DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Hakuna maslahi ya Taifa Kwenye hiki ulichoandika hapa. Kusema IGA siyo mkataba unamaanisha inaweza kupuuzwa wakati wa kuingia HGA? Mbona baada ya MoU imefuata IGA ambayo haijaivunja MoU hata kipengele kimoja?
Huko kwenye sheria si ndo mnafanya mitihani watu 630+ lakini wanafaulu 20+? Wewe uko kundi lipi Kati ya hayo? Kwa uandishi huu wewe uko kundi la "Wengi wape".
 
Hakuna maslahi ya Taifa Kwenye hiki ulichoandika hapa. Kusema IGA siyo mkataba unamaanisha inaweza kupuuzwa wakati wa kuingia HGA? Mbona baada ya MoU imefuata IGA ambayo haijaivunja MoU hata kipengele kimoja?
Huko kwenye sheria si ndo mnafanya mitihani watu 630+ lakini wanafaulu 20+? Wewe uko kundi lipi Kati ya hayo? Kwa uandishi huu wewe uko kundi la "Wengi wape".
 
Magufuli hakuwa mtu wa kuingia mikataba ya kichoko ya kuuza rasilimali pamoja na madhaifu yake yote. Hakuwa na akili mbovu kiasi hicho.
 
Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni
Mkuu wa stendi , news ni bure, kuandika ni bure, situmii gharama yoyote apart from time, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika bure kwa kujitolea silipwi na yeyote!.
P
 
Mkuu wa stendi , news ni bure, kuandika ni bure, situmii gharama yoyote apart from time, mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika bure kwa kujitolea silipwi na yeyote!.
P
𝙿𝚊𝚜𝚌𝚑𝚊𝚕 𝚖𝚋𝚘𝚗𝚊 𝚞𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚖𝚙𝚘𝚕𝚎 𝚗𝚍𝚞𝚐𝚞
 
mikataba ya kichoko ya kuuza rasilimali
Naomba tuache kutumia lugha za matusi!, hakuna rasilimali yoyote iliyokuwa!, inachokuja kufanya DPW ni kile kile kilichokuwa kinafanywa na Ticks ila sasa more efficiently and mechanized!
.Hakuwa na akili mbovu kiasi hicho.
This is defamatory statement, umefanya kitu kinachoitwa defamation by innuendo!
P
 
𝙿𝚊𝚜𝚌𝚑𝚊𝚕 𝚖𝚋𝚘𝚗𝚊 𝚞𝚖𝚎𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚖𝚙𝚘𝚕𝚎 𝚗𝚍𝚞𝚐𝚞
Mimi siku zote ni mtu mpole, ila pale unapojitolea kutetea maslahi ya taifa bure kwa kujitolea, halafu linatokea lijitu lijinga, linakutuhumu umepokea bahasha!, lazima utakasirika!.
P
 
Mimi siku zote ni mtu mpole, ila pale unapojitolea kutetea maslahi ya taifa bure kwa kujitolea, halafu linatokea lijitu lijinga, linakutuhumu umepokea bahasha!, lazima utakasirika!.
P
Unashida mahali,umeacha kujibu hoja zote zilizozungumziwa na wadau uko nyuma lakini unaenda kujibu comment ya mtu anaekuuliza kuhusu upole wako .Wewe umeleta bandiko la ufafanuzu juu ya swala la makubaliano ya ubinafsishwaji w bandali za Tanzania na Dubai lakini umejibiwa kwa hoja nyingi sana na watu makini sana lakini umeshindwa pia kuwajibu hoja zao ili tuone bandiko lako sio batili.Nasema hivi kwasababu umesoma hoja za watu waliokuelewesha utata wa huo mkataba na umekubaliana nao na huna zaidi Cha kuwapinga Basi kubali tu na uchutame ,muugwana akivuliwa nguo huchutama Kaka pasko
 
