BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Isha kija ya Magari nahisi, hizi ni Propaganda mkuu, Taifa limejaaa watu wanao waza kwa Kamasi tupuInamaana haijawahi kuja meli ya ukubwa huo? Be serious
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Isha kija ya Magari nahisi, hizi ni Propaganda mkuu, Taifa limejaaa watu wanao waza kwa Kamasi tupuInamaana haijawahi kuja meli ya ukubwa huo? Be serious
Yanarudi tupu hayo, hakuna mi,igo ya kubeba, huku ni Dampo,Hayo makontena ndiyo yataondoka na vyetu
Nyie viumbe huwa hamueleweki mnataka nini hasa? Kwani bandari zote ulimwenguni zinaangalua experts pekee na sio imports?hizo ni imports, unafurahia imports? angalau ingeondoka bidhaa for exports hapo ningeelewa lkn unafurahi imports???
Unahisi? Lete facts na data hapa sio habari za kuhisi.Isha kija ya Magari nahisi, hizi ni Propaganda mkuu, Taifa limejaaa watu wanao waza kwa Kamasi tupu
Yatarudije matupu wakati mali ghafi nyingi za viwanda vya China na Ulaya zinatoka kwetu?Yanarudi tupu hayo, hakuna mi,igo ya kubeba, huku ni Dampo,
Magufuli kachimba na kutanua bandari harafu sifa anapewa DP world na machawa wajinga wajinga wakati meli kama hizo toka 2021 zilikuwa zinatia nanga hapo ila kwa ushoga wako unagawa sifa tu kwa mabasha zako ambazo hawanaHaya Sasa DP World wameanza kufanya Yao Dar Port Kwa kuleta meli kubwa zaidi ,urefu zaidi ya mita 300👇👇
Kampuni ya DP World iliyoingia ubia na Serikali kwa ajili ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam imeingiza meli ya kwanza yenye urefu wa mita 294.12 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji na maboresho yanayofanywa na kampuni hiyo katika kuendesha bandari hiyo.
Hayo yameelezwa na meneja mizigo mchanganyiko wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA, Abed Galusi.
My Take
Kasi ya kuondoa mzigo ili.kuepusha Msongamano itaendana? 👇👇
Meli kubwa ya MSC ADU V iliyobeba makasha 4,000 imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa meli yenye mzigo mkubwa wa makontena kuwasili Tanzania.
MSC ADU V iliyotengenezwa mwaka 2005 ina urefu wa mita 294.12 unaokaribiana na viwanja vitatu vya mpira wa miguu imetia nanga leo Jumamosi Juni 22, 2024.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Gallus amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na uwekezaji wa Kampuni ya DP- World.
Gallus amesema bandari ya Dar es Salaam imefanya maboresho katika kina cha maji na ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa.
Amesema mwanzo kulikuwapo na kina cha mita nane hadi 12.7 sasa hivi kipo 14.5 chenye uwezo wa kuingiza meli yenye urefu wa mita 305 na kina 13.5.
"Hii ni historia kwetu hapo mwanzoni tulikuwa tunaingiza meli zenye urefu wa mita 267, tumeongeza uwezo wa bandari yetu ya Dar es Salaam katika uingizaji wa meli.
"Uwezo wa utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam utazidi kuimarika zaidi kwa sababu hivi sasa tuna mwekezaji mpya DP World aliyeanza kazi na mabadiliko yameonekana mfano ni meli hii kubwa,"amesema Gallus.
Gallus amefafanua kuwa katika usafirishaji ukipokea meli kubwa unaongeza kiwango cha mizigo unaokuja katika bandari husika sambamba na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo.
Pia Soma
- Bandari ya Dar es salaam yazidi kupokea meli kubwa duniani
Wabongo, kwa hiyo Dar port inashusha bidhaa kwa ajili ya Tanzania tu na je, hapo kabla ya DP World kuingia, tushawahi kupata hiyo Balance of trade
Nadhani swali sahihi sio Import vs Exports Ila je, management ndio sababu ya kupokea meli kubwa au kuongezeka kwa capacity ya "bandari" Mfano kina chake katika kuhudumia meli kubwa
Na je, kazi ya magufuli ya upanuzi wa bandari setu imeleta impact gani au hii tunaoiona yawezekana ni impact yake kuliko kuingia kwa Dp World?..
Hapana mwisho ilikuwa meli ya container 2000 kwa sababu ya kina ila Dp word hawa jaongezakina wao waonekuta tayari TPA wameshaongeza kina cha bandari wao wameongeza mashine za kushusha mzigo mkubwa kwa haraka
Ni mabadiliko gani waliyafanya kuwezesha kuleta meli kubwa ambayo sisi wenyewe tulishindwa kuyafanya?
Iweje leo makasha 4000 mseme haijawahi kutokea? Acheni siasa za bei rahisi na ishatia nanga meli mwaka juzi ilikua na makontena 6000, acheni siasa za bei rahisi kwenye bandari mmevuruga tunawakalia kimya mnatuona mafara, mara gawio wakati tpa ishawahi kutoa gawio kubwa miaka mingi ilopita kuliko gawio lenu
Hauamini unachokisoma?
Ahsante mama Samia.
Aisome FaizaFoxy hii na makuwadi wengine.Miaka 6 nyuma yaani 2018 , meli aina ya northern power ilishusha, makasha 5000, katika bandari ya Dar, siasa zenu za bei rahisi kawafanyieni watoto
Maersk Cubango ilipiga nanga hapo Waziri wa uchukuzi akiwa Mwakyembe ilikuwa na container 4000, tunasahau sana.
Lazima tu export kama tunataka kukuza uchumiHayo makontena ndiyo yataondoka na vyetu
Unahisi? Lete facts na data hapa sio habari za kuhisi.
Meneja wa bandari mwenye mamlaka na takwimu zote za meli zilizowahi kuingia amesema hii ndio meli ya kwanza kubwa kihistoria kutia nanga bandarini hapo sasa wewe unakuja na hisia zako usiyekuwa hata na uelewa wa mambo ya bandani.
Ungejibu kwa hoja ungetusaidia sana sie wasomaji tuelewe vizuriHuo ni Mwanzo tuu,mtajambishwa sana
Kama muda wa kutoa mzigo bandarini haujabadirika mpaka leo bado naona DPW wanayo kazi ngumu, kuna meli zimefika toka tarehe 13/6/2024 lkn mpaka leo hazijashusha mizigo.Ni hii ni mwanzo tu bado mambo makubwa mazuri yanakuja.
Wenye wivu na Mama lazima watahara damu mwaka huu!!!
Kazi inaendelea.
Hao ni waongo tu, kuna meli zimefika 13/6 na bado hazijashusha mizigo lkn hiyo iliyofika jana eti itakaa kwa muda wa siku 5 tu. Je kwa nini meli zilizofika tarehe 17 mbona hazijapangiwa siku ya kusha?Huyo meneji atakuwa punguani au aliyepofushwa akiki na rushwa ya mwarabu.
Kumbukumbu zipo za meli zilizowahi kuketa makasha zaidi ya 4,000; halafu useme kuwa eti kuna mwehu anaitwa meneja wa bandari anasema hakuna meki kubwa kuliko hiyo ya makasha 4,000 iliyowahi kutia nanga bandari ya Dar!! Kichaa mkubwa huyo. Kweki rushwa huondoa akili na aibu.