DP World Washusha Meli yenye Kontena 4,000 Dar Port. Meneja TPA asema ni matokeo ya uwekezaji, adai huo ni Mwanzo tu

DP World Washusha Meli yenye Kontena 4,000 Dar Port. Meneja TPA asema ni matokeo ya uwekezaji, adai huo ni Mwanzo tu

hizo ni imports, unafurahia imports? angalau ingeondoka bidhaa for exports hapo ningeelewa lkn unafurahi imports???
Nyie viumbe huwa hamueleweki mnataka nini hasa? Kwani bandari zote ulimwenguni zinaangalua experts pekee na sio imports?

Hakuna nchi duniani inayojitegemea kwa kila kitu 100% lazima kuwe na imports. Sisi tunachozungumzia sio imports ama exports bali ongezeko la mapato yanayotokana na bandari.
 
Isha kija ya Magari nahisi, hizi ni Propaganda mkuu, Taifa limejaaa watu wanao waza kwa Kamasi tupu
Unahisi? Lete facts na data hapa sio habari za kuhisi.

Meneja wa bandari mwenye mamlaka na takwimu zote za meli zilizowahi kuingia amesema hii ndio meli ya kwanza kubwa kihistoria kutia nanga bandarini hapo sasa wewe unakuja na hisia zako usiyekuwa hata na uelewa wa mambo ya bandani.
 
Hawa watu wanawafanya Waatanzania hawana akili. Maboresho ya kuongeza kina cha bahari yalifanyika kwa mkopo wakati wa awamu ya 5, ambapo serikali ilichukua mkopo wa dola bilioni 1.

Hivi kuleta meli kubwa, nayo ni maboresho? Ukisikia ubabaishaji na hadaa ndiyo hii. Inaonekana hawa watu baada ya ya wizi wao na ule mkataba wa kishenzi kugundulika, wanahangaika sana mioyoni mwao wakifikiria wafanye nini kuwapumbaza Watanzania.

Enyi mafisadi wakubwa na waporaji wa rasilimali za nchi, mnahangaika bure, Watanganyika wana akili timamu, na ushenzi uliofanyika kwenye bandari hautaondoka kwa bla bla za kijinga. Kinachotakiwa ni kufutwa au kurekebishwa ile IGA ya kishenzi.
 
Haya Sasa DP World wameanza kufanya Yao Dar Port Kwa kuleta meli kubwa zaidi ,urefu zaidi ya mita 300👇👇


Kampuni ya DP World iliyoingia ubia na Serikali kwa ajili ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam imeingiza meli ya kwanza yenye urefu wa mita 294.12 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji na maboresho yanayofanywa na kampuni hiyo katika kuendesha bandari hiyo.

Hayo yameelezwa na meneja mizigo mchanganyiko wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA, Abed Galusi.

My Take
Kasi ya kuondoa mzigo ili.kuepusha Msongamano itaendana? 👇👇
Meli kubwa ya MSC ADU V iliyobeba makasha 4,000 imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa meli yenye mzigo mkubwa wa makontena kuwasili Tanzania.

MSC ADU V iliyotengenezwa mwaka 2005 ina urefu wa mita 294.12 unaokaribiana na viwanja vitatu vya mpira wa miguu imetia nanga leo Jumamosi Juni 22, 2024.

Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Gallus amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na uwekezaji wa Kampuni ya DP- World.

Gallus amesema bandari ya Dar es Salaam imefanya maboresho katika kina cha maji na ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa.

Amesema mwanzo kulikuwapo na kina cha mita nane hadi 12.7 sasa hivi kipo 14.5 chenye uwezo wa kuingiza meli yenye urefu wa mita 305 na kina 13.5.

"Hii ni historia kwetu hapo mwanzoni tulikuwa tunaingiza meli zenye urefu wa mita 267, tumeongeza uwezo wa bandari yetu ya Dar es Salaam katika uingizaji wa meli.

