DP World Washusha Meli yenye Kontena 4,000 Dar Port. Meneja TPA asema ni matokeo ya uwekezaji, adai huo ni Mwanzo tu

Watu wameagiza mizigo 10/04/2024 Hadi Leo hawajapata....
Nashangaa Hawa wanaoshabikia ukubwa wa meli wakati meli zinakaa foleni mwezi mzima pale bandarini zikisubiri zamu Yao kushushia mizigo IFIKE.
Hawa DP sijaona faida Yao mpaka sasa
Kuna jamaa mmoja, nisimtaje jina humu, lakini afisa wa juu wa bandari, nilipomwuliza mabadiliko yaliyoletwa na DP World, alinijibu kuwa HAKUNA CHOCHOTE, NI UHUNI TU UMEFANYWA.
 
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Gallus amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na uwekezaji wa Kampuni ya DP- World.
Kwanini wasiwaache DPW wenyewe wazungumze maana ndiyo wanaweza kila kitu sisi hamna kitu ndiyo maana tumegawa bandari kwa wanaoweza
 
unajua madhara ya imbalance ya imports vs exports kwenye uchumi wa nchi? no wonder nchi nzima imegeuka wachuuzi, kila mahali fremu halafu unashangilia meli kubwa ya imports …
Watu wanazungumizia saiv bandari inauwezo wa kupokea meli kubwa kuliko mwanzo na hio iliokuja ndio yakwanza ...asa we unaanza mambo ya import na export huoni we ni chizi
 
unajua madhara ya imbalance ya imports vs exports kwenye uchumi wa nchi? no wonder nchi nzima imegeuka wachuuzi, kila mahali fremu halafu unashangilia meli kubwa ya imports …
Sasa hapo unachanganya mambo, moja ya kazi ya bandari ni kuweza kumudu kuingiza mizigo kwa ufanisi ,na utaweza kufanya hivyo kama utakuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa ,kumbuka kwamba tunahudumia nchi mbali mbali zilizotuzunguka kwahiyo usifikiri hii meli inaleta mizigo ya tanzania tu ,rwanda, congo, zambia,uganda, malawi hawa wote wana mizigo yao humo na wanategemea waipate kwa uharaka ili na nchi yetu iingize pesa kupitia huduma hii, kuna dreva wa kupeleka hayo magari, kuna malori ya kubeba kontena, mafuta ,wauza chakula kuhudumia wageni wanaokuja kufuatilia mizigo yao, hotels etc
Unapozungumzia bandari na meli kubwa kama hii kuna wadau wengi na faida nyingi zinazopatikana kwa nchi na wananchi
 
Hivi huwaga meli zikikaa pale oyster bay mpaka mzigo ushushwe unachukua miezi mingapi?
 
Hapo kidogo inaleta mantiki
 
Jamaa wenye akili zenye mipaka hawawezi kuelewa maana ya meli kubwa kufika na kuhudumiwa pale TPA wao wanakuja na akili zile zile kwamba tunaibiwa!.

Kwamba volume zinazofanyiwa kazi pale TPA ni kubwa kuliko zile za zamani, kwao sio kitu chenye kuonekana kuwa ni faida ya uwekezaji.

Siasa zinakuwa ni nyingi sana na kutunyima uwezo wa kuutazama uhalisia wa mambo.
 


Ilitakiwa utuambie bfr meli kama hiyo ilikuwa inashindwa kuingia Kwa Sababu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…