Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,753
tutagombana sana. ninakiri kuamini kwamba, tungeruhusu wachina kujenga bandari ya bagamoyo, ingepunguza mzigo mwingi sana unaopitia dubai toka china, ndio maana waarabu wanasema hatutaruhusiwa kuendeleza bandari zingine. ninashauri, hawa DP WORLD wapewe tu bandari waiendeleze, ila kipengele cha kuendeleza bandari zingine kisiwepo kutuzuia, turuhusiwe kuendeleza ili wachina waendeleze bandari ya bagamoyo au Tanga au hata sisi wenyewe tukipata pesa tuendeleze wenyewe. na wao DP WORLD hawataathirika kama watakuwa na huduma nzuri mbona wataendelea kupata wateja tu? na huyo mwignine akitaka kuendeleza atashindana nao tu na wote wakiwa na huduma nzuri, ndio faida kwa Tanzania.
TUSIKUBALI MONOPOLY, kwamba mtu mmoja tu ndio awe na mamlaka na bandari zote za bongo, ati tusiendeleze zingine. tumekujengea bandari, tumekujengea na SGR usafirishe mizigo, wewe unaongeza mtaji wa technolojia tu na maboresho ya kiutendaji, afu unataka kutuzuia sisi tusiendeleze bandari zingine? wanajua wakituruhusu kuendeleza zingine tutawapiku dubai, na wamekuja makusudi kwasababu wameshaona Tanzania ni gateway ya landlocked countries na tumejenga SGR ambayo itaifaidisha sana bandari, hivyo wanataka tusijekuendeleza kabisa bandari nyingine ili dubai iendelee kuwa kiini sisi tusiwe kiini?
imagine, DP world wakichukua Dar port, China wakajenga ya Bagamoyo, SGR ipo vizuri hadi mwanza nadi RWanda, tazara ipo vizuri, reli toka Dsm hadi Tanga na Tanga hadi kilimanjaro hadi mwanza kwaajili ya uganda ipo vizuri. bandari zetu tatu (bagamoyo, tanga na dsm) zitamonopolise uchumi wa africa mashariki. wao wanataka DAr port peke yake ndio iwepo na tusiendeleze ingine itakayopunguza mizigo ya moja kwa moja toka china hadi TAnzania, wanataka ipitie dubai. sijui naeleweka?