"Uwezo wa utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam utazidi kuimarika zaidi kwa sababu hivi sasa tuna mwekezaji mpya DP World aliyeanza kazi na mabadiliko yameonekana mfano ni meli hii kubwa,"amesema Gallus.

Gallus amefafanua kuwa katika usafirishaji ukipokea meli kubwa unaongeza kiwango cha mizigo unaokuja katika bandari husika sambamba na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo.

Pia Soma
- Bandari ya Dar es salaam yazidi kupokea meli kubwa duniani
Magufuli kachimba na kutanua bandari harafu sifa anapewa DP world na machawa wajinga wajinga wakati meli kama hizo toka 2021 zilikuwa zinatia nanga hapo ila kwa ushoga wako unagawa sifa tu kwa mabasha zako ambazo hawana
 
Wabongo, kwa hiyo Dar port inashusha bidhaa kwa ajili ya Tanzania tu na je, hapo kabla ya DP World kuingia, tushawahi kupata hiyo Balance of trade

Nadhani swali sahihi sio Import vs Exports Ila je, management ndio sababu ya kupokea meli kubwa au kuongezeka kwa capacity ya "bandari" Mfano kina chake katika kuhudumia meli kubwa

Na je, kazi ya magufuli ya upanuzi wa bandari setu imeleta impact gani au hii tunaoiona yawezekana ni impact yake kuliko kuingia kwa Dp World?..

Kuongeza kina cha bandari kulifanyika wakati wa Magufuli kupitia mkopo wa dola bilioni 1. Hawa DP W kunatengenezwa vihabari vya kipuuuzi na vya kijinga kwa dhamira ya kutaka kufukia ushenzi ule uliomo kwenye IGA. Lakini hilo halitawezekana.

Wangekuwa na akili, (japo tunajua rushwa kubwa iliwapofusha), wangehangaika na kubadilisha vipengere vya kihuni kwenye ile IGA ya kishenzi kuliko IGA zote Duniani.
 
Hapana mwisho ilikuwa meli ya container 2000 kwa sababu ya kina ila Dp word hawa jaongezakina wao waonekuta tayari TPA wameshaongeza kina cha bandari wao wameongeza mashine za kushusha mzigo mkubwa kwa haraka

Maersk Cubango ilipiga nanga hapo Waziri wa uchukuzi akiwa Mwakyembe ilikuwa na container 4000, tunasahau sana.

 
Ni mabadiliko gani waliyafanya kuwezesha kuleta meli kubwa ambayo sisi wenyewe tulishindwa kuyafanya?

Hakuna mabadiliko yoyote, wanacheza na ujinga wa watu. Kina cha bandari kiliongezwa wakati wa maboresho ya bandari yaliyofanyika wakati wa awamu ya 5 kwa mkopo wa dola bilioni 1.

Mioyo yao inahangaika baada ya ujambazi wao walioufanya kupitia IGA ya kishenzi, kugundulika na umma. Kila wakati wanatengeneza hadithi za kijinga.

Hii ni sawa Serikali ijenge barabara ya lami nzuri, halafu mtu alete lorry kubwa, halafu aliyeleta lorry kubwa anaanza kujisifu kuwa uwekezaji wake mkubwa wa kuleta lorry kubwa umeleta unafuu!!
 
Iweje leo makasha 4000 mseme haijawahi kutokea? Acheni siasa za bei rahisi na ishatia nanga meli mwaka juzi ilikua na makontena 6000, acheni siasa za bei rahisi kwenye bandari mmevuruga tunawakalia kimya mnatuona mafara, mara gawio wakati tpa ishawahi kutoa gawio kubwa miaka mingi ilopita kuliko gawio lenu

Hawa makuwadi wa DP W, siyo tu wamekosa akili na uzalendo, bali wamekosa hata kumbukumbu.

