DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Mkuu, watu wanapotosha, hakuna Mkataba uliojadiliwa. Wakianza kujadili Mkataba ndio wataweka muda. Haya ya sasa ni Maazimio tu ya kufanya biashara ya bandari kati ya Nchi na Nchi. Hata Bunge limepitisha maazimio. Kama maazimip yakikubalika ndipo mikataba sasa inaanza. Yaani hii ni kama barua ya Posa, bado mwali kuolewa.
Dubai ni nchi? if yes ina Kiti umoja wa mataifa? vipi na zile masharti ya hayo unayooita maazimio? hivi huwa maazimiao yanakuwa na masharti?
 
Kwenye Magari Kuna kodi za kimafia hakuna mausiano na bandari hata ukipita boda utachajiwa kiasi hicho.
Kitu kama railway dev levy hii ngumu sana kuingia akilini sema ndio hivyo hakuna namna
 
Ndugu mwandishi akili zako ni timamu kweli?Spika wa jamhuri kasimama hadharani kasema kuwa mikataba yote ya tanzania husainiwa kwanza kabla ya kupelekwa bungeni,.unaposema huu mkataba hujasainiwa hii taarifa umetoa wapii?
 
Kama suala ni uboreshaji kutoka kontena laki 6 kwa mwaka Hadi millioni mbili kwa mwaka,kwanini tusiboreshe wenyewe?jicho la pili linahitajika hapa.hakuna mfanyabiashara anayependa hasara.ikitokea dp world wamesain makubalino ya kulipa ushuru wa trillion 10 kwa mwezi kwa serikali ya tanzania,alafu wakawa wanapata mapato mara 100 zaidi, hapa tunakuwa tumepigwaaaa vibaya
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Watanzania walio wengi wanajua kimombo labda wewe
 
Wanachukua nafasi ya ile kampuni ya Karamagi
Ila kiukweli bandari wanazingua sana wacha waje wawekezaji, miaka yote hamna ripoti bora bandari, CAG analia kila ripoti, Marais wote wanaona kizunguzungu juu ya bandari, rushwa, ukwepaji kodi,wizi ndio nyumbani, ifikie hatua tufanyaje kitu tofauti, kama kukosea ni kwa dhamira nzuri!
 
Sio kweli hapa hapa wizi ni kilasehemu pitia report ya CAG kilakulikopigwa hela kubinafsishwe kwa mwarabu?

Tanzania wizi wa mali zauma ufisadi umekuwa utamaduni wetu achana bandari haiuzwi tuuze mali za ccm kama tunashida na hela.
 
Kiufupi DP World bado hajakabidhuwa rasmi kazi, ila dalili zinaonesha atapewa Gati 1 mpaka 7 alafu TPA watabaki na Gati la Abilia tu! Kazi zote zitasimamiwa na wao wenyewe katika Gati hizo na katika maeneo nyeti mengine nje ya bandari ya Dar watakaoyaona yanawafaa.
 
Kwani nilazima kupewa kwanini msimpe mali za ccm kama mnapenda
 
Narudia tena, watanzania sio wajinga, 2025 Mother out aende zenji au huko Dubai lakini Tanganyika yetu tunaichukua wenyewe.

Kama anadhani ni jokes muache aone coz sio mbali ni keshokutwa tu
 
Kwani nilazima kupewa kwanini msimpe mali za ccm kama mnapenda
Viko vitu vichache tu ula ni vya msingi! ambavyo sikubalini navyo kwenye mkataba mama kati ya Tanzania na DP World!

1. Mkataba ulitakiwa utoe masharti pia kwa mwekezaji sio kwa Tanzania pekee kama ulivyo sasa, Mkataba haunyeshi Tagert ya nchi yetu sio kwa kipindi kirefu ila ata kifupi!

2. DP World apewe tender ya kushusha na kupakia Contena sio kila kitu aratibu yeye.

3. Mkataba mama ulipaswa uonyeshe maeneo gani ya ardhi kampuni itapewa sio kuacha shimo kama lililopo sasa kuwa DP World akiamua tu kwamba sehemu fulani napataka na sisi tumpe tu.

