Haya Sasa DP World wameanza kufanya Yao Dar Port Kwa kuleta meli kubwa zaidi ,urefu zaidi ya mita 300👇👇
Kampuni ya DP World iliyoingia ubia na Serikali kwa ajili ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam imeingiza meli ya kwanza yenye urefu wa mita 294.12 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji na maboresho yanayofanywa na kampuni hiyo katika kuendesha bandari hiyo.
Hayo yameelezwa na meneja mizigo mchanganyiko wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA, Abed Galusi.
My Take
Kasi ya kuondoa mzigo ili.kuepusha Msongamano itaendana? 👇👇
Meli kubwa ya MSC ADU V iliyobeba makasha 4,000 imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa meli yenye mzigo mkubwa wa makontena kuwasili Tanzania.
MSC ADU V iliyotengenezwa mwaka 2005 ina urefu wa mita 294.12 unaokaribiana na viwanja vitatu vya mpira wa miguu imetia nanga leo Jumamosi Juni 22, 2024.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Gallus amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na uwekezaji wa Kampuni ya DP- World.
Gallus amesema bandari ya Dar es Salaam imefanya maboresho katika kina cha maji na ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa.
Amesema mwanzo kulikuwapo na kina cha mita nane hadi 12.7 sasa hivi kipo 14.5 chenye uwezo wa kuingiza meli yenye urefu wa mita 305 na kina 13.5.
"Hii ni historia kwetu hapo mwanzoni tulikuwa tunaingiza meli zenye urefu wa mita 267, tumeongeza uwezo wa bandari yetu ya Dar es Salaam katika uingizaji wa meli.
"Uwezo wa utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam utazidi kuimarika zaidi kwa sababu hivi sasa tuna mwekezaji mpya DP World aliyeanza kazi na mabadiliko yameonekana mfano ni meli hii kubwa,"amesema Gallus.
Gallus amefafanua kuwa katika usafirishaji ukipokea meli kubwa unaongeza kiwango cha mizigo unaokuja katika bandari husika sambamba na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo.
Pia Soma
-
Bandari ya Dar es salaam yazidi kupokea meli kubwa duniani