 15 ya nyuma aliwahi kuja muwekezaji mwenye asili ya Asia, kwenye sekta ya usafirishaji (Reli) kwa jina la RITES.
Lkn kutokana ufanisi mbovu, ilibainika kuwa sio ile RITES yenye uzoefu iliyopo INDIA.
Kumbe alikuwa ni Muhindi wa hapa Tanzania amewachukuwa Wahindi kutoka India kuwa jina la RITES hatimae wakatimuliwa.
Ni vyema kuchukuwa tahadhari.
 
Mkuu, kwa sasa Bandari ndo inachangia pakubwa kwenye pato la taifa yaani 35%-37% ambayo ni Trilioni 7 kwa Mwaka. DP World matarajio ni kwamba bandari itaweza kuingiza Trilioni 26 kwa Mwaka ndo maana nikasema 97%.

Kama Trilioni 7 ni 35%) Je, Trilioni 26 itakuwa ni asilimia ngapi? Nimepiga hesabu hivyo nikapata 97% Makadirio.

MASAHIHISHO

Bandari inachangia 35% kwenye bajeti ya Tanzania na mategemeo ni ichangie 67% kwenye Bajeti
Mkuu:
Tukirejea kwenye uhalisia.
Ikiwa TPA kwa sasa ufanisi wake ni makasha 600,000 kwa mwaka na huchangia kwenye pato la Taifa kwa mwaka kwa asilimia 35%.
Na DP World atakapo anza ufanisi wake inategemewa kufikia makasha 2,000,000 hivyo atamzidi TPA mara 3.33 zaidi na kupelekea kuchangia kwenye pato la Taifa kwa mwaka kwa asilimia 97%.
Sasa ikiwa TPA atazidiwa ufanisi mara 3.33 zaidi na DP World ni Dhahir pato la Taifa lingetegemewa kuongezeka kwa uhusiano huo (3.33) hivyo tungetegemea kuongezeka kufikia asilimia 116% na si asilimia 97%.
Vinginevyo gharama za DP World ni asilimia 19% la pato la Taifa?

Nafikiri hapa inahitajika ufafanuzi zaidi.
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Anapakia na kupakua makontena MILELE!
 
Tusijadiliane bila mikataba.

Mikataba yote, makubaliano yote, kutoka vyanzo vya serikali iko wapi?

Serikali isipoweka mikataba na makubaliano haya yote wazi, kutoka tovuti zake, hatuna cha kujadili.

Tutachukulia tu kwamba huu usiri unaashiria wizi na rushwa na hivyo mikataba ya usiri by default inapingwa tu.
 
Watu wanachanganya mambo sana kati upakuaji na upakiaji wa makontena bandarini.Bandari kazi yake ni kupakua na kupakia mizigo bandarini meli zinapowasili na kuondoka,hapo zingatia hiyo ni kazi Yao ya msingi,na kazi hiyo ikifanywa kwa ufanisi maana yake gharama za uondoshaji makasha bandarini na muda utakuwa mdogo,hapo nazungumzia port charges na storage.

Hizo gharama ni tofauti kabisa na Kodi ya ushuru na vat ambayo hutozwa na taasisi ya TRA na gharama za viwango ambazo hutozwa na kusimamiwa na TBS,na Kuna gharama za viwango na ubora wa chakula na madawa ambazo husimamiwa na Taasisi ya TMDA,Kuna gharama pia za chemical permit ambazo husimamiwa na GCLA na Kuna atomic permit.Watanzania waelewe hivi vitu,Mimi Niko kwenye biashara ya clearing and forwarding kwa miaka 13 sasa.

Ukweli ni Kwamba DP world wakipewa huu mkataba,ambavyo kimsingi ni kama mkataba waliopea TICTS na kama kweli wakaweka mazingira mazuri ya upakiaji na upakuaji wa makasha hapo bandarini,maana yake ni kuwa tutakuwa na biashara kubwa sana Tena sana.

Na kutakuwa na ongezeko kubwa la ajira kwa vijana wanaofanya kazi za bandarini kuanzia madereva,mama ntilie,wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotoa huduma maeneo yalipo maofisi ya TRA (customs department),maeneo yenye bandari kavu(ICD) na hata maeneo ya mpakani kama Tunduma ambako mzigo mwingi unapita kutokea au kuelekea Bandari ya Dar es salaam.

Watanzania wapewe elimu wajue Kila taasisi inafanyaje kazi, watu wanajua kuwa hao DP world ndio watakusanya Kodi ya ushuru na vat na storage na port charges,na gharama zingine zinazoambatana hapa,DP world anakuja kuleta ufanisi(Efficiency in port operations,loading and offloading, handlings).

Meli kubwa na hata za kawaida zitakuwa zinakuja hazipotezi muda zinashusha na kupakia mzigo na zinaondoka.Maana yake ni kwamba hata gharama za kusafirisha makontena kuja Bandari ya Dar es salaam zitapungua(freight charges),na hata tozo za kupaki meli kubwa na ndogo katika fukwe zetu zitapungua.

Dar es salaam itakuwa ni kitovu Cha biashara za bidhaa kutoka china,ulaya,India na Dubai.Hata mtu mwenye mtaji kuanzia million Tano tu ataweza kuagiza kamzigo kake na kwenda kuuza huko vijijini.
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Kama unachosema ni kweli, Je! ni kwa nini mkataba haujawa specific kwa mambo hayo mpaka waanze kujieleza kwa maneno mengine lukuki kiasi hicho??

Watu sio wajinga kama wewe
 
Naomba nikutoe hofu Mkuu. Ni kwamba hujaujua ukweli.
Ukweli ndio unaoniogopesha.
Ukweli ndo utakuweka huru na kukuondolea hiyo hofu.
Narudia, ukweli ndio unaonitia hofu.
Najaribu kukuelewa kwani mtu aking'atwa na nyoka kila akiona jani anashituka. Mfano wewe umeaminishwa bandari yote inachukuliwa na hujaambiwa ukweli kwamba ni sehemu ili alokuwa anaendesha TICTS.
Hapana, sijaaminishwa. Naelewa na ninajua fika, tumepigwa!. Hata kama sio bandari yote....bado mkataba huo unaonyesha minyororo inayounga hiyo Bandari, ni himaya ya hso DP. it is wrong! na kingine kinachouma zaidi ni matrilioni tuliyoyaweka. Yaani investment iliyowekwa na Serikali haitarudi mapema na kwa makusudio yote yaliyotolewa na bado vitukuu vyangu vitakua na madeni! Pamoja na, ilikuwa wakombolewe
Umeona tatizo linapoanzia Mkuu?
Tatizo ni kubwa mno! Naliona lilipoanzia na litakapoishia....ni ukoloni mamboleo.
 
Madalali wa DP World wamebakia na chaguo moja tu kati ya matatu.

1. Kuufutilia mbali kwanza mkataba huu wa DP World.

2. Kukaa pembeni kwa hiari.
3. Kukalishwa pembeni kwa nguvu.
 
Bdo ndoto zenu wakenya sio? Ili Bandari zenu ziendelee kuwa juu?

Mtasubiri sana nazi chini ya mwembe.

Tanzania ya sasa sio mliyoiziea
 
Watanganyika amkeni muipiganie nchi yenu

Waarabu wanauziwa nchi na watu wasio kuwa wazalendo mliowaamini mkawapigia kura
 
Back
Top Bottom