4. Mkataba ulipaswa kuweka mda maalumu kuwa kila baada ya miaka 15 mkataba utakoma na kutoa fulsa ya kuzungumza tena kama kuna mawneo tutaona sasa haya tunaweza fanya wenyewe tuyachukue tufanye wenyewe na yaliyopo bado tuwaache waendelee kwa kurenew mkataba mwingine.
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Kama DP World atafanya kazi za TICTS kwa nini TPA isiingie nae mkataba moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa TICTS? Kama lengo lilikuwa hilo IGA imeingiwa kwa sababu gani wakati ilikuwa rahisi kuingia nayo mkataba kama kampuni bila ya IGA?

Kama DP World Imeletwa ili kuongeza ufanisi na kupunguza upigaji kwa nini maeneo yenye upigaji mkubwa ( mafuta, magari n.k.) yametolewa katika mkataba?

Msitake kusogeza magoli kwa ku insinuate kuwa wanaohoji mkataba huu wamehongwa na Kenya au nchi nyingine washindani. Watu wanahoji kwa kuhofia kuwa hatma yake sio nzuri kwa nchi yao. Bahati mbaya mpaka sasa hivi majibu yenu hayajaondoa hofu zao.

Mimi binafsi naona Waziri Mbarawa anajitahidi kujibu ( ingawa majibu yake hayatoshelezi( na anajibu kwa heshima. Sio kama viongozi wengine wa kisiasa.

Amandla...
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Hii ndio shida ya mambo ya muhimu na mambo ya kitaalam kuongelewa na watu ambao hamna wanalolijua

Umewahi kusoma document za huo mkataba? Umesoma vizuri ukaelewa?
 
Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.

Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.

Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.

Watu wanapinga because ya uelewa mdogo

Yan Jambo ni kubwa na zito but awareness ni ndogo Sana, hata wataalamu hawajapata muda wa kuliongelea zaidi ya wanasiasa tu

So kila mtu anaongea kipande anachokijua yeye

Hata ww umeongea 1% tu
 
Vipi kuhusu Zenji? Kuleni nchi waarabu, zama zenu hizi. Tumeshaanza kuona joto ya jiwe mitaani. Mandinga tunayaona na kanzu zenu.
 
Viko vitu vichache tu ula ni vya msingi! ambavyo sikubalini navyo kwenye mkataba mama kati ya Tanzania na DP World!

1. Mkataba ulitakiwa utoe masharti pia kwa mwekezaji sio kwa Tanzania pekee kama ulivyo sasa, Mkataba haunyeshi Tagert ya nchi yetu sio kwa kipindi kirefu ila ata kifupi!

2. DP World apewe tender ya kushusha na kupakia Contena sio kila kitu aratibu yeye.

3. Mkataba mama ulipaswa uonyeshe maeneo gani ya ardhi kampuni itapewa sio kuacha shimo kama lililopo sasa kuwa DP World akiamua tu kwamba sehemu fulani napataka na sisi tumpe tu.

4. Mkataba ulipaswa kuweka mda maalumu kuwa kila baada ya miaka 15 mkataba utakoma na kutoa fulsa ya kuzungumza tena kama kuna mawneo tutaona sasa haya tunaweza fanya wenyewe tuyachukue tufanye wenyewe na yaliyopo bado tuwaache waendelee kwa kurenew mkataba mwingine.
Kuna kitu hujaelewa bado. Makubaliano ya mashirikiano hayana muda

Pili Hakuna mkataba wa Bandari haddi sasa.

Tatu DPW anapewa sehemu ya bandari ya Dar aiendeshe.

Nne, hapewi kitu kingine nje ya sehemu ya bandari ya Dar.

Sema wewe umesoma upotoshaji na ndio umeshikia bango kama watu wengine. Ila taratibu tutaelewana
 
Back
Top Bottom