Kwa umri mimi ni mwanao wa mwisho. Nina maswali machache kidogo.
1. Umesema hii ni IGA. Yani ni memorandum of understanding. Je mbona kuna sehemu imesema tayari walishaingia MOU toka February?
2. Mbona hatuna uwezo wa kujitoa??? Kwa nini?? Hata tukiwa vitani na UAE bado hatujitoi kwenye makubaliano. Je twaweza kuwa na bandari zote chini ya mtu mmoja tena ambae twaweza kupigana nae siku moja?
3. Tumempa eneo la bandari zetu zote. Pia tumempa mamlaka ya kuanzisha maeneo ya kiuchumi kama tulivyo na ile export processing zones. Je, unajua hatutaweza tena kuanzisha eneo la kiuchumi maana haki zote tumempa DP World?
4. Kwenye mambo ya muungano kwa mujibu wa katiba ya Tanzania toleo la 2000, namba 11 kwenye nyongeza ya kwanza inahusu usafiri wa anga, bandari, mawasiliano na posta. Je kwa nini bandari za Zanzibar ambazo ni mambo ya muungano hazijawekwa humo??? Tuwaamini vipi wazanzibar wawili waliopewa dhamana mmoja wa kusimamia vya muungano na mwingine vya muungano na vya Tanganyika??? Tukidai Tanganyika je, tunakosa???
 
kaka kuna watu wanapinga kwa ujinga hawana wanalijua,lakini kuna watu oia wamepewa fedha na tics ili kuuupinga tu mkataba
 
Iga ni intergovernmental agreement au memorandum of understanding kati ya sirikali ya Tz na Sirikali ya Dubai? Sasa DPW ni sirikali.
Pili katika IGA kwa sababu unahusisha sirikali kwa sirikali kwanini Mwana Sheria Mkuu asiwe ndio mtia Saini labda labda na waziri wa mambo ya nje .
 
Hivi nkataba wa loliondo unasemaje na tulinufaika nini na bado unaendelea?
 
Sasa Defamation kafanyiwa nani hapo? Au kuna defamation za hisia mkuu?

Magufuli ameshakufa au kuna kesi za marehemu siku hizi?

Kingine wakati TICTS wanapewa mkataba je kulikuwa na vificho vificho juu ya namna ambavyo umeingiwa na ukomo wake wa kuishi.
 
Nyerere alishindwaje? Alijenga kila kitu kwa jasho na damu vilikufaje? Maana alipaswa kuwa mwenye hasira kali zaidi, UNAPIKUWA POSITIVE, NA MAZINGIRA YOTE YAKAWA NEGATIVE, WORK DONE HUWA ZERO HATA UWE NA JUHUDI GANI.
Ndio maana nikakuambia Serikali iliyopo haina uhalali wa kutuongoza.
Maana imekiiri yenyewe kuwa haiwezi kutusimamia watanzania,
yaani watu wote wamekuwa "negative' hili ni tusi kwa waTanzania na Serikali yenyewe.
Hata km ni kweli waTZ wote ni wezi Serikali ingeweza kufunga mfumo mzuri wa kudhibiti hao wezi au hata kuajili watu kutoka mataifa mengine na sio kugawa bandari zetu kwa kisingizio hicho Cha aibu.

Pia Nyerere alishindwa wapi na kipi?
Maana ubinafsishaji holela ulianza baada ya Nyerere kutoka madarakani.
 
Japo kuwa sina uelewa mkubwa na masuala ya kisheria,

Nikiangalia mikataba ya miaka ya nyuma huko.

Nikaangalia na jinsi hayo makubaliano na DP world yamekuwa drafted,

Nkiangalia jinsi watu wanavyoreason baadhi ya vipengele vya hayo makubaliano,

Nikiangalia jinsi mnafail kujibu hizo hoja kiufasaha mnaishia kukaa kimya kama ulichokifanya humu, umeleta hoja ya utetezi kwa kujiamini kabisa na watu wanakujibu then umekaa kimya.
Hapo jibu ni kuwa umezidiwa hoja, ulikuja kudanganya watu na nikienda mbali zaidi kimawazo nnahisi wewe uko kiitikadi zaidi kama siyo maslahi tu.
Wewe ni CCM hivyo lazima umkingie kifua Rais kivyovyote vile.

Binafsi naona hawa watu wanaopinga hzo agreement wanamantiki, wameiwin psychologia za watanzania wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…