Hello JF Members....
Sijausoma mkataba (nina aleji na maelezo marefu so nitapita humu kny hii topic kwa kusikia maneno ya watu wakiuuzungumzia... 😁 😁 😉),
Binafsi SIUFAGILII...
1. Nimeona moja ya reason ni kuwa bandari yetu ilikua na uozo mwingi ilikua haileti tija kwa taifa, hiii sio enough kwa sisi wengine kuingia into such contract, sababu ukiziweka kwenye lens sectors/offices nyingi nchini zina perform below standard level, uozo ni mwingi Je tukianza kuingia kwenye mikataba na nchi nyingine hamuoni kuwa hii inamaanisha itabidi tuingie mikataba na sectors zote nchini, that means ultimately ni nchi yetu kutawaliwa na nchi nyingine, unless hili ndilo mnalitaka kutawaliwa na nchi nyingine kisa mmeshindwa kujiendesha na kuwa na confidence ya kujiletea maendeleo wenyewe kama taifa.
2. Kama ni uozo kiutendaji kwa nini tusi deal specific na uozo?,badala ya kuingia kwenye deal kubwa kwa taifa kusolve minor issue kama tu administration bandarini? Kwa nini kutumia rungu kubwa kutaka kumuua inzi??? Namaanisha kwa nini kuingia mkataba mkubwa nchini kwa ishu ndogo tu kama UTENDAJI? Kuuza nchi yetu was this effective possible solution kwa uozo nchini? hell no sababu hata hao walionunua nchi hujui kama hawataoza baada ya kipindi,namaanisha mkataba una ambiguity in long term na ambiguity peke yake inamaanisha haikuwa effective solution to our problem.
Again uozo upo karibu sehemu zote nchini, kama bandari mme identify ina uozo mwingi kwa nini msitumie bandari hio hio kama model kujenga framework kuondoa uozo katika bandari na sectors zote nchini?,naona mmeweza ku identify tatizo ila mmeshindwa kuja na simple but effective solution, characteristic of incompetent leaders!. Kushindwa kutumia creativity?critical thinking for solutions ambazo hazina ambiguity in long term.
Sikatai mkataba una immediate benefits but was this only EFFECTIVE solution?,Kwa nini hakukua na analysis ya all possible solutions na kuja ambayo haiko costly in long term kwa watanzania? sawa mtaniambia costs kwa watanzania kwa sasa na baadae hazijulikani ,sawa ila kama costs HAMZIJUI is this not enough reason kuuona huu mkataba hautufai?.
Mimi sina ufahamu na hii DP World, nasikia ina operate nchi nyingine, je tutatumia kigezo wao kuwa successful nchi nyingine kama kigezo kuwa watakuwa successful nchini kwetu? je hizo nchi nyingine hazina factors nyingine zinazowafavour wao kuwa successful ambazo kwetu hamna au baadae hazitakuwepo??, ningependa kujua kwenye hii topic,nielimisheni kama hizi nchi wanazo operate zina profile kama letu na wameweza kuwa successful particularly wame contribute nini ili tufanye comparison.
At least miaka 100 ya wao ku operate kwenye least developed country na jinsi walivyo contribute 🙂🙂😉 .Ningekuwa conviced kama bandari yetu ingekuwa imeshikilia 75% ya uchumi wetu na kuna demonstratable factors zinazoonyesha kutakuwa na maendeleo zaidi ya hapo au baada ya miaka fulani tutakua tumefikia uchumi fulani sio na maendeleo kidogo,viajira vichache kila mwaka ndio i justify mkataba usio na kikomo.
At least kungekuwa na community participation. watanzania tuu udiscuss huu mkataba kabla ya kuwa signed. Tungekua tunajua,tunadiscuss huu mkataba kabla haujasainiwa kusingekuwa na confusion kama sasa hivi. Sijui kwa nini serikali iliona mkataba huu ambao ni mkubwa na wa kudumu sio swala la watanzania. Kwanza tungediscuss watanzania wangeweza kuna na possible alternatives na kila mtu kuwa happy.
Sio mwandishi mzuri, sorry.