Maboresho ya bandari ya Dar ikiwemo kina cha maji, ni miongoni mwa mambo mazuri na muhimu yaliyofanywa na utawala wa marehemu Magufuli. Hawa washenzi wa DPW, hakuna chochote cha maana walichokifanya. Pekee wanachodai kuwa wamefanya ambacho hakijaleta mabadiliko yoyote eti ni maboresho ya mifumo ya TEHAMA.

Niliwasiliana na afisa mmoja wa bandari mwezi May, katika kuongelea uwekezaji wa DP W, alisema kwa kifupi kuwa NI UTAPELI TU HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA.
 
Hauamini unachokisoma?

Ahsante mama Samia.

Mwehu mwingine huyu hapa.

Bandari ya Dar ilikwishawahi kupokea meli yenye makasha 5,000 mpaka 6,000. Halafu leo mafisadi wajinga wanataka waone maajabu meli ya makasha 4,000 kutia nanga bandari ya Dar.

Kama una access na afisa yeyote mtendaji wa bandari ya Dar, mwulize DPW wamefanya tangu waingie. Jibu ni HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA KILICHOFANYIKA MPAKA SASA. Wao wanadai eti wameboresha mifumo ya TEHAMA. Na wanasema hivyo kwa sababu mifumo ya TEHAMA huwezi kuiona kwa macho mpaka uingie kwenye electronic systems zao.

Majizi yanahangaika kuhalalisha uwepo wa DP W kupitia ile IGA ya kishenzi, lakini hakuna wa kudanganyika na stories za kipuuzi kama hizi.
 
Miaka 6 nyuma yaani 2018 , meli aina ya northern power ilishusha, makasha 5000, katika bandari ya Dar, siasa zenu za bei rahisi kawafanyieni watoto
Aisome FaizaFoxy hii na makuwadi wengine.
 
Unahisi? Lete facts na data hapa sio habari za kuhisi.

Meneja wa bandari mwenye mamlaka na takwimu zote za meli zilizowahi kuingia amesema hii ndio meli ya kwanza kubwa kihistoria kutia nanga bandarini hapo sasa wewe unakuja na hisia zako usiyekuwa hata na uelewa wa mambo ya bandani.

Huyo meneji atakuwa punguani au aliyepofushwa akiki na rushwa ya mwarabu.

Kumbukumbu zipo za meli zilizowahi kuketa makasha zaidi ya 4,000; halafu useme kuwa eti kuna mwehu anaitwa meneja wa bandari anasema hakuna meki kubwa kuliko hiyo ya makasha 4,000 iliyowahi kutia nanga bandari ya Dar!! Kichaa mkubwa huyo. Kweki rushwa huondoa akili na aibu.
 
Ni hii ni mwanzo tu bado mambo makubwa mazuri yanakuja.
Wenye wivu na Mama lazima watahara damu mwaka huu!!!
Kazi inaendelea.
Kama muda wa kutoa mzigo bandarini haujabadirika mpaka leo bado naona DPW wanayo kazi ngumu, kuna meli zimefika toka tarehe 13/6/2024 lkn mpaka leo hazijashusha mizigo.
 
Huyo meneji atakuwa punguani au aliyepofushwa akiki na rushwa ya mwarabu.

Kumbukumbu zipo za meli zilizowahi kuketa makasha zaidi ya 4,000; halafu useme kuwa eti kuna mwehu anaitwa meneja wa bandari anasema hakuna meki kubwa kuliko hiyo ya makasha 4,000 iliyowahi kutia nanga bandari ya Dar!! Kichaa mkubwa huyo. Kweki rushwa huondoa akili na aibu.
Hao ni waongo tu, kuna meli zimefika 13/6 na bado hazijashusha mizigo lkn hiyo iliyofika jana eti itakaa kwa muda wa siku 5 tu. Je kwa nini meli zilizofika tarehe 17 mbona hazijapangiwa siku ya kusha?
 
Kama ni kweli dp wameleta mabadiliko makubwa wapewe hata wizara moja nyeti hasa ya fedha na kilimo,yawezekana mambo yakawa mazuri zaidi.
 
Back
Top Bottom