DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

Kwa watanzania walivyo wajinga wajinga na wavivu nawashauri wabaki TPA!
Hao DPW sio watu wa mchezo wajiandae kwa mchaka mchaka chinja….kama ni mwizi lazima wakutose baharini hawana mchezo ndio maana wanesema wanaotaka kuajiriwa na sio wanaotaka kuamia maana yake unachagua kuacha kazi TPA au kubaki au kwenda kuajiriwa DPW na utasaini mkataba mpya hapo hautozidi miaka mitano….
Kwa watanzania niwajuavyo watapoteza kazi sana hapo…
Mifumo ya KPI inayoendesha private sector ndio mwarobaini kwa hili tatizo , watu wanaajiriwa kula mishahara ya bure tu ,mengine yashazeeka na kustaafu hayataki
Ndio hayo ya inefficiency ya hizo bandari na TPA

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Wale waliokuwa wakitetea kuwa DP World wakija hawatapunguza watu kazi njooni hapa mtueleze. Jamaa ndio wameishauziwa taratibu wanaanza kuondoa watu. Kiko wapi?

---
Tarehe 22 Oktoba, 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliingia Mkataba na Kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai unaohusu uendeshaji wa Gati Na. 0 hadi 3 na Gati Na. 4 hadi 7 za Baridari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30). Kutokana na makubaliano hayo yanayohusisha usimamizi na uendeshaji wa maened tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam wanapaswa kuchagua kati ya kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na papo hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.

Menejimenti imekamilisha zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi wote wa TPA walio kwenye maeneo husika lililoanza Tarehe 4 hadi 19 Machi, 2024 kwa lengo la kuwapa Watumishi wote uelewa sahihi wa mabadiliko ya uendeshaji yanayoendelea Bandari ya Dar es Salaam. Pamoja na masuala mengine, elimu hii inahusisha mabadiliko ya uendeshaji wa bandari, utaratibu wa makabidhiano, utaratibu wa mtumishi kusitisha mkataba na TРА па раро hapo kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World (KWA MTUMISHI ATAKAYEKUWA AMEAMUA KUFANYA HIVYO KWA HIYARI YAKE MWENYEWE BILA KUSHURUTISHWA), pamoja na stahiki ambazo zitatolewa na TPA kwa mtumishi atakayeamua kusitisha mkataba wa ajira wa TPA na kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World.

Kwa msingi huo, nawajulisha Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa, makabidhiano kati ya TPA na Kampuni ya DP World yameanza kutekelezwa. Kwa kuwa zoezi la utoaji elimu kwa Watumishi limekamilika, Watumishi watakaoamua kuajiriwa upya na Kampuni ya DP World wanatakiwa kufika na kuorodhesha taarifa zao Jengo la TPA Makao Makuu, Ukumbi wa Mikutano Ghorofa ya 32 kabla au ifikapo Tarehe 29 MACHI, 2024.

Update:
- Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam
Parapanda italia
 
Apo kama hutaki kwenda Dp word....ujiandae kwenda bandari za masasi au namtumbo ukadili na wavuvi haramu..[emoji23]
 
Mimi kwa maoni yangu wakimaliza kubinafsisha TPA wafate Dart mwendokasi. Na yenyewe apewe muwekezaji mgeni

Waswahili hatuwezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Tunapenda ajira kuliko majukumu ya ajira
Mimi naomba ibinafsishwe TANESCO
 
Kwanza utakuwa unafuga majini wewe!Shahada yenyewe uliyonayo ni miaka 1980s .Tukikupeleka kwenye Telecommunication towers za sikuhizi huna unachokijua .
Hakuna jipya linalokua gumu duniani.

Hao unaowaona wa zamani ndiyo waliokuletea hayo unayoyaona mapya.
 
Back
Top Bottom